Wanafunzi Tunduma walala barabarani ,Field Force Unity (FFU) Washidwa La Kuwafanya


 Lori lililosababisha ajali na kuua mwanafunzi na kusababisha wanafunzi wa shule za msingi Tunduma kulala barabarani wakishinikiza kuwekwa kwa matuta.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za Msingi Umoja,Mlimani na Tunduma za mjini Tunduma wakiandamana kushinikiza kuwekwa matuta kwenye inayoelekea Sumbawanga kutokana na ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na mwendo kasi wa madereva. 

Lori linaloonekana pembeni limepinduka, limesababisha ajali na kuua mwanafunzi.
 Wanafunzi wakiwa wamekaa barabarani mjini Tunduma
 Askari wa usalama Barabarani mjini Tunduma akipewa maelezo ya hali ya mtoto aliyejeruhiwa katika ajali hiyo Jackson Sichalwe(7) kutoka kwa baba yake Mzazi Norbert Siichalwe,Mtoto Jackson  amelazwa katika hospitali ya serikali mjini Tunduma baada ya kugongwa na gari ambalo pia lilisababisha kifo cha Emmanuel Sichalwe mwanafunzi wa shule ya msingi Umoja ya mjini Tunduma
 Mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma wakiwa katika mkusanyiko kufuatia taharukii iliyoibuka mjini i
Diwani wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka akizungumza na wanaanchi baada ya kutokea tafrani iliyosababisha wanafunzi wafunge barabara kwa kushinikiza kuwekwa matuta.Picha na Rashid Mkwinda
 

SAUTI zilizochanganyika na hisia na majonzi kutoka kwa wanafunzi wa shule tatu za Msingi, Umoja, Mlimani na Tunduma zilisikika hewani na kutoa ujumbe ulioashiria kupata ufumbuzi wa tatizo la ajali za mara kwa mara katika barabara kuu iendayo Sumbawanga kutokea mjini Tunduma.

Ijapokuwa zilikuwa ni sauti za watoto, zilibeba ujumbe mzito wenye shinikizo la uchungu uliofuatia kufariki kwa mtoto mwenzao Emmanuel Sichalwe (7) ambaye aligongwa na lori na kufariki hapo hapo baada ya kukanyagwa na kupasuka kichwa.

Haikuwa rahisi kuhisi machungu ya watoto hao ambao ni kilio cha muda mrefu kutoka kwa wazazi na wananchi waishio maeneo ya barabara kuu ya kuelekea Sumbawanga ambapo takribani watu 18 wakiwemo watoto 10 na watu wazima 8 hali ambayo imekuwa ikijenga hofu miongoni mwa wakazi wa maeneo hayo.
Insurance  
Wanafunzi hao walifunga barabara na kulala barabarani kuanzia saa 12:30 alfajiri huku wakihanikiza sauti zao hewani kwa maneno yaliyosikika, "Tunataka!!, Matuta!!. Magari!!, Yanatumaliza!!!" sauti hizo zilikaririwa mara kwa mara huku baadhi yao wakionesha mabango
KUTAZAMA PICHA na VIDEO  BONYEZA HAPA CHIN>>>>
Wanafunzi Tunduma walala barabarani ,Field Force Unity (FFU) Washidwa La Kuwafanya Wanafunzi Tunduma walala barabarani ,Field Force Unity (FFU) Washidwa La  Kuwafanya Reviewed by habari motto on 2:59 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.