Maneno ya Waziri wa Fedha kuhusu fedha zilizotumika kuboresha Miundombinu

.

Agosti 25 ni siku ambayo Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alizindua bodi ya PPF na mafao mapya ya mfuko huo.Katika mazungumzo ya Waziri huyo pia alitoa ufanunuzi kuhusiana na fedha za mfuko wa jamii zilizotumika katika kuboresha miundombinu.
‘Na mimi kama msimamizi wa wizara ya fedha nina wajibu wa kujitolea maelezo kuhusiana na madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii, sisi Serikali ama hazina pale tumeunda kikosi kazi kwanza tuseme hatukuweza kulipa haya madeni kwasababu tulikuwa tumekwenda katika utaratibu wa kiserikali ni lazima maamuzi ya jinsi gani madeni haya yatalipwa katika baraza la Mawaziri’ – Saada Mkuya
Mratibu wa Kanda za Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mbaruku akielezea namna fao hilo lilivyozingatia Mwanachama na Mwenza wake.
‘Kwa hiyo tulikuwa katika process lazima waraka uandaliwe na unaandaliwa katika ngazi ya chini kabisa lakini baada ya kufanyiwa marekebisho kwasababu inakwenda inaangaliwa inapewa comment, inafanyiwa marekebisho baada ya hapo imekwenda katika kikao cha makatibu wakuu baada ya kutolewa ufafanuzi baadhi ya maswali ama kuboreshwa zaidi  waraka ule ukawasilishwa katika Baraza la Mawaziri’ – Saada Mkuya

3X6A5632
Na kweli  siku ambayo tulikuwa tumekaa katika baraza la Mawaziri  mada ilikuwa ni hiyo moja tu ni lazima tuangalie ishu ya ulipaji wa mfuko ya pension napenda kuwahakikishia kwamba tumetoka na jawabu na  muongozo mzuri  na tulikuwa na timu ambayo inaangalia jinsi gani tunaweza tukatoa bond‘ -Saada Mkuya
.
Waziri Saada Mkuya akimpongeza Mwanachama wa PPF, Sara Jonas Haule, baada ya kumkabidhi shilingi milioni moja ikiwa ni malipo ya fao la uzazi.
‘Na hizi fedha lazima wananchi wakumbuke tulizitumia kweli tulikopa lakini tumekopa kwa madhumuni mazima ya kuendeleza miundombinu mbalimbali ya nchi hii, tumejenga Barabara, tumejenga Madaraja, tumejenga na sehemu nyingi.kwahiyo tulizitumia  kwaajili ya kuweka miundombinu ya kiuchumi lakini vile vile kwasababu hizi  ni fedha za wanachama ni lazima tuangalie utaratibu wa jinsi gani kuzirudisha fedha hizo’ – Mh.Saada Mkuya
Maneno ya Waziri wa Fedha kuhusu fedha zilizotumika kuboresha Miundombinu Maneno ya Waziri wa Fedha kuhusu fedha zilizotumika kuboresha Miundombinu Reviewed by habari motto on 7:13 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.