Staa wa Muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga ‘Linah’ akiwa ameketi na William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo.
MREMBO anayefanya poa kunako Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’, anadaiwa ‘kujiegesha’ kimahaba kwa shemeji yake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo.
Ndani ya Ukumbi wa Triple 7 uliyopo Kawe jijini Dar hivi karibuni, paparazi wetu aliwaona wakiingia sambamba na kukaa beneti kama mtu na mpenzi wake jambo lililozua maswali kibao kutoka kwa wateja waliokuwepo ukumbini hapo.
Ndani ya Triple 7, paparazi wetu aliamua kumfuata Linah ili ajiridhishe uwepo wake na mwanaume huyo ambapo msanii huyo alijing’atang’ata na kusema:
“Huyu ni mtu wangu huwa natoka naye. Sijui umenielewa? Natoka naye sehemu mbalimbali.Ila kukutoa wasiwasi tambua kwa sasa sina mpenzi na nina haki ya kuwa naye, sina mpaka wa kujiachia na Boss Mtoto,” alisema.
Linah Ajiweka Kimahaba Kwa Kaka Yake Zari
Reviewed by habari motto
on
9:19 AM
Rating:
![Linah Ajiweka Kimahaba Kwa Kaka Yake Zari](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgF5GtbJpzpylVtY3VNDxkSIb8CqX0rm8_w7vqXUEShwof7_iKXe-yxrYKFGkLJroIGK_VySwemkIwlT_1VGxALREAOuZ29eDFS6X7Ag1nYA6cmJtH5SaCTGlak3vB1-b3DUq9Brgii/s72-c/Linah.jpg)