Mtangazaji wa TV na redio ambaye pia ni muimbaji, Vanessa Mdee amesema uoga ulimfanya ashindwe kuonyesha kipaji chake mapema.
Akiongea na Bongo5 leo, Vanessa amesema muziki anaoufanya sasa hivi ni muziki aliokuwa nao miaka 4 iliyopita lakini alishindwa kuonyesha kipaji chake kutokana na kuogopa.
“Kitu ambacho kimechelewesha kuonyesha kipaji changu, I think kila kitu ni timing. Na kitu kingine ambacho nilikuwa na tatizo nacho nilikuwa sina ile confidence ya kupanda stejini, nilikuwa narekodi muziki kwa muda mefu sana, muziki ambao niko nao ni wa miaka mitatu minne lakini nilikuwa sina ile conficance ya kuitoa because in my head is was imperfect. Mimi ni mtu ambaye nataka niwe perfect,” amesema Vanessa.
“Lakini kuna mtu alinikalisha akaniambia ‘sikiliza dada muziki wako hata siku moja kwenye sikio lako hautausikia kama ni mzuri hundred % siku zote, siku zote utakuwa unajitolea kasoro, unatakiwa ukifikia asilimia 75 iachie kwasababu that’s good enough’. Mimi nikachukua huo ushauri nikawa naufanyia kazi kadri siku zinapozidi kwenda japo bado sijafikia sehemu ambayo yaani nipo confident kabisa, lakini kiasi chake nimeanza kujaribu kujiachia.”
Katika hatua nyingine Vannesa ambaye atafanya show katika jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 jijini Mwanza ameweka wazi mipango yake ya kuachia album.
“Nimekuwa kwenye mipango ya kufanya collabo na wasanii mbalimbali wa Afrika ingawa nisingependa kuliweka wazi zaidi, lakini nyimbo zinakuja na nyingine zinaweza zikaja pamoja kwenye album yangu,” amesema Vee.
“Album yangu ipo naifanyia kazi lakini haitatoka mpaka mwakani. Itakuwa inaitwa ‘Money Monday’. Mimi ninapenda sana kutengeneza album ili mashabiki wangu wapate taste ya muziki wangu na nina muziki mwingi ambao umekaa studio sasa kwa nini nisitengeneze album nikaiachia tu? Japo watu wanasema soko letu limekuwa gumu na kuna watu wanaiba muziki, mimi nimeona kuna platform mbalimbali kama Mkito. Mimi naweza nikatumia iTunes hata watu ambao wapo nje ya nchi wanaweza kupata na kusikiliza muziki wa kitanzania kutokana na platform ambazo mimi nimeweka.”
NA SABABU HIZI ZILISABABISHA VANESA MDEE KUCHELEWA KUINGIA KWENYE SANAA
Reviewed by habari motto
on
3:23 PM
Rating: