Idadi Ya Watu Waliofariki Yafikia 42 Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya Akiongea na wahanga wa tukio hilo la ajabu Tanzania katika eneo la tukio.

Idadi ya watu waliopoteza maisha kufutia janga la mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeongezeka na kufikia 42 na waliolazwa hospitalini 91.

Akizungumza na Dunia kiganjani blog akiwa kwenye eneo la tukio, mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya amesema idadi hiyo imeongezeka kutoka vifo 38 na majeruhi 82 kama ilivyotolewa taarifa jana mchana.

Mpesya amesema katika majeruhi 91 wanne hali zao siyo nzuri na kwamba wamepewa rufaa wako katika hospitali ya mkoa katika manispaa ya Shinyanga.

Na Beka Mtanzania
Idadi Ya Watu Waliofariki Yafikia 42 Shinyanga Idadi Ya Watu Waliofariki Yafikia 42 Shinyanga Reviewed by habari motto on 3:12 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.