Mtuhumiwa Madawa Ya Kulevya Auawa Akitaka Kutoroka

 

Saa kadhaa zilizopita Polisi walimfyatulia risasi mtuhumiwa aliejaribu kutoroka baada ya kufikishwa kwenye Mahakama ya Kisutu Dar es salaam asubuhi ya December 31 2014.
Muda mfupi baadae Polisi ikatoa taarifa kwamba mtuhumiwa wa dawa za kulevya aliyeuwawa ni Abdul Koroma raia wa Sierra Leone na aliuwawa kwa risasi wakati akitoroka Mahakamani.

 

Mtuhumiwa wa dawa za kulevya Adul Koroma raia wa Sierra Leone amepigwa risasi na kufa leo asubuhi wakati akijaribu kutoroka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa mahabusu aliyekuwa anatuhumiwa kubeba madawa ya kulevya, Abdul Koroma raia wa Sierra Leone baada ya kupigwa risasi.
Koroma akiwa  kwenye machela tayari kwa kupelekwa kuifadhiwa hospitalini.

Mtuhumiwa wa madawa ya kulevya raia wa Sierra Leone akiwa amepigwa risasi baada ya kutaka kuwatoroka askari magereza katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam. 

Mtuhumiwa Madawa Ya Kulevya Auawa Akitaka Kutoroka Mtuhumiwa Madawa Ya Kulevya Auawa Akitaka Kutoroka Reviewed by habari motto on 2:43 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.