News Alert ; Mez B Afariki Dunia Leo, Dodoma


Msanii wa Chemba Squad, Moses Bushagama  ‘Mez B’ enzi za uhai wake. -

MSANII wa Chemba Squad, Moses Bushagama  ‘Mez B’ amefariki leo saa nne asubuhi mkoani Dodoma ambapo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pneumonia.  


Moja ya taarifa ya kushtua na kuhuzunisha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii,
pamoja na watu kutumiana message ni kuhusu msiba wa aliyekuwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, katika kipindi cha LEO TENA wametafutwa watu wa karibu ili kuthibitisha taarifa hiyo.
Dada wa marehemu ambaye jina lake ni Rachel amethibitisha kuwa msanii MEZ B amefariki akiwa nyumbani kwao Dodoma.
MEZ-B2
Noorah ni msanii ambaye walikuwa karibu na Mez B, amesema Mez B alikuwa na homa tangu mwezi December mwaka jana na baadaye akasafiri kwenda Dodoma huku hali yake ikiwa bado sio nzuri, mara ya mwisho wameongea kwenye simu ni siku tano zilizopita, leo simu yake imepokelewa na dada yake akimtaarfu kuwa Mez B amefariki muda mfupi uliopita baada ya kuzidiwa.
Mez B aliwahi kuwa kundi moja Chamber Squad na akina Ray CNoorah na marehemu Albert Mangwea pia.
Msiba uko nyumbani kwao eneo la Kisasa, Dodoma.
millardayo.com itakusogezea taarifa zaidi kutoka msibani Dodoma kila zinaponifikia, #RIP Mez B.
Hii sauti kutoka kwenye Leo Tena @CloudsFM, kasikika NOORAH, TIMBULO na RACHEL ambaye ni dada wa MEZ B.

News Alert ; Mez B Afariki Dunia Leo, Dodoma News Alert ; Mez B Afariki Dunia Leo, Dodoma Reviewed by habari motto on 2:41 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.