
Kituo cha habari cha Uingereza BBC kimemtaja nyota wa timu ya taifa ya Algeria Yacine Brahimi kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2014.
Brahimi ambaye anachezea klabu ya Ureno ya Fc Porto anakuwa raia wa kwanza wa Algeria kutwaa tuzo hiyo ambayo hutolewa na BBC kila mwaka .

Yacine Brahimi ametwaa tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa Afrika .
BBC imekuwa na utaratibu wa kuandaa tuzo hizi kila mwaka ambapo kwa miaka miwili iliyopita kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure amekuwa akitawala .

Bon
Huyu Ndiye Mchezaji Bora Wa Afrika
Reviewed by habari motto
on
9:59 AM
Rating: