Ajali Arusha: Askari Polisi wagongwa na gari
Ni baada ya dereva kusimamishwa akakataa, Trafiki wakapiga simu mbele, alipofika akakutwa askari wameweka kizuizi njiani akawagonga.
Taarifa zisizo rasmi watatu wamefariki hapo hapo
Askari saba wa Jeshi la Polisi nchini,
kitengo cha Usalama
Barabarani, wamenusurika kifo kufuatia ajali
iliyohusisha gari la Polisi na gari moja binafsi mjini Arusha leo hii.
Ni baada ya
dereva kusimamishwa akakataa, Trafiki wakapiga simu mbele, alipofika
akakutwa askari wameweka kizuizi njiani akawagonga.
Taarifa ambazo bado hazijadhibitishwa na jeshi hilo zinaelewa kuwawatatu wamefariki hapo hapo.
Gari zilizohusika katika ajali hiyo,
zote ni aina ya Toyota Land Cruiser, moja likiwa ni mali ya Jeshi la
Polisi nchini, na jingine lenye namba T 549 ADM, ambalo ni mali ya
kampuni moja ya Utalii mkoani humo.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo, kupitia
taarifa fupi iliyopatikana kwenye mtandao wa kijamii unaoendeshwa na
Mabalozi wa Usalama Barabarani, taarifa ya Jeshi hilo imesomeka kama
ifuatavyo.
Ni kweli ajali imetokea na kusababisha
majeruhi 7 wakiwa ni askari wa Usalama barabarani Arusha. Chanzo cha
ajali ni mwendokasi wa dereva hatimaye kushindwa kumudu gari na
kusababisha gari kuhama njia na kugonga gari la Polisi lililokuwa
linakuja mjini Arusha.
Dereva alikuwa amelewa na kwa kiwango
kikubwa baada ya kupimwa. Majeruhi walipelekwa Serian hospita kwa
matibabu, majeruhi wanne wameruhusiwa na watatu wamelazwa na wanaendelea
vizuri.

KAMA HUJAONAILE VIDEO CHAFU YA ZARI THE BOSS LADY ILIYOVUJA BONYEZA HAPA CHINI==>>>
Ajali Arusha: Trafiki Saba, wanasurika kifo, gari la Polisi lagongwa
Reviewed by
habari motto
on
7:16 AM
Rating:
5