Majanga: Atokomea Kusikojulikana Na Kidole Cha Mtoto


KATIKA hali isiyo ya kawaida mtu asiyefahamika amemkata kidole cha mkono wa kushoto mtoto wa miaka sita (siyo mwenye ualbino) na kutokomea nacho kusikojulikana katika mtaa wa Mtakuja eneo la Majengo Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Akizungmza na mwandishi wa habari aliyefika nyumbani kwa mtoto aliyekatwa kidole juzi  Machi 17, 2015, Bi Lucy Savery (26) mama wa mtoto huyo ambaye ni mjane alisema mwane anaitwa Chrispin Leonard Nkana (6) wanaishi katika mtaa huo wa Mtakuja kata ya Majengo katika
Manispaa ya Sumbawanga.
Alisema kuwa juzi Machi 16, 2015 majira ya saa sita mchana alikuwa kibaruani kwake katika hoteli moja mjini Sumbawanga akapigiwa simu na majirani kuwa mwanae amekatwa kidole na mtu asiyefahamika na kuondoka nacho, alipofika nyumbani alimkuta mwane Chrispin akilia sana akiwa
amepakatwa na jirani yao.
Alisema walipomuuliza mwanae nani kamkta kidole alisema kuwa ni baba mmoja aliyefika akamkamata na kuingia nae kwenye shamba la mahindi akamfunga na nguo mdomoni akatoa mkasi mkubwa mfukoni na kumkata kidole kisha akakimbia kuelea ndani ya mahindi.
Alisema waliamua kumkimbiza hospitali ya Dk Artman (Kristu Mfalme) Sumbawanga wakaelekezwa wafike kituo cha polisi kwanza wapewe fomu namba tatu ndipo mtoto apate matibabu maelekezo ambayo waliyetekelezwa mtoto akatibiwa.
Alipohojiwa na mwandishi wa habari, mtoto aliyeumizwa, Chrispin Leonard Nkana alisema kuwa mtu huyo alikuwa amevaa suruali nyeusi na shati jeupe na kuwa aliwahi kumuona mara moja mashineni siku za nyuma.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Rukwa Jacob Mwaruanda alipoulizwa kuhusu tukio la kukatwa mtoto kidole eneo la Majengo mjini Sumbawanga alisema kuwa bado lipo kwa RCO wake bado halijafika kwake.
“Tukio hilo kwangu bado halijafika lakini kama walitoa ripoti polisi litakuwa katika ofisi ya RCO kwa hatua zaidi na wakilikamlisha faili wataniletea nami nitawapa taarifa tutakachokuwa tumebaini juu yake” alisema Mwaruanda.
Majanga: Atokomea Kusikojulikana Na Kidole Cha Mtoto Majanga: Atokomea Kusikojulikana Na Kidole Cha Mtoto Reviewed by habari motto on 7:09 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.