Mkazi mmoja wa Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma,Bibi
Scholastica Mhagama amesema miaka mingi ameishi maisha dhiki na kunyanyaswa bila msaada kutoka kwa jamii anayoishi hali ambayo imemfanya amuombe Mungu amchukuwe ili azikwe kwenye jeneza alilojiandalia.
Bibi Scholastica akiwa kwenye jeneza alilojiandalia “Kila siku naomba Mwenyezi Mungu anichukue haraka ili nikapumzike kutokana na mateso ninayoyapata, lakini hofu yangu nikifa je, nitazikwa kama binadamu wengine? Ndiyo maana nimeamua kujitayarishia jeneza langu,” anasema Scholastica
Mhagama (76) mwenye ulemavu wa viungo anayeishi pekee yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi.
“Nimetengeneza kabisa jeneza langu siku nikifa wanizike humu. Naomba Mungu anichukue haraka ili kuepukana na mateso haya. Nimetengwa na jamii na majirani wanashindwa
kunisaidia wanadai eti mimi ni mchawi kwa sababu watoto wangu wote wanne walikufa
wakiwa wadogo. Naumia sana kusingiziwa kitu ambacho sikijui,’’ anasema kwa
masikitiko.
Bibi huyo anasema kuwa aliweza kutengeza jeneza hilo baada ya kupewa Sh40,000 na mfadhili mmoja. “Tayari nilikuwa na mbao kwangu, hivyo kazi ilikuwa
kumlipa kijana fedha na kumpa mbao ili anitengenezee jeneza,” anasema.
Source:Mwananchi
BIBI AWATAJA WALIOCHANGIA YEYE KUJITENGENEZEA JENEZA MWENYEWE
Reviewed by habari motto
on
10:28 PM
Rating: