Prof Jay Kuanza Kutimiza Ahadi Ndani Ya Miezi Sita

Mgombea ubunge jimbo la Mikumi, Joseph Haule maarufu Profesa Jay akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge na udiwani kupitia ukawa katika uwanja wa Bustani Mikumi mjini wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Sept 04/2015. PICHA/ Juma Mtanda


Na Juma Mtanda, Morogoro.
Mwanamuzi wa kizazi kipya ambaye ni ubunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule maarufu Profesa Jay alizindua kampeni za ubunge huku akiahidi kuanza kutafutia ufumbuzi kero mbalimbali ikiwemo kufuatilia kwa karibu mradi wa maji uliofadhiliwa na benki ya dunia wenye thamani ya sh800 katika vijiji 10 na fedha zake kudaiwa kutafunwa na wajanja mkoani Morogoro. ilikuwa 
Septemba 04/2015.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge, udiwani na urais katika mji mdogo wa Mikumi uwanja wa Bustani, Profesa Jay alieleza kuwa dhamira yake ya kuingia katika kinyang’anyiro hicho ni kusukuma mbele maendeleo na kupunguza changamoto ambazo anaweza kuzitafutia ufumbuzi ndani ya miezi sita.

Profesa Jay alisema kuwa endapo atashinda (wakati ule) katika uchaguzi mkuu, atashirikiana vizuri na viongozi wa ngazi zote na kuona wanapunguza kero moja baada ya ngingine kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora katika sekta za maji, elimu, kilimo na sanaa.

Alisema kuwa kati ya vipaumbele hivyo ataanza na mradi wa maji kwa kufuatilia kiasi cha fedha cha sh800 mil ambazo zimeyeyuka na kuacha mradi ukiyumba na wananchi kushindwa kufaidika. 

“Natangaza vipaumbele vyangu ambavyo tayari nimefanyia kazi na kuona ninaweza kutekeleza ndani ya miezi sita hasa katika sekta ya elimu, maji, kilimo na sanaa ili vijana wetu ambao wengi hawana ajira watakuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe kupitia muziki”.alisema Profesa Jay.
Aliongeza kwa kusema kuwa jimbo la Mikumi limekosa mwakilishi mwenye uchungu na maendeleo ya kweli kwa wananchi na kuweza kusaidia kutatua kero zao za msingi hasa katika sekta hizo na kero hizo zinaweza kutatuliwa kwa nguvu za mbunge kupitia fedha za mfuko wa jimbo na wahisani ili kuiletea maendeleo Mikumi.

Aliongeza kwa kueleza kuwa mji wa Mikumi una vyanzo vingi vya maji vinavyotokana na mito inayotiririsha maji ya kutosha lakini ubunifu, maalifa na kutoona mbali kumechangia wananchi kuteseka huku akiwatupia lawama wabunge waliotangulia kukosa mbinu hizo za kuwapunguzia matatizo hayo.

Kwa upande wa changamoto nyingine Profesa Jay alisema kuwa kiwango cha elimu kinazidi kushuka mwaka hadi mwaka kutokana na matokeo mabaya hasa kwa shule za sekondari na kutolea mfano kuwa mwaka jana, wanafunzi 73 walifanya mtihani wa taifa na wanafunzi 23 ndiyo waliofanikiwa kusonga mbele.

“Nitatumia kikamilifu fedha za mfuko wa jimbo ambazo zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali za afya, elimu, kilimo pamoja na miundombinu ya barabara na itasaidia pia kupunguza pia tatizo la wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari kukimbilia mijini”.alisema Haule.

Elimu ni kila kitu hivyo vijana wa Mikumi wamekuwa hawajiamini kwa sababu ya kukosa elimu ya kutosha na ili kuwajengea uwezo atalazimika kujenga shule ya utalii ili kuweza vijana kutumia vyema fulsa za hifadhi ya taifa ya Mikumi.

Kuna fulsa wanazikosa vijana wetu hapa Mikumi, ukiuliza ni nani anafaidika zaidi na hifadhi ya Mikumi utaelezwa watu wanaoishi nje ya mji huo ndio wanafaidika zaidi na hiyo inatokana na watu wengi kushindwa kuongea kiingereza huku kazi ya kuwapokea watalii na kuwatembeza bungeni ikifaidisha vijana wengine. Alisema Profesa Jay.

Akifafanua zaidi juu ya fedha za mfuko wa jimbo, alisema kuwa amejifunza mambo mengi kupitia kwa wabunge vijana wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (SUGU) na Joshua Nassari wa jimbo la Arumeru Mashariki namna walivyoweza kutumia vyema fedha za jimbo kwa kusomesha watoto wa walalahoi, masikini na kusaidia watu wasiojiweza ikiwemo na kujifunza siasa kupitia kwao.

Kwa upande wa afya alisema kuwa huduma za afya zitaboreshwa kwa kuziwezesha zahanati za kata kuwa na vifaa tiba na dawa za kutosha ili kusaidia kupunguza msokomano katika hosptali ya St Kizito Mikumi ambayo imekuwa tegemeo kubwa.

Profesa Jay alisema kuwa atahakikisha anawezesha kila zahanati ya kata kupata kitanda kimoja kwa ajili ya akinamama wajawazito kujifungulia na kununua magari matatu ya wagonjwa ili kusaidia kubeba wagonjwa wataohitaji msaada zaidi kupelekwa hospali za rufaa.

Lengo langu likitimia sitaona shida kuhamisha studio yangu ya kisasa ya Mwanalizombe Record kuhamishia Mikumi ili vijana wenye vipaji vya sanaa waweze kurekodi katika viwango vya kimataifa na kufanya kazi zao kukubaliki kila sehemu.CHANZO/MTANDA BLOG
Prof Jay Kuanza Kutimiza Ahadi Ndani Ya Miezi Sita Prof Jay Kuanza Kutimiza Ahadi Ndani Ya Miezi Sita Reviewed by habari motto on 6:48 PM Rating: 5
Powered by Blogger.