SIKU chache baada muigizaji nyota wa filamu nchini, Rose Ndauka kutemana na bwana wake, Malik Bandawe, Jumanne iliyopita aliangusha bonge la sherehe iliyofana ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao, Ijumaa lilikuwepo.
Msanii nyota wa filamu nchini, Jack wa Chuz akimtunza msanii mwenzake, Rose Ndauka Sherehe hiyo ya Rose, ambaye alizaliwa siku moja na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ilishuhudia mastaa wengi wa kike walioalikwa, licha ya kunywa na kula kwa kadiri walivyojisikia, lakini pia wakiwa wamevalia vivazi vilivyoonyesha sehemu kubwa ya miili yao.
Lakini kivutio zaidi kwenye shughuli hiyo iliyoshuhudia pia Mussa Issa ‘Cloud’ anayekaimu uongozi wa Bongo Movie Unity akiutangaza upya umoja wao, alikuwa ni shoga mkubwa wa Rose, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’ambaye alionekana ‘akimkogesha’ fedha rafikiye wakati wa kutoa zawadi ulipowadia.
Sherehe ya Rose Ndauka Ilivyofana. Ni Mwendo wa Vinguo Vifupi, Pombe na Manoti
Reviewed by habari motto
on
10:39 AM
Rating: