Wafa wakisindikiza mzigo nyeti

Valentino Mlowola
GARI lililokuwa likisindikiza mzigo nyeti limepinduka leo likijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki na kuua waliokuwemo na kujeruhi wengine.

kamanda wa polisi mkoa wa mwanza, Valentino Mlowola  amethibitisha kuwepo kwa ajali hiyo.

Amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 7.40 katika eneo la Mkuyuni, jijini hapa ambapo
ilihusisha gari la Benki Kuu (BOT) lenye usajili namba SU 35296 toyota land cruiser.

Alisema waliokufa ni  Beatrice Wanzagi Lumereja (37) afisa wa BOT na mkazi wa Kiseke na Dereva Mohamed Mumba (45).

Waliojeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando ni pamoja na Sajenti
Joel na PC Jumane waliokuwa wakisindikiza mzigo huo nyeti pamoja na dereva pikipiki
Deus Kalokola (32).

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa pikipiki namba T 792CTGkuingilia msafara
ghafla.

Hata hivyo Mlowola alisema mzigo huo nyeti upo salama na kwamba miili ya marehemu
imehifadhiwa katika hospitali ya Bugando.
Wafa wakisindikiza mzigo nyeti Wafa wakisindikiza mzigo nyeti Reviewed by habari motto on 10:06 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.