Tarehe 12/4/1984 alasiri Taifa lilipatwa na Msiba wa kuondokewa na Aliekuwa Waziri Mkuu kwa wakati ule Marehemu Edward Sokoine
Kwa upande wa Muziki nadhani wanamuziki wa iloyokuwa bendi ya Orchestra Makassy kwa wale ambao bado wapo hai awatausahau msiba huu.
Kuna kisa aliwai kukielezea Marehemu Issa Nundu (Prince) kwamba wakati msiba unatokea bendi ndio ilikuwa imefika Mjini Kigoma hivyo baada ya ajali kutokea na kusababisha kifo Cha Mh Sokoine Taifa lilitangaza siku kadhaa za Maombelezo hivyo bendi ilibidi kukwama kurejea Dar kwakuwa awakuwa na nauli ya kuwaleta Dar na sio nauli tu hata pesa za mahitaji mengine ya chakula na malazi ilikuwa ni shida kwao alisema hayo Hayati Prince Issa Nundu.
Pichani hilo ni gari aina ya Mercedes Benz kama linavyoonekana baada ya kupata ajali na kusababisha kifo cha Mh Sokoine tarehe 12/4/1984
Ajali Mbaya Ilitokea, Waziri Mkuu Afariki Dunia
Reviewed by habari motto
on
8:46 AM
Rating:
