Akamatwa Na Noti Bandia, Mashine Ya Kutengenezea Pesa Bandia

 Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kibara wilayani Bunda mkoani Mara Jonathan Daniel (33) kwa tuhuma za  kupatikana na noti bandia 75, za shilingi elfu kumi kila moja zenye thamani ya shilingi 750,000, pamoja na vifaa vya kutengenezea pesa hizo bandia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  kwa vyombo vya habari na  kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga Bw. Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea Desemba 27 mwaka huu,majira ya saa 2 na dakika 45 usiku katika eneo la kituo cha mabasi kwenye kijiji na kata ya Kakola  tafara  ya Msalala wilayani Kahama.

Amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wa jeshi hilo wakati wakiwa katika doria ya kawaida kwenye kituo hicho cha mabasi akiwa na noti hizo bandia na kuwa kati yake noti 3 zina namba BL, 0315207, noti (32) BB 0315203, noti (21) BE 0315206 ,  na noti (19) zikiwa na namba BC 0315209.

Kamanda Kamugisha amesema licha ya kumkamata mtuhumiwa na noti hizo  bandia, pia amekamatwa akiwa na  bando ya karatasi , Sindano pamoja na chupa  ya konyagi iliyokuwa na unga mweupe, vifaa ambavyo vinasadikiwa kuwa vinatumika kutengenezea noti hizo.

Aidha kamanda Kamugisha ameongeza kuwa Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazo mkabili mara baada ya upelelezi wa jeshi hilo kukamilika.
Akamatwa Na Noti Bandia, Mashine Ya Kutengenezea Pesa Bandia Akamatwa Na Noti Bandia, Mashine Ya Kutengenezea Pesa Bandia Reviewed by habari motto on 2:34 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.