Bwa’mdogo kutoka Tandale, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa madansa wake ndani ya Lagos, Nigeria.
WALIANZIA HOTELINI
Kwa
mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond nchini humo, saa chache
kabla ya shoo kuanza, P-Square walimuibukia kwenye Hoteli ya Eko
aliyofikia jijini humo na kummwagia pongezi nyingi sambamba na kumshauri
baadhi ya vitu vya kimaendeleo.
‘Diamond Platnumz’ akifurahia jambo na Peter Okoye wa 'P Square'.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo
hicho kilisema, P-Square walionekana kuvutiwa zaidi na juhudi binafsi
za Diamond kiasi cha kuweza kuipeperusha bendera ya Afrika Mashariki
katika levo za kimataifa.
“Jamaa
walipomuona tu hotelini waliguswa sana na juhudi zake binafsi maana
wanatambua jinsi gani muziki ulivyokuwa mgumu kuuvusha nje ya nchi yako
lakini kwa kuwa Diamond ameweza, walimpigia saluti,” kilisema chanzo
hicho.
ARUHUSIWA KOLABO
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga data za ndani kwa kusema, mbali na kumpigia
saluti, P-Square walionesha wako tayari kumsapoti Diamond kwa kumpa
nafasi ya kufanya nao kazi yaani kolabo.
“Wamempa
nafasi ya kufanya naye kazi pale atakapojisikia kutokana na mipango
yake, kama akiamua kufanya sasa au baadaye ni uamuzi wake lakini jamaa
(P-Square) hawana kinyongo naye lengo lao ni kuona muziki wa Afrika
unateka dunia,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
‘Diamond Platnumz’ akiwa na Paul Okoye wa 'P Square'.
“Walimwambia
the way (namna) alivyo na juhudi kwenye kazi yake anatambulika Nigeria
utafikiri ni msanii kutoka Nigeria, walimpa mbinu zao za namna
walivyopigana hadi kufika hapo walipo.”
MASTAA WAMUIBUKIA
Mbali
na P-Square, mastaa mbalimbali wa Nigeria walimuibukia Diamond hotelini
hapo akiwemo Mr Flavour na Jude Abaga ‘M.I’, ambao walimpa pongezi
Diamond kwa kujua kumiliki vyema jukwaa kwani wamekuwa wakifuatilia shoo
zake hasa anapotupia video zake mitandaoni.
Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Mr Flavour akiteta jambo na 'Diamond Platnumz'.
APIGA SHOO YA MAANA
Ulipofika
wakati wa kupanda jukwaani, Diamond aliitikisa Nigeria kwani alionesha
vitu vya tofauti wakati akiimba nyimbo zake na kuwafanya Wanigeria na
waalikwa mbalimbali wapigwe na butwaa huku wengi wakiishia kumpigia
makofi na shangwe la kufa mtu.
DIAMOND ANASEMAJE?
Paparazi
alimcheki Diamond kupitia mtandao wa WhatsApp ambapo aliwashukuru
mastaa hao wa Nigeria kwa upendo wao na kuahidi kuendelea kufanya
maajabu zaidi katika levo za kimataifa.
“Wana
wamenisapraizi hotelini, tumepiga stori nyingi, wameonesha wanakubali
kile ambacho mimi nafanya, jukwaani nimefanya vizuri, watu na heshima
zao mwishoni walipiga makofi kuonesha wamekubali.
KUHUSU KOLABO?
“Kuhusu
kolabo na P-Square, ni mapema sana kuzungumzia kwa kuwa nina mipango
mingi ya kufanya mwaka huu, mashabiki wakae mkao wa kula, nikiona
inafaa, nitafanya nao maana wao hawana shida na mimi,” alisema Diamond.
P-SQUARE NI ZAIDI YA DAVIDO
Awali,
kabla Diamond hajakutana na P-Square, alishirikiana na mkali mwingine
wa Nigeria, Davido katika wimbo wake wa Number One Remix ambaye
inaaminika kwa umaarufu na uwezo wa kimuziki yupo chini ya P-Square.