Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na Vyombo vya habari mbalimbali mapema leo makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar kuhusiana na sakata la viungo vya binadamu vilivyokamatwa jana ambapo Kamanda Kova amesema kuwa watu wanane wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Kamanda Kova amesema kuwa jopo la Wataalamu saba limeundwa kuchunguza tukio hilo na amethibitisha kuwa viungo vile vilikuwa ni vya maiti,ambavyo hutumika na madaktari kwa elimu ya matibabu na utafiti.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA SAKATA LA VIUNGO VYA BINADAMU VILIVYONASWA DAR-ES-SALAAM..
Reviewed by habari motto
on
8:55 PM
Rating:
