Mbunge Wa Arusha Mjini Apatwa Na Ajali

Mbunge wa Arusha mjini, Mhe.Godbles Lema amepata ajali ya gari alasiri hii. Ajali hiyo imetokea katika eneo la Burka, karibu na Uwanja wa ndege wa Arusha. Alikuwa akielekea bungeni-Dodoma.

Gari lake-Land Cruiser limegongana na Suzuki. Magari yote mawili yameumia vibaya, hasa Suzuki, kiasi cha kutoamini kama kuna mtu katoka salama. Hata hivyo Mungu ni mkubwa, Mbunge, Dereva wake na watu wengine wako salama.

Ameahirisha safari, amerejea mjini kwa taratibu nyingine, ikiwa ni pamoja na kucheki afya hospitali.

Mbunge Wa Arusha Mjini Apatwa Na Ajali Mbunge Wa Arusha Mjini Apatwa Na Ajali Reviewed by habari motto on 7:16 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.