Rais Magufuli Aagiza Pesa Za Sherehe Ya Wabunge Zipelekwe Muhimbili.

Hii stori ilianza kuenea kwenye mitandao ya kijamii, wapo walioamini na wapo walioona kama huo ni ujumbe wa uzushi… wakati unavyozidi kusogea ukweli umezidi kuthibitika kwamba haikuwa uzushi, agizo hilo limetolewa na Rais Magufuli mwenyewe !!
Nakusogezea uthibitisho mwingine kutoka Ikulu, hii ni nukuu ya alichokisema Rais Magufuli kuhusu agizo hilo >>> “Nitaomba mnisamehe sana, inawezekana sherehe ya leo isiwe nzuri kama mlivyozoea, hakuna bia… inawezekana kama kuna chupa za wine ni chache, mengi ni mani na soda.”
Sentensi zake nyingine hizi hapa >>> “Nilipoambiwa kwamba zimechangwa shilingi milioni 250 kwa ajili ya sherehe, nikasema fedha hizo zipelekwe katika hospitali ya Taifa Muhimbili zikasaidie kununua vitanda“- Dk. J.P Magufuli.
Video yake hii hapa kwenye dakika mbili.

Lakini hili agizo liliwekwa pia kwenye Website ya Ikulu jana hiyohiyo
IKULU
Rais Magufuli Aagiza Pesa Za Sherehe Ya Wabunge Zipelekwe Muhimbili. Rais Magufuli Aagiza Pesa Za Sherehe Ya Wabunge Zipelekwe Muhimbili. Reviewed by habari motto on 5:11 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.