KADA wa Chama cha Mapinduzi na Waziri wa zamani Dk. Hans Kitine jana alichukua fomu za kuwania Urais na kusema akikosa Rais haumwi hata kidogo kwanza hakuutaka wamemlazimisha tu.
Akizungumza jana baada ya kuchukua fomu alisema ameamua kugombea Urais kutokana na kulazimishwa ndiyo maana hata akikosa hawezi kuumwa.
Alisema yeye si kama wagombea wengine wanaosema kuwa wameoteshwa ili kuweza kugombea.
“Nikiukosa Urais siwezi kuumwa hata kidogo kwanza sikuutaka wamenilazimisha tu” alisema
Aidha alisema Rais anayekuja awe na uadilifu wa asili kwani mtu fisadi na mla rushwa anaonekana tu.
Pia alitaka kufanyika kwa midahalo kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza
“Nikiwa Rais nitapitisha sheria wabunge wazungumze lugha zote mbili, ni lugha ambazo zinatumika kimataifa”.
“Ni lazima viongozi wajue Kiingereza vizuri na si kubahatisha bahatisha tu
Pi alitaka wgombea wote kupimwa afya zao.
“Sikuwahi kuoteshwa kugombea Urais” alisema
Pia alisema alilazimika kuingia kwenye siasa kutokana na shinikizo la watu waliomtaka kuwa kiongozi.
“Sikuoteshwa wala kufanya chochote nilifikiria kuendelea na utaalam tu kwani nilisoma nikiwa yatima ila nilipata presha za kunitaka niwe kiongozi.
“Nikinyimwa urais siumwi hata kidogo ni presha za watu tu hata mkininyima na sijawapa hela yoyote sawa, lakini hakuna thamani ya fedha unaweza kuipa kura yako, kura yako ina thamani zaidi ya fedha” alisema
“Mimi ni msomi niliyetaka kuandika vitabu lakini nilipata msukumo wa kugombea Urais”
Aliwataka watanzania kumchagua kwani ni msomi aliyesoma nje ya nchi.
“Mimi sio mwanasiasa nilikuwa ni mtaalam wakaja wanasiasa wakanishawishi nigombee Ubunge” alisema.Aliwahi kumwambia baba wa taifa kuwa akisoma na kurudi nchini atakuja kufundisha na aliporudi kweli alifundisha.
“Nimeamua kugombea ili kusaidia kuijenga nchi” alisema.
Alijiuzulu kutoka Waziri wa Nchi Ofisi ya rais Utawala bora, Mkapa alimteua kuwa waziri wa kwanza baada ya tume ya Jaji Warioba kumchunguza juu ya mianya ya rushwa.
Alisema jambo llililomsikitisha ni baada ya alisema alikuwa mkuu usalama kwa muda mrefu lakini mtu anayechukia rushwa hasemi hata mara moja.
“Wanaochukua rushwa hawasemi wanasema watu wengine, nachukia sana rushwa na ufisadi
Alisema watu hawamchukii kwa sababu ana sura mbaya bali kutokana na tabia yake ya kusema ukweli.
Amekuwa mwanachama wa CCM tangu akiwa shuleni, alikuwa ni kati ya wanafunzi waliofukuzwa na baba wa taifa.
Alisema sasa nchi inavurugwa na mambo ya kipuuzi lakini sasa watanzania wamekuwa wabaya zaidi ya wanyama.
Source: Sifa Lubasi,Dodoma
Hata Nikiukosa Urais Siumwi,
Reviewed by habari motto
on
11:40 PM
Rating:
Reviewed by habari motto
on
11:40 PM
Rating:
