Messi Aweka Historia Mpya Soka La Argentina.

ArgentinaHiguain amefunga goli pekee lililoipeleka Argentina kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Copa America inayozidi kushika kasi huko Chile. Goli la Argentina limefungwa mapema kipindi cha kwanza dakika ya 11, goli hilo liliipa Argentna ushindi wa goli 1-0 mbele ya Jamaica ‘Reggae boys’ ambao hawajashinda mchezo wowote kwenye kundi B.
Ushindi huo unaifanya Argentina kumaliza ikiwa kinara wa kundi B na huenda ikakutana na Ecuador, Peru au Venezuela kwenye mtanange wa robo fainali utakaopigwa siku ya Ijumaa.
Argentina 4Nyota wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi alicheza mechi yake ya 100 akiwa ndani ya uzi wa Argentina akiisaidia timu yake kufuzu na kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali. Messi ambaye mpaka sasa bado hajatwaa taji lolote akiwa na timu yake ya taifa licha ya mafanikio makubwa aliyopata kwenye ngazi ya klabu, mafanikio makubwa aliyopata akiwa na timu ya taifa ni kuifikisha timu hiyo kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka jana dhidi ya Ujerumani lakini timu yake iliambulia kichapo na kombe hilo likaenda Ujerumani.
Argentina 5Mchezo wa kwanza wa kundi B uliikutanisha Uruguay dhidi ya Paraguay ambapo pambano hilo lilimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya kufungana goli 1-1 lakini Uruguay wamekata tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo.

Jose Gimenez alianza kuifungia Uruguay goli la kuongoza dakika ya 29 ya mchezo lakini Lucas Barrios aliisawazishia Paraguay goli hilo japo sare hiyo haijawasaidia Paraguay kusonga mbele kwenye mashindano hayo makubwa kwa bara la Amerika ya Kusini.
Messi Aweka Historia Mpya Soka La Argentina. Messi Aweka Historia Mpya Soka La  Argentina. Reviewed by habari motto on 9:34 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.