Mtendaji wa Mtaa auawa



Mwili wa Afisa Mtendaji wa mtaa wa Kabwe Kata ya Ruanda jijini Mbeya Clementina Enock Monga (34)mkazi wa Uyole ya kati jijini Mbeya umekutwa baada ya kuuawa na mtu au watu wasiofahamika kisha kutupwa pembezoni mwa uwanja wa ndege wa zamani karibu na shule ya sekondari 
Samora.

Marehemu aliondoka majira ya mchana January mosi mwaka huu akiaga kwenda matembezini na gari ya familia yenye namba za usajili T 234 DGW aina ya Toyota Spacio rangi ya fedha. Tangu muda huo simu ya marehemu iliita bila kupokelewa hadi usiku wa manane . 

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba marehemu alikuwa na watu wanaomfahamu vizuri hivyo ameomba yeyote mwenye taarifa za watu waliohusika na lilipo gari hilo.

Hata hivyo Kidavashari amesema marehemu alikuwa eneo jingine kisha kutupwa eneo la uwanja wa ndege wa zamani. Aidha amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hili.
Mtendaji wa Mtaa auawa Mtendaji wa Mtaa auawa Reviewed by habari motto on 7:44 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.