Majonzi Yazidi Kutanda, Mke Wa Noorah Afariki Dunia

Mke wa rapper Noorah, Camila Kingwalu amefariki dunia jana nyumbani kwao Morogoro baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Ndugu wa karibu wa marehemu ambaye hakutaka kutajwa jina lake, amesema Camila baada ya kuanza kuugua alirudi nyumbani kwao mpaka mauti yalipomkuta hapo jana.

“Kweli amefariki alikuwa kwao Morogoro na bado haikujulikana alikuwa anaumwa nini na mume wake naye anaumwa yupo kwao Shinyanga,” amesema.

“Kwahiyo msiba upo Morogoro, kuna mtu ambaye anaelekea Morogoro sasa hivi akifika kule tutajua kila kitu. Morogoro alienda muda kidogo baada ya kuachana na mume wake. Baada ya kuachana, Noorah akaenda kwao na mke wake akaenda kwao. Hawakubahatika kuwa na watoto,” ameongeza.

“Marehemu alikuwa anaitwa Anna Kigwalu lakini baada ya kuolewa na Noorah akabadilisha jina na kuitwa Camila.”

Tunampa pole Noorah kwa msiba huo.

~Bongo5
Majonzi Yazidi Kutanda, Mke Wa Noorah Afariki Dunia Majonzi Yazidi Kutanda, Mke Wa Noorah Afariki Dunia Reviewed by habari motto on 2:01 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.