NAKUMATT YAZIDI KUTANUA MIPAKA YAKE YAFUNGUA TAWI LA KWANZA DAR ES SALAAM, YAPANGA KUFUNGUA MENGINE MAWILI



Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt Holdings, Atul Shah akimuonesha baadhi ya bidhaa Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene wakati wa ufunguzi huo leo



 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene akiangalia bidhaa wakati wa ufunguzi
huo leo



Wafanyakazi wa Nakumatt Mlimani wakifurahia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mall hiyo
Mlimani City jijini Dar es salaam leo


Furaha ya kuanza kazi Nakumatt Mlimani leo.

KAMPUNI ya Nakumatt Holdings, imezindua rasmi tawi la kwanza kati ya matawi yake matatu
makubwa nchini Tanzania ambayo awali yalimilikiwa na Kampuni ya Shoprite ya Afrika ya Kusini. 
Ikiwa ni mpango wake mpya wa kuboresha zaidi huduma zake, Nakumatt holdings, imezindua tawi hilo kubwa ambalo litakuwa utambulisho muhimu wa huduma zake katika eneo la biashara la
Mlimani City litakaloitwa Nakumatt Mlimani. Tawi hilo la 48 la Nakumatt limepambwa kwa rangi na mwonekano wa alama za Nakumatt na kwa ubunifu wa hali ya juu.
Pamoja na Nakumatt Mlimani, kampuni hiyo pia iko mbioni kuzindua tawi lengine kubwa
litakalojulikana kama ‘Nakumatt Pugu Road’ jijini Dar es salaam ambako pia kutakuwa makao yake
makuu. Pia itafungua Nakumatt Arusha siku zijazo. 
 Kwa kufungua matawi yake matatu moja baada ya jingine, Nakumatt pia itakuwa imefikisha
matawi 50 katika mtandao wake wa huduma za uuzaji bidhaa na hivyo kutekeleza mkakati wake
wa maendeleo ambao ulizinduliwa mwaka 2011.
 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka lake la kwanza in Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji
wa Nakumatt Holdings, Atul Shah alisema kufunguliwa kwa matawi matatu mapya yaliogharimu
takriban dola za Marekani milioni 3 ni sehemu ya mpango wa upanuzi wa huduma za uuzaji
bidhaa katika kanda ya Afrika.
Kutokana na uzinduzi wa Tawi la Nakumatt Mlimani, Shah alisema kuwa Nakumatt sasa ina
maduka mawili makubwa yanayofanya kazi nchini Tanzania. 
Nakumatt Mlimani inaungana na duka jingine la la Nakumatt Moshi lililofunguliwa mwaka 2011
katika mji huo ambako kuna Mlima Kilimajaro. 
”Uzinduzi wa Nakumatt Mlimani ni ndoto ya muda mrefu ambayo sasa imekuwa kweli ambapo
tumekuwa tukifikira mahali pa kuweka duka letu jijini Dar es salaam na maeneo mengine nchini
Tanzania,” alisema Shah na kuongeza:
“Uzinduzi huu pia ni hatua nzuri itakayopelekea uzinduzi mwingine wa duka letu la 50 katikati ya
Agosti ambapo tutakuwa tumefanikiwa kufikia malengo yetu tuliyojiwekea kuyafikia Februari
mwakani.”
Maduka matatu ya Shoprite yalifungwa mwezi uliopita ili kufanikisha kazi ya kuyaboresha zaidi
sambamba kwa kuzingatia viwango na uzoefu wa Nakumatt. 
Pia Nakumatt inatarajia kufungua matawi mengine matatu ya biashara nchini Kenya kabla ya
mwisho wa mwaka huu.
 Pia kampuni hiyo itakuwa na duka kubwa katika eneo kubwa la kifahari la Green Square mjini
Kericho nchini Kenya.
Shah alisema Nakumatt ina mkakati wa kukuza biashara wa kampuni ambao unategemea zaidi
uwepo wa vitega uchumi ambapo kampuni inaweza kuendesha shughuli zake za maduka ya
supermaketi. Shah aliongeza kwa kusema:
 “ Kwa sasa tunaendesha shughuli zetu katika nchi 12 na tunashirikiana na wamiliki wa maeneo ya
biashara nchini Kenya ambao wanaweza kutoa huduma za kujenga maeneo ya maduka makubwa
katika maeneo ya Machakos, Nyeri, Kajiado, Garissa, Embu, Naivasha,Narok Busia and Homabay.” 
Ili kutimiza masharti ya Nakumatt, Shah aliwahimiza waendelezaji wa maeneo ya biashara na
Mameneja wa Miradi kushauriana na wataalam wa Nakumatt kuhusu namna ya kuboresha uchoraji
wa ramani na ujenzi wenye mvuto kwa wateja katika maduka ya kampuni hiyo.

Na mwandishi wetu..
NAKUMATT YAZIDI KUTANUA MIPAKA YAKE YAFUNGUA TAWI LA KWANZA DAR ES SALAAM, YAPANGA KUFUNGUA MENGINE MAWILI NAKUMATT YAZIDI KUTANUA MIPAKA YAKE  YAFUNGUA TAWI LA KWANZA DAR ES SALAAM, YAPANGA KUFUNGUA MENGINE MAWILI Reviewed by habari motto on 10:19 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.