Hiki Ndicho Kilichosababisha Ofisi Ya Marehemu Kanumba Kuhamishwa

MAMA mzazi wa marehemu Kanumba Flora Mtegoa amefunguaka baada kuongea nasi kuwa moja ya sababu iliyofanya ofisi yake kuhama kutoka maeneo ya Sinza Meeda ilipokuwa wakati wa uhai wa mwanaye ni gharama za pango hilo kupanda kila mwaka.

“Kuna watu ambao wanadai na kuandika hata katika mitandao ya kijamii kuwa eti ofisi za Kanumba The Great Films zimefungwa na hazipo tena, si kweli kodi ni kubwa sana hivyo tumehamishia Kimara Temboni,”anasema Mama Kanumba.


Mama Kanumba amesema kuwa ofisi hiyo inafanya kazi wala haijafungwa na kwa uhakika ni kwamba kuna filamu ambayo imekamilika na itatoka hivi karibuni chini ya kampuni, filamu hiyo imewashirikisha wasanii Flora Mtegoa, Mohamed Mwikongi ‘Frank’, Rose Ndauka na wasanii wengine.
Hiki Ndicho Kilichosababisha Ofisi Ya Marehemu Kanumba Kuhamishwa Hiki Ndicho Kilichosababisha Ofisi Ya Marehemu Kanumba Kuhamishwa Reviewed by habari motto on 3:21 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.