ASAS DAIRIES LTD Wapokea Sifa Nzito

Rais Dr Jakaya Kikwete akipata  maelezo ya  bidhaa  za Asas Daireis Ltd  kutoka kwa afisa masoko  wa kampuni  hiyo  Bw Jimy  alipotembelea  mabanda mbali mbali  katika  maonyesho ya  sikukuu ya   sabasaba yanayotaraji  kuhitimishwa kesho jijini Dar es salaam
Na MatukiodaimaBlog
BANDA la  kampuni ya maziwa ya  Asas Dairies Ltd ya  mkoani Iringa lililopo  limeendelea  kuwavuta  wananchi   na  viongozi mbali mbali  wanaotembelea  viwanja  wa  Saba saba jijini Dar e Salaam  kulitembelea  kupata  bidhaa  zake 
Banda   hilo  ambalo  wiki  iliyopita  lilitembelewa na Rais Dr  Jakaya  Kikwete na  viongozio  mbali mbali  limeendelea  kuvutia  wananchi  wengi  wanaotembelea maonyesho  hayo  kupenda  kufika  kupata  bidhaa mbali mbali  .
Baadhi ya  wananchi  waliofika katika  banda   hilo  walisema  kuwa  wamevutiwa  zaidi ya  bidhaa  zenye  ubora  zinazotengenezwa na kampuni hiyo ya  Asas Dairies  Ltd kutoka mkoani  Iringa na   hivyo kulazimika  kumiminika  zaidi  kupata  bidhaa pamoja na kupata  elimu mbali mbali ya  ubora  wa  bidhaa  hizo .
Alisema Amina  Athuman  ambae ni mmoja wa  wateja  waliofika katika banda   hilo kupata  bidhaa  mbali mbali , kuwa yapo makampuni  mengi ya maziwa ila ubora  wa bidhaa  za maziwa  zinazotengenezwa na kampuni  hiyo ya Asas Dairies Ltd  ndizo  ambazo  zinawavutia  watu wengi  zaidi  kufika katika banda  hilo.
" Mimi  nilikuwa nasikia tu juu ya ubora  wa maziwa  haya toka mkoani Iringa ila baada ya  kufika hapa  nimeshuhudia na  kuanzia  leo  sihitaji maziwa na  bidhaa nyingine kama  hizi  nje ya Asas Dairies Ltd " 
Huku John Mwene  akieleza  kufurahishwa  zaidi na hatua  ya  Rais wa nchi Dr  Kikwete  kutembelea  mabanda  ya  wakulima mbali mbali  likiwemo  banda  hilo la Asas kwani ni ukweli  usiopingika kuwa kwa  Tanzania kampuni  hiyo ya  Asas Dairies  Ltd imeonyesha  uwezo  mkubwa wa kuzifanya bidhaa zake  kuendelea  kuwa na ubora  kwa miaka  mitatu mfululizo.
Kwani  alisema kampuni  kuongoza  miaka mitatu  mfululizo ni jambo la  kujipongeza na kuwa  si rahisi  kwa kampuni kushikilia ubora  wake kwa miaka miwili mfulilizo ila kampuni hiyo imeweza kufanya  hivyo .
Alisema ni jambo la nchi kupitia bodi ya maziwa  na wizara   husika kuangalia  kutoa uwezeshaji  zaidi kwa makampuni bora  ili  kuwezesha  bidhaa zake  kuingizwa katika  soko la dunia . 
Afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy Kiwelu pamoja na kumpongeza Rais Dr Kikwete kwa  kutembelea  banda  lao na kupongeza kwa ushiriki na ubora  wa bidhaa  zao bado  aliwashukuru  wananchi  wanaoendelea  kutembelea banda  hilo .
Alisema kuwa mbali ya kampuni  hiyo kuonyesha  ushiriki mzuri katika maonyesho  hayo ya saba saba bado  wamekuwa  wakishiriki maonyesho mbali mbali yakiwemo yale ya nane nane kwa kushiriki katika kanda mbali mbali na  kuwataka  wananchi wa kanda  zote  nchini kujipanga kwa ajili ya kutembelea mabanda yao wakati wa nane nane mwaka  huu .
Kuhusu kuendelea  kuongoza kwa  ubora  alisema  kuwa hivi  sasa ni  mwaka  wa tatu mfululizo bado  bidhaa  zao  nyingine  zimeendelea  kushinda medali mbali mbali na kuonyesha uwezo mkubwa wa kampuni  hiyo katika ubora .
ASAS DAIRIES LTD Wapokea Sifa Nzito ASAS DAIRIES LTD Wapokea Sifa Nzito Reviewed by habari motto on 11:19 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.