CLUB YA DRAFT YAFANYA ZIARA

 Mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Mzumbe mkoa wa Morogoro, Dk Mnzava Kikonje wa pili kutoka kulia na Mwenyekiti wa klabu ya Draft ya Mosea Manispaa ya Morogoro, Hamidu Ndossa wa kwanza kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji 10 bora ambao wameondoka leo katika ziara ya kimichezo Dodoma iliyoratibiwa na klabu hiyo baada ya shindano lililoshirikisha washiriki 36 mkoani hapa. 
Mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Mzumbe mkoa wa Morogoro, Dk Mnzava Kikonje akimkabidhi zawadi ya sh15,000 Dickson Sanga baada ya kushika nafasi ya kwanza ya shindano la kusaka wachezaji 10 bora kwa ajili ya ziara ya kimichezo mkoani Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa klabu hiyo Hamidu Ndossa.PICHA/MTANDA BLOG

Jumla ya wachezaji 25 wa 
Mosea Draft Club Manispaa ya Morogoro wameondoka leo na kwenda mkoani Dodoma kwa ajili ya ziara ya kimichezo.

Mchezaji Dickson Sanga ndiye ayeibuka kidedea katika shindano la kusaka wachezaji 10 bora kwa kushika nafasi ya kwanza na kuzawadiwa zawadi ya sh15,000.

Akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi 10 bora katika makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Juwatta, Mwenyekiti wa Mosea, Hamidu Ndossa alisema kuwa katika shindano hilo mchezaji Dkickson Sanga aliibuka mshindi wa kwanza na kuzawadi sh15,000 baada ya kukusanya pointi 54.


Ndossa alisema shindano hilo lililenga kupata wachezaji 10 bora wataokwenda mjini Dodoma kwa ziara ya kimichezo septemba 7 mwaka huu huku nafasi ya pili ikichukuliwa na James Januari aliyepata zawadi ya sh10,000 kwa kupata pointi 49 wakati Ally Hamad (Dogo Ally) akishika nafasi ya tatu kwa pointi 47 na kupata zawadi ya sh5,000.


Ndossa alisema safari hiyo imeratibiwa na mfadhili mkuu mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Mzumbe mkoa wa Morogoro Dk Mnzava Kikonje.


“Tuna ziara ya kimichezo mjini Dodoma septemba 7 mwaka huu lakini kutokana na wachezaji wengi wakali katika mchezo wa draft ilituwia vigumu kuteua timu na tulichofanya ni kuendesha shindano lililoshirikisha washiriki 36 na kati yao 10 tu ndiyo waliohitaji lakini mshindi wa kwanza hadi wa tatu wamepatiwa zawadi.”alisema Ndossa.


Ndossa aliwataja wachezaji waokwenda Dodoma ni pamoja na a George Lyimo, Sebastian Mkiunde a.k.a Bang’ara, Kimosa Rashid, Haroun Hassan, Said Nyange.


Wengine ni Shabaan Kipa na Innocent Mtey na kuongozwa na viongozi ikiwemo na washangiliaji 15 na kufanya idadi kuwa na msafara wa watu 25.


Mtanda Blog, Morogoro.
CLUB YA DRAFT YAFANYA ZIARA CLUB YA DRAFT YAFANYA ZIARA Reviewed by habari motto on 3:59 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.