Habari zilizotufikia muda huu zinaeleza kuwa msafara wa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye suti nyeusi)umepata ajali ambapo gari la DPP limepata ajali na kupinduka baada ya tairi la mbele kulia kupasuka wakati Dereva alipokuwa akijitahidi kuwekwapa watoto wawili waliokuwa wakivuka barabara ghafla na bila kuwa na tahadhari yoyote,ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Bwanga na msafara unaelekea Chato kutokea Geita.
Taarifa zinaeleza kuwa gari hilo limeishainuliwa na safari inaendelea huku
Dereva na Abiria wote akiwemo Mkurugenzi wa makosa ya jinai Mhe. Biswalo Mganga na msaidizi wake wakiwa wametoka salama.
Msafara Wa DKT Harrison Mwakyembe Wapata Ajali
Reviewed by habari motto
on
5:59 AM
Rating:
