MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo leo ameutaka uongozi wa Jiji la Mwanza kupitia kwa mkurugenzi wake kuwapatia maeneo ya biashara wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la Machinga wote waliopo jijijini humo.
Mulongo amesema wafanyabiashara hao wapewe maeneo yao ya kufanyia biashara ili kuepusha msongamano na kurundikana maeneo mbalimbali ya jiji hilo bila sababu za msingi wakati uwezekano wa viongozi wa serikali kuwapa maeneo ya kufanyia kazi upo.
Mulongo ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Wamachinga maeneo ya soko kuu jijini Mwanza . Aidha Mhe. Mulongo amekemea tabia ya viongozi wa serikali kuwaamuru askari wa jiji kuwapiga, kuwakamata na kuwanyang'anya mali zao wafanyabiashara hao huku wakiwa wameshindwa kuwapa maeneo ya kufanyia biashara.
Katika hatua nyingine, Mulongo ameeleza kuwa amepokea maombi yote ya wafanyabiashara hao na Jumatano ijayo watakutana katika Uwanja wa CCM Kirumba ili kufanya uchaguzi wa viongozi wao sambamba na kukabidhiwa maeneo yao maalum kwa ajili ya kufanyia biashara.
Mulongo ameongeza kuwa ni wajibu wa viongozi wa maeneo husika kujua majukumu yao ya kuwatumikia wananchi ili wasilalamike kuhusu utendaji kazi wa serikali na matokeo yake kuichafua serikali tawala ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
NA JOHNSON JAMES, MWANZA
Mkuu Wa Mkoa Awajia Juu Viongozi Wa Jiji, Haya Ndiyo Maamuzi Yake
Reviewed by habari motto
on
9:39 AM
Rating: