Bobbi Kristina Brown apumzishwa pembeni mwa mama ake

MTOTO wa Mwimbaji maarufu duniani , Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown amezikwa jana pembeni mwa kaburi la mamayake kwenye makaburi ya Fairview yaliyopo Westfield.
Bobbi Kristina Brown  mtoto pekee kwa mwimbaji huyo na Bobby Brown ambaye waliishi naye kwa miaka 17 kabla ya kutengana alikufa Julai 26 baada ya kuzimia kwa takribani miezi sita.
Mwili wake ulishughulikiwa katika mochwari ya Whigham, New wark ambayo pia miaka mitatu iliyopita ilishughulikia mwili wa mama yake.
Bobbi Kristina aliondolewa nyumbani kwake Atlanta  akiwa bafuni hajitambui.
Alikutwa kwa namna ambayo mama yake alikutwa miaka mitatu iliyopita.
 Mwili wa Whitney Houston ulikutwa katika bafu kwenye hoteli aliyokuwa amefikia ya  Beverly Hilton kabla ya tuzo za Grammy za mwaka 2012 .Wataalamu walikuta karatasi iliyoandikwa dawa na kokeni katika mwili wake lakini walisema kwamba alizama kwenye maji kwa bahati mbaya.
Bobbi Kristina Brown apumzishwa pembeni mwa mama ake Bobbi Kristina Brown apumzishwa pembeni mwa mama ake Reviewed by habari motto on 6:24 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.