Lulu akiwa kwenye pozi..
..Afunga ‘akaunti’ yake ya Instagram kwa siku zisizojulikana
..Wema Sepetu ampongeza, amuonea huruma kifo cha Seki
Na Andrw Chale wa Modewji blog
Habari maalum hadi tunakuwekea hapa, Leo Aprili 16.2015, ni siku ya kipekee kwa muigizaji na Msanii wa filamu na ‘modo’ kwenye matangazo mbalimbali ya Bongo, Elizabeth Michael maalufu kama Lulu ambaye ametimiza miaka 20.
Hata hivyo hadi hivi sasa Lulu ambaye pia amekuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao yake ya kijamii hasa Instagram na twitter pamoja naa facebook, ameamua kujiondoa kwa muda husio julikana kufuatia kuwapo kwa taarifa za kifo cha mwanaume anayeelezwa alikuwa ‘akitoka’ naye.
Modewji blog ilipowasiliana na Lulu kwa njia mbalimbali ikiwemo simu yake ya mkononi haikuweza kupatikana licha ya ukituma meseji yaani ujumbe mfupi kupokelewa.
Aliyekuwa na mahusiano naa msanii Lulu, Seki ambaye imeelezwa amefariki dunia.
Hata hivyo baadhi ya watu wa karibu wakiwemo mastaa wakubwa wa Bongo, Aliyewahi kuwa Miss Tanzania na ambaye kwa sasa ni Msanii wa filamu Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliweka picha ya Lulu na kumtakia kheri ya kuzaliwa posti inayoendelea kupokea LIKES nyingi sana ambapo hadi sasa zimefika 9,088 huku kommenti zikiendelea kufika 328, Posti hiyo aliyoweka masaa mawili hata hivyo baada ya saa la tatu, Wema alitupia Post nyingine akiwa ameweka picha ya mwanaume huyo aliyefariki anayeelezewa kuwa alikuwa bwana wa Lulu, aliyefahamika kwa jina la Seki.
Katika picha hiyo, Wema aliandika: “Ulikuwa ni mtu wa watu..Saaana..najua utaliliwa na Wengi.. They say vizuri havidumu..Pumzikaa kwa amani baba…Its jus too hard to sink..in..(huku akiwa ameweka emoji ya majonzi) aliandika Wema huku akipata LIKES nyingi na komenti ambazo nyingi zilikuwa zikimuonea huruma Lulu.
Hata hivyo, licha ya Lulu kufunga akaunti yake hiyo ya Instagram anayoitumia ya OfficialLuluMichael, moja ya mtandao wake wa kijamii wa twita, majira ya masaa 7 hadi 6 yaliyopita Lulu alikuwa akitumia mtandao huo kujibu salamu za pongezi za kuzaliwa kwake.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Awali jana Aprili 15,Lulu alitoa posti kwenye twitter akieleza kuwa, anaingia kutimiza miaka 20,kamili na mtu mwenye wasiwas basi aende taasisi ya usajili ya vizazi na vifo,RITA, atapata ukweli.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ atimiza miaka 20, akutwa na majanga makubwa tena?
Reviewed by habari motto
on
9:13 AM
Rating: