HATARI KWA AFYA;;Mayai mabovu yasambaa Dar !

Egg-In-Tray
AFYA za wakazi wa jiji la Dar es Salaam ziko hatarini kutokana na kula mayai ya kuku yaliyooza, ambayo yameingizwa kinyemela nchini na baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni wawekezaji.
Mtoa taarifa hii anasema mayai hayo yamekuwa yakisambazwa kwa wingi mitaani huku hatua stahiki hazichukuliwi .
 Alisema kama Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi itashindwa kuwadhibiti wakezaji hao wasio waminifu wakaingiza mayai hayo kinyume na sharia basi serikali ijiandae kwa fedha nyingi kwa ajili ya kuja kutibu magojwa yatakayotokana na ulaji wa mayai hayo.
“Nimejaribu kupita katika maeneo yanako uzwa kwa kweli hali ni mbaya kwani ni uozo mtupu kiasi kwamba ahata wakazi wanaoishi karibu na maduka hayo kiafya wako mashakani na  wanashangaa kuona mayai hayo yakiachwa bila kudhibitiawa,”alisema daktari huyo.
Alizitaja majina ya baadhi ya kampuni ambazo zinahusika na uingizaji wa mayai hayo huku zikidaiwa pia kuwa na mashine za kutengenezea mayai bandia katika mashamba yao yaliyoko wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
HATARI KWA AFYA;;Mayai mabovu yasambaa Dar ! HATARI KWA AFYA;;Mayai mabovu yasambaa Dar ! Reviewed by habari motto on 8:38 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.