Results for "TECHNOLOGY"

Hii Ndiyo Sababu Ya Sumsung Galaxy Note 7 kurudisha gharama Kwa Wateja

1:57 PM
Kampuni ya Sumsung Afrika Mashariki (SEEA) imetangaza kuwabadilishia simu au kuwarudishia gharama zao wateja wote walionunua simu za Samsung Galaxy Note 7 popote duniani.
Hatua hiyo imefuata baada ya kubainika kwamba simu hizo ni hatari kwa sababu betri zake zinalipuka. Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopiga marufuku uingizaji wa simu hizo nchini kwa sababu za kiusalama.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye vyombo vya habari, watu walionunua simu hizo watabadilishiwa na kupewa simu ya Galaxy S7 au Galaxy S7 Edge au Galaxy Note 5 na watarudishiwa gharama za ziada.
Mbali na kuwabadilishia simu, kampuni hiyo imefafanua kwamba wateja wanaotaka kupewa fedha taslimu watarudishiwa fedha kamili walizonunulia Samsung Galaxy Note 7 kama wana uthibitisho wa risiti.
Hii Ndiyo Sababu Ya Sumsung Galaxy Note 7 kurudisha gharama Kwa Wateja Hii Ndiyo Sababu Ya Sumsung Galaxy Note 7 kurudisha gharama Kwa Wateja Reviewed by habari motto on 1:57 PM Rating: 5

Hii Ni Picha Ya Kwanza Ya Sayari Ya Jupiter

1:15 PM
JupiterImage copyrigh
Image captionPicha ya kwanza ya sayari ya JupiterChombo cha anga za juu cha shirika la Marekani la NASA kilichopewa jina Juno kimetuma picha za kwanza za sayari ya Jupiter.
Moja ya hizo, iliyotolewa na NASA Jumanne inaonesha sayari hiyo ikiwa imezungukwa na miezi mitatu kati ya miezi yake minne mikubwa.
Miezi inayoonekana ni Lo, Europa na Ganymede. Mwezi huo mwingine uitwao Callisto hauonekani.
Picha hiyo ilipigwa Jumamosi sayari Juno ilipokuwa inazunguka sayari hiyo ikiwa umbali wa maili milioni tatu.
Hata katika umbali huo, Shimo Jekundu, lililosababishwa na dhoruba kali kwenye sayari hiyo karne nyingi zilizopita, linaonekana.
JunoImage copyrigh
Image captionWataalamu wa Nasa wakisherehekea kufika kwa Juno mzingo wa Jupiter
Juno iliingia katika mzingo wa Jupiter wiki iliyopita na kuanza kuizunguka sayari hiyo ambalo pia hufahamika kama Zohali au Zozali.
Safari yake kutoka duniani hadi ilichukua miaka mitano.
Juno itachunguza na kupeleleza sayari hiyo kwa miezi 20, lengo kuu likiwa kusaidia wanasayansi kubaini asili ya sayari hiyo ambayo wanaamini inaweza kuwasaidia kuelewa zaidi asili ya mfumo wa jua.
Chombo hicho cha juu kilipokuwa kinaikaribia Jupiter, kamera zake na mitambo mingine muhimu vilizimwa kuzuia visiharibiwe na miali nururishi. Baadaye, vilifunguliwa.
JunoImage copyrigh
Image captionPicha za karibu zaidi za Jupiter zinatarajiwa mwezi ujao
Wanasayansi wanatarajia picha za karibu zaidi za Jupiter zitapokelewa mwezi ujao.
  • Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na uzito wake ni mara 300 zaidi
  • Sayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja huko hudumu saa 10.
  • Muundo wake ni kama wa nyota , sana haidrojeni na helium.
  • Nasa inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018.
Hii Ni Picha Ya Kwanza Ya Sayari Ya Jupiter Hii Ni Picha Ya Kwanza Ya Sayari Ya Jupiter Reviewed by habari motto on 1:15 PM Rating: 5

WhatsApp Yawaponza Ndugu, Wapandishwa Kizimbani

10:39 AM
 
WATU wanne wakiwemo ndugu watatu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kusambaza taarifa za uongo kwenye mtandao wa Whatsapp, kuwa nchi inaingia kwenye machafuko wakati wa uchaguzi. 

Washtakiwa hao Leila Sinare (36), pamoja na ndugu watatu, Godfrey Soka (45), Deo Soka (40) na Monica Soka (32), walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha. 

Wakili wa Serikali Wankyo Simon akisaidiwa na Wakili Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Johannes Kalungura, alidai kati ya Oktoba 20 na 30 mwaka huu, kupitia mtandao wa Whatsapp, Leila alisambaza ujumbe wa sauti uliokuwa na taarifa za uongo zenye lengo la kupotosha jamii. 

Alidai ujumbe huo ulikuwa unasema “ Ndugu zangu wa kigango cha siasa, hakuna cha kutakiana uchaguzi mwema wala nini, nchi yetu inaingia kwenye machafuko muda wowote kuanzia sasa hivi na kama tulivyoambiwa nchi hii itageuka kuwa nchi ya vita, ni kweli imeingia kwenye vita.” 

Taarifa hiyo inaeleza “maboksi yenye kura feki yamekamatwa, Jimbo la Vunjo yamekamatwa matatu, tumekamata maboksi matatu yenye kura feki Moshi mjini, maboksi sita Ilemela, Maboksi 12 Hanang, kwa kifupi uchaguzi umeshavurugika na Tanga nasikia magari yamesimama sehemu, makamanda wetu bado wanaendelea kufuatilia lakini inasemekana ni maboksi ya kura na mpaka sasa hali siyo nzuri.” 

Aidha, taarifa hiyo inaendelea kueleza “ CCM wameingiza kura nyingi feki na niseme kutokana na hali halisi ambayo ipo hatuponi kwa sababu Mwanza vijana wameshaanza kuuawa, wameshakufa vijana wanne, watano mpaka sasa hali hiyo inaendelea…, CCM jamani tunaomba mtuachie nchi kwa amani, kweli ingelipaswa kutuua angalau kwa sumu mkabaki wenyewe, msitutese, msitutese…” 

Wankyo alidai, Leila alisambaza ujumbe huo wa uongo kwa lengo la kuposha jamii kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu. 

Katika mashitaka mengine yanayowakabili, ndugu watatu Godfrey, Deo na Monica, alidai kati ya Oktoba 20 na 30 mwaka huu, Dar es Salaam, kwa pamoja walisambaza ujumbe huo kupitia mtandao wa Whatsapp, group la Soka, kwa lengo la kupotosha jamii kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu. 

Washtakiwa walikana mashitaka na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa. 

Waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini hati ya Shilingi milioni tano. Kesi imeahirishwa hadi Desemba 3 mwaka huu. 
Chanzo-Mpekuzi blog
WhatsApp Yawaponza Ndugu, Wapandishwa Kizimbani WhatsApp Yawaponza Ndugu, Wapandishwa Kizimbani Reviewed by habari motto on 10:39 AM Rating: 5

Ndege Ya Boeing 747-8 Sasa Ni jumba La kifahari Angani

8:03 AM

Sehemu ya ndani chumbani kama inavyoonekana.

Picha/Habari:- kwa msaada wa Mashirika ya Habari.
Huenda bado ujasikia juu ya baadhi ya ndege ndogo, za kati na zile kubwa zimekuja na mfumo mpya zaidi ndani ya ndege zao ikiwemo kutengeneza chumba cha kifahari ndani ya ndege kiasi cha kujiona kama upo nyumbani kwako kwenye jumba la kifahari.
rawimage-11
Ndege ya Gulfstream G650,  miongoni tu waliokuja na mfumo huo kwenye ndege yao hiyo ya usafiri wa anga kifahari, lakini kuna wachache ambao wanaweza kumudu zaidi ya hapo kwani kwa mteja atakayetaka kupata daraja la ndege hizo atahitaji tiketi za VIP, kwa bei kubwa zaidi.
rawimage-13_1
Hata hivyo, mahitaji ya tiketi,  Airbus na Boeing wameanza kuuza “VIP” matoleo ya ndege yao chini ya Airbus Corporate Jet na Boeing daraja la Biashara kwa ndege ndogo Airbus A320 na Boeing 737, ambazo zimekuja hivi karibuni na mfumo huo mpya.

 
Sifa ya chumba hicho ni nyingi ila kikubwa ni pamoja na kitanda cha kifahari, sehemu ya ofisi, chumba cha chakula,  choo, sehemu ya kujipumzikia pekee, sehemu ya kuwasiliana, sehemu ya kujiliwaza na mambo mbalimbali  kama inavyoonekana pichani.
This Luxury Boeing 747-8 for the Super-Rich is a Palace in the SkyMost of us can’t afford to fly first-class, let alone buy our own jet. And even within that exclusive world, it’s a big step up from your standard private jet to a personalized Boeing 747-8. Greenpoint Technologies, of Kirkland, recently fitted out the industry’s first VIP 747-8 for a private, undisclosed client.
This Luxury Boeing 747-8 for the Super-Rich is a Palace in the SkyMost of us can’t afford to fly first-class, let alone buy our own jet. And even within that exclusive world, it’s a big step up from your standard private jet to a personalized Boeing 747-8. Greenpoint Technologies, of Kirkland, recently fitted out the industry’s first VIP 747-8 for a private, undisclosed client.
For most people, private jets such as the $65 million Gulfstream G650 or the Bombardier Global Series are the epitome of luxury air travel, but there are a select few who can afford more than that. They’re converting airliners into private flying palaces. To meet this demand, Airbus and Boeing have begun selling “VIP” versions of their airliners under the Airbus Corporate Jet and Boeing Business Jet brands. While most of these planes are based on smaller Airbus A320 series or Boeing 737 models, one recent VIP conversion took luxury to a new level.
Lounge luxury
 One very lucky, very wealthy, and very confidential client took delivery of a personalized Boeing 747-8, completed by Greenpoint Technologies of Kirkland, Washington. Its incredible 4,786 sq. ft. of space features a stateroom, lounges, an office, and a massive dining room.
Conduct business in the sky
The Greenpoint Technologies 747 is based off of a Boeing 747-8,Muonekano wa ndege hiyo kwa nje ikiwa angani..
Ndege Ya Boeing 747-8 Sasa Ni jumba La kifahari Angani Ndege Ya Boeing 747-8 Sasa Ni jumba La kifahari Angani Reviewed by habari motto on 8:03 AM Rating: 5

Hawa Ni Masta 3 waliotajwa na iPhone kumiliki simu kali zaidi Duniani ..

2:17 PM
group11
iPhone 6 wanasema huenda zikawa simu za bei kali zaidi kwa sasa duniani.
Mastaa wanapenda pia vitu vizuri na vya thamani, mfano simu za iPhone ziko mikononi mwa mastaa wengi sana hata hapa Bongo.
Kampuni ya Apple ambao ndio watengenezaji wa iPhone wamesema kuwa miongoni mwa wateja wao wakubwa duniani ni hawa; mwanariadha Usain Bolt Mjamaica, mwanasoka mstaafu David Beckham na star wa mziki P Diddy.
david-beckham-and-apple-iphone-4-gallery
Hapa Beckham alikuwa na iPhone4 yake wakati huo
Unaambiwa mastaa hao kila mmoja ana iPhone 6 ambayo imetengenezwa kwa madini ya almasi, thamani ya simu hiyo kila moja ni paundi mil. 2.3 (kama bil. 6.5 za TZ).
Hawa Ni Masta 3 waliotajwa na iPhone kumiliki simu kali zaidi Duniani .. Hawa Ni Masta 3 waliotajwa na iPhone kumiliki simu kali zaidi Duniani .. Reviewed by habari motto on 2:17 PM Rating: 5

Sasa hivi kwa kutumia Smartphone yako unaweza kufanya vipimo vya HIV na magonjwa ya zinaa.

7:00 AM
pimaTimu ya watafiti kutoka chuo cha Columbia Univesity kimebaini simu za kisasa za smartphone zinaweza kupima kwa haraka na urahisi virusi vya Ukimwi na magonjwa wa zinaa.
Kwa kutumia App ambayo una-install kwenye smartphone ama iPad, halafu unaunganisha kwenye simu kupitia tundu la kuwekea headphone, basi majibu ya vipimo hivyo yanapatikana ndani ya dakika 15!
Kifaa hicho kinapatikana kwa gharama ya Dola 34 (sawa na sh. 55,000/= Tshs).
.
Hii ni iPhone ikiwa imeungwa na kifaa hicho.
Inasemekana hadi sasa wanawake 96 kutoka Uganda wamefanyiwa vipimo kwa njia hiyo na kupata majibu yanayoridhisha na kuchapishwa kwenye jarida la masuala ya sayansi na tiba Uganda.
Chanzo:Millardayo.
Sasa hivi kwa kutumia Smartphone yako unaweza kufanya vipimo vya HIV na magonjwa ya zinaa. Sasa hivi kwa kutumia Smartphone yako unaweza kufanya vipimo vya HIV na magonjwa ya zinaa. Reviewed by habari motto on 7:00 AM Rating: 5

Teknolojia tena, unatumia camera ya simu kutafsiri neno lolote! Kuna haja ya kuuliza?

12:38 PM
G Translate
Hii itakuwa rahisi sana mtu wangu, hivi mara ngapi umeshawahi kwenda sehemu ukakutana na maandishi ambayo umeshindwa kuyaelewa?
Teknolojia imekuwa msaada kwenye mengi mtu wangu, pata picha unasafiri kwa mara ya kwanza kwenda China, unaingia mgahawani, unapewa menu imeandikwa kichina, unaanzia wapi kwanza?
Google wanatusogeza hapa, google translate app itakusaidia kama unayumia smartphone yako unaweka app hiyo halafu unaanza kuitumia, mfano unakutana na bango lenye maandishi unafungua app, unaionyesha camera ya simu kwenye maandishi hayo unapiga picha, kwenye kioo cha simu inakuonyesha maana ya neno hilo!
googletranslate
Mbali na hivyo app hiyo inaweza kukutafsiria kwa sauti hata kile ambacho mtu anakiongea, yenyewe inakupa tafsiri kwa lugha unayotaka.
Ni rahisi tu, hauhitaji kuwa na internet ili uitumie, ni app ambayo inafanya kazi hata kama huna bundle mtu wangu, inapatikana bure kwa wanaotumia android na iPhone pia.
Cheki app hiyo kwenye video hii.
Teknolojia tena, unatumia camera ya simu kutafsiri neno lolote! Kuna haja ya kuuliza? Teknolojia tena, unatumia camera ya simu kutafsiri neno lolote! Kuna haja ya kuuliza? Reviewed by habari motto on 12:38 PM Rating: 5

Sasa Nokia Imekuja Na Simu inayokaa Na Chaja Mwezi mmoja!

2:07 PM

Simu za Nokia ni moja ya simu ambazo zimekuwa na umaarufu mkubwa Duniani, mbali na hiyo hii ni moja ya Kampuni kongwe zaidi kwenye soko la bidhaa hizo.

Kuna wakati ambao umaarufu wa bidhaa za Nokia ulishuka, lakini unaambiwa kwa sasa wanakuja hivi; Nokia wametengeneza simu za Nokia 215, zitakuwa za line moja na line mbili.



Simu aina hii ina uwezo mkubwa wa kukaa na chaji mpaka mwezi mmoja kwa ile ya line moja, ya line mbili ina uwezo wa kukaa na chaji kwa siku 21, zina internet na mtumiaji ataweza kutumia Facebook na Twitter ambazo zimeungwa moja kwa moja tofauti na ilivyo kwa smartphone.

Wanakadiria kwamba zikiingia sokoni bei yake itakuwa ni dola 29, ambayo ni sawa na sh. elfu 50 kwa T’zania.

Microsoft wamepanga kuiuza simu hii Afrika, Asia, Ulaya, na Mashariki ya Kati japo hawajasema lini itakuwa sokoni.

Hii ni moja ya hatua kubwa ambazo Nokia imezipiga sokoni tangu Kampuni hiyo inunuliwe na Microsoft.
Sasa Nokia Imekuja Na Simu inayokaa Na Chaja Mwezi mmoja! Sasa Nokia Imekuja Na Simu inayokaa Na Chaja Mwezi mmoja! Reviewed by habari motto on 2:07 PM Rating: 5

Instagram Yazidi Kujaa Juu Duniani, Hizi Ni Takimu Zake Kwa Sasa

2:04 PM

Mtandao wa Instagram umetajwa kuwa na watumiaji wengi zaidi kuliko kuliko twitter. Mmiliki wa Instagram Kevin Systrom amesema instagram imefikisha watumiaji milioni 300 mpaka sasa na wanazidi kuongezeka.

Tofauti na mtandao wa twitter ambao kwa sasa unawatumiaji milioni 284 kwa mujibu wa takwimu zilizofanywa wiki 8 zilizopita.

Baada ya miaka minne toka kuanzishwa kwa mtandao wa instagram sasa Mtandao huu una zaidi ya picha na video milioni 70. Mpaka sasa Facebook inaongoza kwa kuwa na watumiaji bilioni 1.35 .
Instagram Yazidi Kujaa Juu Duniani, Hizi Ni Takimu Zake Kwa Sasa Instagram Yazidi Kujaa Juu Duniani, Hizi Ni Takimu Zake Kwa Sasa Reviewed by habari motto on 2:04 PM Rating: 5

Huawei Wazindua Simu Yao Mpya Ya Ascend 6-Inch Mate 7 Jijini Dar Es Salaam

10:42 AM
unnamedMeneja wa Kampuni ya vifaa vya teknolojia ya Huawei Tanzania, Peter Zhang (kulia) na Meneja Bidhaa wa kampuni hiyo, Joseph Lyimo (kushoto) wakionyesha simu mpya aina ya Smartphone 6-inch Ascend Mate 7 katika hafla ya uzinduzi wa simu hiyo jijini Dar es Salaam leo.unnamed1
Meneja wa Kampuni ya vifaa vya teknolojia ya Huawei Tanzania, Peter Zhang (kulia) na Meneja Bidhaa wa kampuni hiyo, Joseph Lyimo (katikati) wakionyesha simu mpya aina ya Smartphone 6-inch Ascend Mate 7 katika hafla ya uzinduzi wa simu hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Masoko wa kampu hiyo, Lydia Wangari.  
unnamed2
unnamed4Meneja Bidhaa wa Kampuni ya Huawei, Joseph Lyimo (katikati) akionyesha jinsi simu ya Ascend Mate 7 inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi huo.
Huawei Wazindua Simu Yao Mpya Ya Ascend 6-Inch Mate 7 Jijini Dar Es Salaam Huawei Wazindua Simu Yao Mpya Ya Ascend 6-Inch Mate 7 Jijini Dar Es Salaam Reviewed by habari motto on 10:42 AM Rating: 5

Facebook kuja na Kitu Kipya Kabisa ‘Facebook at Work’

1:47 PM
Facebook inaanzisha mtandao wa kijamii kwaajili ya wafanyakazi kuwasiliana na kushirikiana kuhusiana na masuala ya kazi.
facebook-front_1796837b
Facebook at Work utaonekana vile vile kama Facebook ya kawaida, lakini watumiaji watakuwa na uwezo wa kutengenesha akaunti zao binafsi.
Watumiaji watakuwa na uwezo wa kuchat na wenzao, kutengeneza mtandao wa kazi na kushare nyaraka mbalimbali.
Mtandao huo ambao tayari unatumika kwenye ofisi za Facebook, utakuwa mpinzani kwa huduma zingine kama Google Drive, Microsoft Office na LinkedIn.
Facebook kuja na Kitu Kipya Kabisa ‘Facebook at Work’ Facebook kuja na Kitu Kipya Kabisa ‘Facebook at Work’ Reviewed by habari motto on 1:47 PM Rating: 5

Samsung Tanzania Yazinduwa Simu za Galaxy Note 4

8:09 AM
Bw Sylvester Manyara, Meneja mauzo na usambazaji wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung Tanzania akielezea sifa za simu aina ya  Samsung Galaxy Note 4 kwa mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa simu hiyo Profesa Patrick J Makungu  katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na tekinolojia katika uzinduzi rasmi wa simu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Terrace Slip way.
Bw Sylvester Manyara, Meneja mauzo na usambazaji wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung Tanzania akielezea sifa za simu aina ya Samsung Galaxy Note 4 kwa mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa simu hiyo Profesa Patrick J Makungu katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na tekinolojia katika uzinduzi rasmi wa simu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Terrace Slip way.
Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielectroniki ya Samsung Tanzania, akimkabidhi mshindi wa bahati nasibu Bw Ibrahim Bukenya katika uzinduzi rasmi wa simu ya Samsung Galaxy Note 4
Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielectroniki ya Samsung Tanzania, akimkabidhi mshindi wa bahati nasibu Bw Ibrahim Bukenya katika uzinduzi rasmi wa simu ya Samsung Galaxy Note 4
Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielectroniki ya Samsung Tanzania akizindua rasmi simu ya Samsung Galaxy Note 4.
Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielectroniki ya Samsung Tanzania akizindua rasmi simu ya Samsung Galaxy Note 4.
Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Tanzania, akielezea sifa za simu aina ya  Samsung Galaxy Note 4 kwa mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa simu hiyo Profesa Patrick J Makungu  katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na tekinolojia katika uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Terrace Slip way.
Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Tanzania, akielezea sifa za simu aina ya Samsung Galaxy Note 4 kwa mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa simu hiyo Profesa Patrick J Makungu katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na tekinolojia katika uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Terrace Slip way.
Bw John Paul, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Kielectroniki ya Samsung Afrika Mashariki akielezea sifa za saa ya Samsung Gear S kwa mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa simu ya Galaxy Note 4, Profesa Patrick J Makungu  katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na tekinolojia na  Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Tanzania,  katika uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Terrace Slip way.
Bw John Paul, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Kielectroniki ya Samsung Afrika Mashariki akielezea sifa za saa ya Samsung Gear S kwa mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa simu ya Galaxy Note 4, Profesa Patrick J Makungu katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na tekinolojia na Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Tanzania, katika uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Terrace Slip way.
Mwanamuziki, Vanessa Mdee akiwaonyesha wageni waalikwa saa ya Samsung Gear S kwenye uzinduzi wa simu ya Samsung Galaxy Note 4.
Mwanamuziki, Vanessa Mdee akiwaonyesha wageni waalikwa saa ya Samsung Gear S kwenye uzinduzi wa simu ya Samsung Galaxy Note 4.
Kutoka Kushoto, Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Tanzania, Bw Sylvester Manyara, Meneja mauzo na usambazaji wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung Tanzania, hiyo Profesa Patrick J Makungu  katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na tekinolojia na Bw John Paul, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Kielectroniki ya Samsung Afrika Mashariki wakiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa simu ya Samsung Galaxy Note 4 uliofanyika katika ukumbi wa Terrace Slip way.
Kutoka Kushoto, Bw. Mike Seo, Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Tanzania, Bw Sylvester Manyara, Meneja mauzo na usambazaji wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung Tanzania, hiyo Profesa Patrick J Makungu katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na tekinolojia na Bw John Paul, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Kielectroniki ya Samsung Afrika Mashariki wakiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa simu ya Samsung Galaxy Note 4 uliofanyika katika ukumbi wa Terrace Slip way.
BAADA ya kusubiriwa miezi kadhaa, Kampuni ya kielektroniki ya Samsung Tanzania imeongeza rasmi mwanafamilia mpya katika simu aina ya Note. Tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Terrace, Slipway ni alama ya uzinduzi rasmi na upatikanaji wa Samsung Galaxy Note 4 katika soko Tanzania.
Tukio hilo la uzinduzi lilijumuisha watu mashuhuri ndani ya Mkoa wa Dar es salaam ambao walipata nafasi za VIP. Watu hao ni pamoja na uongozi wa Kampuni ya Samsung, Viongozi wa Serikali, wasambazaji wa Samsung, waandishi wa habari, wadau na watu maarufu.
Kama Simu nzuri na ya kisasa ya mwaka Samsung Galaxy Note 4 inatazamiwa kuteka soko Tanzania. Simu hiyo imetengenezwa kutokana na maoni na marejesho ya watumiaji. Na pia inadhihirisha na ni ushahidi wa maendeleo na uwezo wa kiteknolojia wa akili ya kisasa. Miongoni mwa sifa zake nyingi inakuja na S pen iliyoboreshwa zaidi. Katika simu mpya ya Samsung Galaxy Note 4, S pen imeimarishwa na kufanya kuandika kuwa halisi zaidi.
Pia simu hiyo ina brush ambayo umfanya mtumiaji kuhisi kama anaandika kwenye karatasi. Air commands inayopatikana kwenye simu pia, umruhusu mtumiaji kutengeneza mahudhui kwa urahisi zaidi. Photo Note, inaruhusu mtumiaji kuchukua picha ya maandishi kutoka sehemu flani na kubadili maandishi hayo katika S Note.
Kwenye Uzinduzi wa Samsung Gallaxy Note 4, Meneja mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania Mr Mike Seo, aliongelea furaha waliyonayo katika kuzindua simu hiyo. Pia Aliezelea safari yao ya utengenezaji wa simu aina ya Note iliyoanza mwaka 2011 ampapo wataalamu wa viwanda waliwashauri kuwa”Hakuna mtu atayeweza kununua simu za kisasa zenye kioo kikubwa”. Mabadiliko ya mahitaji ya watumiaji yameifanya kampuni ya Samsung kuendelea kubaki kama kiongozi kwenye utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki. Kutokana na simu za Gallaxy Note kufanya vizuri sokoni, makampuni yaliyokuwa yakiwakatisha tamaa yanafuata nyayo zao pia.
Simu hii sio tu ongezeko jingine katika familia ya Note bali pia ni mwenza wa maisha ya kisasa ya watanzania. Kampuni ya vifaa vya kielektroniki inadhihirisha uthamini na kujitoa kwao kwa wateja wao katika utengenezaji wa Gallaxy Note 4 kwani ujio wa simu hii umetokana na muunganiko wa maoni na mrejesho wa watumiaji na pia ukuaji wa technolojia umechangia katika utengenezaji wa simu hii.
Katika kumalizia kuelezea kazi ya simu hiyo, Mr. Seo anasema ”Simu ina nguvu ya kufanya hisia zako kuwa za kidigtali” Imeundwa kwa fremu nzuri ya chuma na mfumo wa kitechnolojia wa 4.4 Android (Kitkat) pia ina pen na karatasi vinavyoendana na utamaduni wetu. Ina kioo chenye upana wa 15mm.
Uzinduzi wa simu hii ulitanguliwa na kampeni ya pre oder wiki mbili zilizopita. Wateja walipata nafasi ya kuweka oda ya simu hiyo. Kampeni hiyo itawawezesha wateja 100 kujipatia zawadi ya Gia S. Gia S ni saa ya kisasa ya kampuni ya Samsung. Saa hii ina fanya kazi kipekee mbali na simu, inampa mtumiaji uwezo wa kupiga simu. Saa hii ina fanya kazi kipekee mbali na simu, inampa mtumiaji uwezo wa kupiga simu, kutuma meseji, ina blututhi na pia ina 3G Wi-Fi inayoweza kumuunganisha mtumiaji kwenye mtandao
Tukio la uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 4 halikuwa kwaajili ya kutambulisha simu hiyo katika soko la Tanzania pia ilikuwa ni sherehe ya mafanikio ya Samsung.
Waliohudhuria katika tukio hilo ni, Katibu mkuu wa mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na technolojia, Patrick J Makungu. Katibu huyo ameipongeza kampuni ya Samsung kwa kusaidia kukuza technohama nchini Tanzania. Kampuni hii imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika wizara kutokana na biashara yake sio tu kwa kukuza uchumi wa nchi bali pia imesaidia kukomesha bidhaa bandia nchini.
Professor Patrick anaongeza kuwa” Vifaa hivi vinatengeneza maisha yetu ya kila siku, tunavitumia kazini na nyumbani pia. Pia vinawakilisha jamii ya kitanzania ya kisasa kama kwingineko duniani wanavoendana na technolojia. Simu ina mchango mkubwa kwa kiwanda, chanzo kikuu cha mawasiliano kwa wafanya biashara, wawekezaji na watanzania wote kwa ujumla.
Simu hii ya kisasa inapatikana kwa Tsh 1,500,000/- inakuja na bandle ya Vodacom ya 5GB worth. Simu mpya ya kisasa ya Galaxy Note 4 itapatikana katika maeneo yafuatayo.
Maduka ya Samsung Dar es Salaam: Samsung Mlimani city, Samsung NHC House, Samora Avenue, Samsung JM Mall, Samora Avenue. Mwanza: Samsung Mwanza along barabara ya Nyerere. Arusha: Samsung Arusha barabara Themi, Barabara ya Sokoine na Agakhan. Dodoma: Samsung Dodoma barabara ya Nyerere.
Vodacom Shops
Vodashop Mlimani City, Vodashop NHC (Dsm), Vodashop Oysterbay (Dsm), Vodashop Quality Centre, Vodashop Arusha na Vodashop Mwanza. Kwa kumalizia Bw Mike Seo anatoa wito kwa watanzania kupitia kwenye duka la Samsung ya lililopo ili kujipatia hicho anachoahidi kuwa” uzoefu mzuri usiosaulika kutoka kwa Galaxy Note 4”
Kuhusu Samsung Electronics Co. Ltd 
Samsung Electronics Co, Ltd ni kampuni ya kimataifa inayoongoza katika teknolojia na kufungua fursa mpya kwa watu kila mahali. Kwa njia ya uvumbuzi na ugunduzi, unabadilisha ulimwengu wa TV, simu za kisasa, Tablet, Kompyuta, kamera, vyombo vya nyumbani, Printa, mifumo ya LTE, vifaa vya tiba, semiconductors and LED solutions. Tumeajiri watu 286,000 katika nchi 80 na mauzo ya kila mwaka ni $ 216,700,000,000.
Kujua zaidi tafadhali tembelea www.samsung.com.
Samsung Tanzania Yazinduwa Simu za Galaxy Note 4 Samsung Tanzania Yazinduwa Simu za Galaxy Note 4 Reviewed by habari motto on 8:09 AM Rating: 5

Instagram Yafanya Maboresho

9:59 AM

Wale watumiaji wa mtandao wa kupost picha maarufu kama instagram, sasa tatizo lao nimepatiwa ufumbuzi baada ya kuweka update mpya katika app hiyo ya kuweza kuedit caption, mwanzoni watumiaji walikuwa wakishindwa kuedit maandishi yanayoendana na picha baada ya kupost hivyo wakati mwingine kupelekea kuweka makosa na kushidwa kufanya masahihisho ya makosa hayo.
Baada ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa watumiaji hatimaye Instagram wameweka update kwa watumiaji wa iOS na Android, update App yako sasa kupata mabadiliko hayo mapya.
Instagram Yafanya Maboresho Instagram Yafanya Maboresho Reviewed by habari motto on 9:59 AM Rating: 5

NA HIZI NI SABABU ZA MWANZILISHI WA KAMPUNI YA APPLEKUWAZUIA WATOTO WAKE KUTUMIA BIDHAA ZAKE

4:09 PM
Bidhaa za kampuni ya Apple zina mashabiki na wateja wengi duniani, hii inathibitishwa na foleni kubwa ya watu waliojitokeza kwenye vituo mbalimbali duniani kununua toleo jipya la iPhone6.
Tumesikia watu wakiachana ama familia zikitengana kwa sababu tu baba ameshindwa kununua bidhaa za kielekroniki za kampuni ya Apple. Mwaka jana familia moja nchini China iliwauza watoto wao ili kupata pesa ya kununua iPhone5.
Kwa kuzingatia hayo, huenda ukadhani watoto wa mwanzilishi wa kampuni ya Apple na mgunduzi wa bidhaa hizo, Steve Jobs wanafaidi zaidi bidhaa hizo.
Na huenda ukadhani hata kuta za nyumba yao zingeweza kuwa za mfumo wa simu za kisasa za kupangusa ‘Screen Touch’ na mawasiliano ya hali ya juu ndani ya nyumba hiyo kwa mfumo huo.
Lakini ukweli ni kwamba, marehemu Steve Jobs hakuwaruhusu hata kidogo watoto wake kutumia iPhones, iPods wala iPads nyumbani kwake.
Katika article iliyoandikwa na New York Times wiki hii, mwandishi wa habari Nick Bilton ameeleza jinsi ambavyo alishangaa majibu ya Steve Jobs alipomuuliza jinsi ambavyo watoto wake wanapenda bidhaa za kampuni hiyo.
“Hawajawahi kutumia kabisa. Tunadhibiti kiasi ambacho watoto wetu wanatumia teknolojia nyumbani.” Alijibu Steve Jobs.
Nae mwandishi maalum wa Steve Jobs, Walter Isaacson ambaye alikuwa akitumia muda mwingi nyumbani kwa boss wake huyo alithibitisha kuwa maoengezi ya uso kwa uso yalitawala katika nyumba hiyo.
“Kila jioni Steve alikuwa akipata chakula cha usiku na familia yake kwenye meza kubwa jikoni, wakijadili vitabu na historia na vitu vingine vingi. Hakuna mtu aliyekuwa na iPad au computer. Watoto hawakuonekana kuwa addicted hata kidogo na vifaa hivyo.” Alieleza Isaacson.
Inaelezwa kuwa hata Steve Jobs hakuwa na tabia ya kutumia vifaa hivyo kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Steve Jobs aliyefariki mwaka 2011 sio mtu maarufu pekee aliyeamini katika kuweka sheria kali kwa watoto wake kutumia vifaa hivyo, Chris Anderson, mhariri wa zamani wa Wired pia alieleza kuwa yeye na mkewe wamewazuia watoto wao kiasi kwamba watoto hao huwalalamikia sana wakilinganisha na uhuru wanaouona katika familia za mafiki zao.
Utafiti uliofanywa katika eneo la Chuo Kikuu cha California, Los Angeles na kuchapishwa hivi karibuni unaonesha kuwa siku chache baada ya kuzuia watoto kutumia vifaa vya kieletroniki vya simu, ufaulu wa watoto katika masomo ulipanda ghafla.
Utafiti unaonesha kuwa kwa wastani watoto nchini Marekani hutumia zaidi ya saa saba na nusu kwa siku katika matumizi ya simu za kupangusa na vifaa vingine vya kielekroniki kama iPads, iPod n.k.
Uamuzi ni wako, kumnunulia mwanao vifaa vya hivyo au kumuweka mbali na mapinduzi hayo ya kiteknolojia.

NA HIZI NI SABABU ZA MWANZILISHI WA KAMPUNI YA APPLEKUWAZUIA WATOTO WAKE KUTUMIA BIDHAA ZAKE NA HIZI NI SABABU ZA MWANZILISHI WA KAMPUNI YA APPLEKUWAZUIA WATOTO WAKE KUTUMIA BIDHAA ZAKE Reviewed by habari motto on 4:09 PM Rating: 5

KUWA WA KWANZA KUIONA BIDHAA MPYA YA APPLE - I WATCH

12:27 PM
Kampuni ya Apple imezindua saa mpya aina ya smartwatch ijulikanayo kama 'The Apple Watch'.
Huu ni uzinduzi wake wa kwanza wa bidhaa nyinginezo nzuri tangu kufariki kwa mwanzilishi wa kampuni hiyo Steve Jobs.
Saa hiyo inatumia programu na pia ni kama kifaa cha kumsaidia mtu kujiweka katika hali nzuri ya kimwili kwa kuangalia mazoezi anayofanya na hata kumshauri mtumiaji, kwa kuwasiliana na simu yake ya iPhone.
Wakati simu nyingine kama hizo tayari zikiwa sokoni, wataalamu wanasema kuwa kampuni ya Apple ina historia ya kuingia katika sekta mbali mbali kwa kuchelewa lakini kikubwa ni kuwa huwa inabadilisha teknlojia na kuja na vitu vipya.
Apple pia ilizindua simu zake mbili mpya ambazo ni kubwa ikilinganishwa na simu zake za awali.
Skirini ya iPhone 6 ina upana wa nchi 4.7 huku iPhone 6 Plus ikiwa na skrini yenye nchi 5.5.
Haya ni mabadiliko ambayo wadadisi wanasema inawazuia wateja wa Apple kuhamia kwenye simu zenye mfumo wa Android.
Kampuni hiyo pia ilitangaza, huduma mpya ijulikanayo kama Apple Pay, ambayo mkurugenzi wake anasema wanatumai itakuwa kama mfuko wa mtu kubeba pesa.
Saa ya Apple ina sura 11 na huruhusu mtumiaji kubadili mikanda yake.
KUWA WA KWANZA KUIONA BIDHAA MPYA YA APPLE - I WATCH KUWA WA KWANZA KUIONA BIDHAA MPYA YA APPLE - I WATCH Reviewed by habari motto on 12:27 PM Rating: 5

KUWA WAKWANZAKUIONA I-PHONE 6 MPYAA

8:24 AM
iPhone 6 isn’t simply bigger — it’s better in every way. Larger, yet dramatically thinner. More powerful, but remarkably power efficient. With a smooth metal surface that seamlessly meets the new Retina HD display. It’s one continuous form where hardware and software function in perfect unison, creating a new generation of iPhone that’s better by any measure.
KUWA WAKWANZAKUIONA I-PHONE 6 MPYAA KUWA WAKWANZAKUIONA I-PHONE 6 MPYAA Reviewed by habari motto on 8:24 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.