Wengi walinitaka pia nielezee huku nikiulizwa mbona hakuna nilichozungumza. Nilifarijika sana kwani muda uliopita wengi hawakua wakihoji juu ya maswala ya udukuzi pamoja na usalama mitandao na huwenda hii ilitokana na kutokua na uelewa wa maswala husika.NINI HASA KILITOKEA?Kwanza kabisa Kulikua na Itlafu ya Umeme ambayo ilisababisha baadhi ya Mashine kuzima.
Lakini pia ikumbukwe mifumo kuzima na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi huwenda ni maswala tu ya kiufundi na isi husiane kabisa na uhalifu nilio uzungumzia.Panapo zimika kwa mitambo ya umeme wakati mwingine husababisha komputa kuzima ghafla kama mifumo ya kuhifadhia moto kutokua vizuri.Watu wengi wanapotuma maombbi kwenye mfumo wanaweza kuisababishia kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo kutokana na kuzidiwa nguvu – Hii inafanana na aina ya uhalifu nilio uzungumzia ingawa huwenda ikawa ni wengi wametaka kwa nia njema kujua kiasi cha pesa zao baada ya kusikia kuna tatizo.Niendelee kuwasihi wa Tanzania, wanapo ona tatizo ni vizuri kulifatilia na kulichunguza kwa makini kabla ya kulitolea taarifa na pia kuwapongeza kwa dhati kwa kuweza kuchanganua mambo hadi kuweza kufikiria juu ya uhalifu mtandao ambapo ni hatua nzuri ya uelewa wa maswala ya usalama mitandao nchini.
Aidha, Nimefahamishwa kua tayari taarifa kuhusiana na tukio hilo lilio ambatana na taarifa zilizo sambazwa limetolewa ufafanuzi na uongozi wa benki hiyo kwa wateja wake. Na Pia Nitafurahi sana kuona pakiwa na wa Tanzania wakiendelea kutaka kujuua zaidi kuhusiana na maswala ya usalama mitandao.
NA Yusuph Kileo
Kilichotokea Jana Kuhusiana Na Benki Ya NBC
Reviewed by habari motto
on
9:12 AM
Rating: