Padri Fake Apandishwa Kizimbani

Josephat Asenga(47) Mchumi na mhasibu wa kujitegemea ambaye ni Padri feki Mkazi wa mtaa wa Lusanga,jana amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro kujibu shitaka la udanganyifu na kujifanya Padri wa kanisa Katoriki. 

Wakili wa serikali Gloria Rwakibarika akisoma maelezo ya kosa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Agripina Kimaze,alisema kuwa Asenga kwa nyakati tofauti Mei mwaka 2014 na Mchi 5 mwaka huu 2015 majira tofauti alifika katika kanisa katoriki parokia ya Maria Mtakatifu Modeco na kudanganya kuwa yeye ni padre.

Rwakibarika alisema kuwa Asenga alipofika Parokiani hapo na kujitambulisha kuwa yeye ni Padri wa kanisa hili kinyume na kifungu cha sheria namba 369(1) na kifungu cha sheria namba 35 vyote vikiwa vya sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16 ya mwaka 2002.

Wakili Rwakibarika alisema kuwa mshtakiwa huyo alijitambulisha kwa Padri wa Parokia ya Maria Mtakatifu Modeco Padri Maliti Joseph Dyfrig kwa nia ya kutapeli huku akijua kuwa ni kinyume cha sheria.

Wakili huyo alisema kuwa upelelezi juu ya shitaka hilo bado haujakamilika.

Mshitakiwa Josephat Asenga amekana shitaka lake na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili wa uhakika mmoja wapo akiwa mtumishi wa serikali.

Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Kimanze alisema mahakamani hapo kuwa dhamana ya mshitakiwa iko wazi ya watu wawili wa uhakika moja wapo akiwa mtumishi wa serikali wawe na kiasi cha shilingi 1 milioni kila mmoja,na kumtaka mshtakiwa kama kuna watu wa kumdhamini wajitokeze.

Mshitakiwa alipotakiwa wadhamini kujitokeza walikosekana na kuamuliwa kurudishwa rumande hadi Machi 25 mwaka huu shitaka lake litakaposikili tena mahakamani hapo.

Nje ya mahakama,baadhi ya watu(waliojitambulisha kuwa wao ni waumini) waliohudhulia kusikilizwa shitaka hilo la padri feki walisema kuwa kufikishwa mahakamani kwa padre huyo itakuwa fundisho kwake na kwamba amekuwa akifanya shughuli ya kutoa huduma hiyo kwa muda mrefu kanisani hapo.

Salome Ambros na Amani Amandus waliokuwapo mahakamni hapo alisema kuwa padre huyo amewahi hata kufungisha ndoa zaidi ya mbili kanisani hapo na kuutaka uongozi wa kanisa katoriki kufanya utaratibu kuwabariki wale wote waliofungishwa ndoa na padre huyo.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti la Mwananchi Rose Dilunga mwenyekiti wa mtaa wa Lusanga alioyekuwapo mahakamani hapo,alisema Padri huyo alifika mtaani hapo na familia yake mwaka jana(Mwanamke anayeishi naye) na kujitambulisha kwake kuwa yupo katika mtaa wake.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa Padri huyo amepanga katika mtaa huo,na kwamba aliwahi kujitambulisha yeye kama Padri lakini hawakumfatilia kwani ni maisha ya mtu binafsi.

Aidha alisema kuwa juzi (Machi 10 mwanamke anayeishi na padri huyo alifika ofisi ya mtaa kwa ajili ya kupata barua ya dhamana na kupatiwa lakini mpaka padre huyo anapadishwa kizimbani mwanamke huyo walikuwa wakimtafuta na kumpigia simu bila kupatikana.

Marchi 5/2015 Padri feki akamatwa na polisi kwa kujifanya padre. 
Lilian Lucas, Morogoro 
Mtu mmoja aliyejifanya padri wa kanisa katoriki kutoka jimbo la Newyork nchini marekani Josephat Asenga(47)Mhasibu na mkazi wa mtaa wa ujenzi Manispaa ya morogoro anashikiliwa na polisi kwa kujifanya padri.
Asenga alikamatwa na jeshi la polisi mkoani hapa Machi 5 mwaka huu majira ya saa 10.30 jioni huko katika kanisa katoriki parokia ya mtakatifu Maria Modeko jimbo la Morogoro iliyopo kata ya mazimbu akiwa na majoo saba (7) ya upadri.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonald Paulo akizungumza na waandishi wa habari jana alisema kuwa Padri huyo feki alifika parokiani hapo mwezi Mei na Juni mwaka jana 2014 na kujitambulisha kwa Paroko wa parokia hiyo ya Modeko na viongozi wa kanisa hilo kuwa amekuja nchini Tanzania kwa ajili ya Mapumziko na kuomba kufanya ibada.
Alisema kuwa Padri huyo feki alionyesha kitambulisho na kuaminiwa na kuruhusiwa kuendesha misa bila matatizo katika kanisa hilo na baada ya kumaliza misa uongozi wa kanisa ulimtilia shaka na kuanza kumfatilia.
Aidha kamanda Paulo  alisema kuwa kwa muda wote huo viongozi wa kanisa hilo pamoja na waumini walianza kumfatilia na kupata taarifa kuwa alikuwa akiishi na mwanamke kinyume na sheria na taratibu za kipadri kwa kanisa Katoriki.
Kamanda huyo alisema kanisa hilo liliweka mtego na ndipo Padri huyo feki Machi 5 mwaka huu alimpigia simu Paroko wa kanisa la modeko na kuomba nafasi ya kwenda kuendesha misa  na alikubariwa ndipo uongozi ulifanya mawasiliano na jeshi la polisi na kumkamata.
Pia kamanda Paulo alisema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni Padri Feki baada ya kuhojiwa alikiri kuwa yeye si Padri na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea na utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
Kiongozi mmoja wa kanisa katoriki parokia ya mtakatifu Maria ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini alisema kuwa,siku alipoendesha misa Padri huyo feki waligundua baadhi ya mapungufu ndipo walipomtilia shaka na kuanza kumchunguza.
Alisema kuwa taarifa nyingine walizipata kutoka kwa mkuu wa kituo cha Amani  kilichopo maeneo ya Chamwino kuwa Padri huyo amekuwa akiishi na mwanamke eneo la mtaa wa Ujenzi manispaa ya morogoro.
Aidha alisema kuwa Padri huyo feki alipohojiwa na uongozi wa kanisa alidai kuwa yeye alipata daraja la Upadri jimbo kuu la Dar es salaam na walipofanya mawasiliano na katibu wa jimbo hilo alikana kuwapo kwa jina la Padri huyo. 
Lilian Lucas, Morogoro 
NA MTANDA BLOG
Padri Fake Apandishwa Kizimbani Padri Fake Apandishwa Kizimbani Reviewed by habari motto on 8:45 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.