Ofisi yateketezwa kwa moto


Watu wanne wanashikiliwa na polisi mkoani Kigoma kwa tuhuma za kuchoma moto ofisi ya masijala ya Idara ya Ardhi ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuteketeza hati na nyaraka
mbalimbali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jafari Ibrahim, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Anna Fanuel (46), Makrina Paul (49), Saimon Pius (37) na Tumaini Esau (44).
Alisema Oktoba mosi, mwaka huu saa 4.15 usiku, ofisi ya masijala ya idara hiyo ilichomwa moto na kuteketeza hati na nyaraka mbalimbali. Kamanda Ibrahim alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kitendo hicho ni njama za kupoteza vielelezo Alisema kuwa uchunguzi umebaini kuwa idara hiyo imegubikwa na migogoro inayohusiana na ugawaji wa viwanja.
“Uchunguzi wetu wa awali unaonyesha watu hao walitumia mafuta ya petroli kuchoma ofisi hiyo…tunaendelea kufuatilia zaidi tukio hili,” alisema Ibrahim

Ofisi yateketezwa kwa moto Ofisi yateketezwa kwa moto Reviewed by habari motto on 11:08 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.