
Wananchi wa kijiji cha mwakata katika kata ya Isaka wilayani Kahama juzi walifanya zoezi la kuwatambua
wauaji wa vikongwe kwa kuwakata mapanga kwa njia yakupiga kura baada ya vifo hivyo kuongezeka mwaka huu
Katika zoezi hilo lililosimamiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Bensoni Mpesya wananchi hao walidai
mazingira yote ya vifo vya kina mama wanaouwawa kwa kukatwa mapanga inaonyesha wauaji ni miongoni mwa wanafamilia wa marehemu hao
Kufuatia hali hiyo mkuu wa ulinzi wa jadi wa kata ya Isaka sungusungu Machimu Ndalo amesema vifo
hivyo vya kina mama kuuwawa kwa mapanga licha ya kugubikwa na imani za kishirikina lakini wengi wao ni migogoro ya urithi ikiwemo umiliki wa Ardhi
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Mpesya amewataka wananchi kupiga kura hizo za
kutambua wauaji hao kwa haki bila chuki wala kumuonea mtu na wale watakaopata kura nyingi
majina yao yatawakilishwa kwenye kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya ili wafanyiwe uchunguzi
Uamuzi wa kuanzisha kupiga kura hizo umekuja baada ya mwaka huu kwa kipindi cha miezi saba
NI MFANO WA KUIGWA:.. MKUU WA WILAYA ATUMIA MBINU HII KUWANASA WAHALIFU
Reviewed by habari motto
on
4:31 PM
Rating:
Reviewed by habari motto
on
4:31 PM
Rating: