Aliyekuwa afisa habari wa klabu ya Yanga Bw. Jerry Muro ameamua kukubali hukumu iliyoolewa dhidi yake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayomtaka kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka mmoja.

Kupitia instagram, Muro ameandika:
Kila nikifikiria figisu za soka la Bongo aisee nachoka kabisa, let me walk away for a while though I will be missing my fans and my people wa kimataifa but I must walk away for a while.
Kamati ya nidhamu ya TFF ilimtia hatiani Jerry Muro kwa kosa la kupinga uamuzi wa TFF na kulishambulia kupitia vyombo vya habari shirikisho hilo la soka nchini ambapo kamati hiyo ilitoa adhabu ya kumfungia Muro kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja pamoja na faini ya shilingi milioni tatu za Tanzani
Jerry Muro aikubali adhabu ya TFF, atoa ujumbe huu kwa mashabiki wa Yanga
Reviewed by habari motto
on
1:00 PM
Rating: