Results for "UGANDA"

NDEGE YATUA BARABARANI HUKO UGANDA

8:57 PM

Ndege ndogo ikiwa imebeba wafanyakazi wa jeshi la Marekani imetua kwa dharura katikati ya barabara nchini Uganda baada ya kuishiwa mafuta.
Philip Mukasa msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda amesema ndege hiyo iliyokua imebeba abiria wanane wakiwemo wafanyakazi wawili wa ndege hiyo, ilikuwa iliyokua ikielekea Sudani ya Kusini baada ya rubani kugundua hakuwa na mafuta ya kutosha aliamua kurudi uwanja wa kimataifa wa Entebbe ndipo ikabidi itue kwa dhalura katikati ya barabara kwenye mji wa Mityana uliopo kilomita 67 (maili 41) kutoka mji mkuu wa Kampala.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa, rubani ametua ndege kwa dhalura katikati ya barabara na watu wote wametoka salama.

Haikujulikana ni kwa nini rubani hakuelekea Sudan ya Kusini na badala yake kaamua kutua katikati ya barabara baada ya ndege hiyo kuishiwa mafuta. 
NDEGE YATUA BARABARANI HUKO UGANDA NDEGE YATUA BARABARANI HUKO UGANDA Reviewed by habari motto on 8:57 PM Rating: 5

MAUWAJI MABAYA ZAIDI KUTOKEA UGANDA..

9:44 PM

WATU ZAIDI YA 50 WAUAWA UGANDA
Watu wasiopungua 50 wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia vituo vya polisi na kambi za jeshi nchini Uganda, kwa mujibu wa jeshi.
Miongoni mwa waliokufa ni washambuliaji 41 na polisi pamoja na raia 17.
Mashambulio hayo yametokea magharibi mwa Uganda, karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Jeshi limesema mashambulio hayo yalisababishwa na mzozo baina ya makabila hasimu, lakini kuna wasiwasi wa uwezekano wa kuzuka kwa waasi wa Uganda waliopo Mashariki mwa Kongo.
Mashambulio hayo yamelenga majeshi katika wilaya za Kasese, Ntoroko na Bundibugyo.
Msemaji wa jeshi amesema mashambulio hayo hayana uhusiano wowote na kundi la waasi la ADF, ambalo lilikuwa likifanya shughuli zake katika eneo hilo zaidi ya muongo mmoja uliopita.
"Tunachofahamu ni kuwa wanamgambo hawa hawana uhusiano na ADF-NALU, lakini tunachunguza kuona sababu hasa na nani wanawaunga mkono," amesema Paddy Ankunda, msemaji wa jeshi akizungumza na shirika la habari la Reuters.
Watu 17 walikamatwa na wanahojiwa kwa mujibu wa polisi.

 Watu wasiopungua 50 wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia vituo vya polisi na kambi za jeshi nchini Uganda, kwa mujibu wa jeshi.
Miongoni mwa waliokufa ni washambuliaji 41 na polisi pamoja na raia 17.

 Mashambulio hayo yametokea magharibi mwa Uganda, karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Jeshi limesema mashambulio hayo yalisababishwa na mzozo baina ya makabila hasimu, lakini kuna wasiwasi wa uwezekano wa kuzuka kwa waasiwa Uganda waliopo Mashariki mwa Kongo.
Mashambulio hayo yamelenga majeshi katika wilaya za Kasese, Ntoroko na Bundibugyo.

 Msemaji wa jeshi amesema mashambulio hayo hayana uhusiano wowote na kundi la waasi la ADF, ambalo lilikuwa likifanya shughuli zake katika eneo hilo zaidi ya muongo mmoja uliopita.
"Tunachofahamu ni kuwa wanamgambo hawa hawana uhusiano na ADF-NALU, lakini tunachunguza kuona sababu hasa na nani wanawaunga mkono," amesema Paddy Ankunda, msemaji wa jeshi akizungumza na shirika la habari la Reuters.
Watu 17 walikamatwa na wanahojiwa kwa mujibu wa polisi.
MAUWAJI MABAYA ZAIDI KUTOKEA UGANDA..  MAUWAJI MABAYA ZAIDI KUTOKEA UGANDA.. Reviewed by habari motto on 9:44 PM Rating: 5

NEW AUDIO; JOSE CHAMELEON WALE WALE

3:40 PM
bChameleone8
NI MSANII ANAYEPAA TOKA ANGA LA  UGANDA KUIBURUDISHA NAFSI YAKO KWA NYIMBO YAKE MPYA  INAYOKWENDA KWA JINA LA WALE WALE

NEW AUDIO; JOSE CHAMELEON WALE WALE NEW AUDIO; JOSE CHAMELEON WALE WALE Reviewed by habari motto on 3:40 PM Rating: 5

TISHIO UWANJA WA NDEGE WA ENTEBBE

10:11 AM

Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umetoa onyo ukisema kuna "tishio dhahiri ... kutoka kundi lisilojulikana" kushambulia uwanja wa ndege wa Entebbe. Onyo hilo limechapishwa kweye tovuti ya ubalozi huo kufuatia tahadhari nyingine iliyotolewa na mamlaka za Marekani siku ya Jumatano ya kuimarisha ulinzi katika viwanja vya ndege vya Mashariki ya Kati na Ulaya vyenye ndege za moja kwa moja kwenda na kutoka Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi, kuna tishio thabiti kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe leo kati ya saa tatu usiku hadi saa tano- imesema taarifa hiyo.
TISHIO UWANJA WA NDEGE WA ENTEBBE TISHIO UWANJA WA NDEGE WA ENTEBBE Reviewed by habari motto on 10:11 AM Rating: 5

ALICHOPOST COMEDIAN KANSIMEE KIKO HAPAA

8:34 AM

Akipaa kutoka anga la Uganda mwanadada maarufu na mchekeshaji (comedian) amekuwa akisifika sana kwenye tasnia ya uchekeshaji. 
Siku ya alhamisi alipost picha yake ambayo ni alionekana kama mwanamuziki wa hip hop. kofia juu , shingoni amezagaa cheni kubwa, hiyo suruali ndio kituko zaidi. na hapo chini alivaa raba kama za michael jordan.. on aalichocapture kwenye picha hiyoo

Captioned: ”Y’all wasap? Good morning y’all!!!!#100%swaggerific.”
Check her out

ALICHOPOST COMEDIAN KANSIMEE KIKO HAPAA ALICHOPOST COMEDIAN KANSIMEE KIKO HAPAA Reviewed by habari motto on 8:34 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.