Results for "michezo" na "brurudani"

Mo Salah achunguzwa

7:02 AM

Haki miliki ya picha

Related image
Mshambuliaji wa Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah anachunguzwa na polisi baada ya video yake kuibuka akionekana kuendesha gari akiwa bado anatumia simu.
Klabu yake inadaiwa kuwa ndiyo iliyopiga simu kwa polisi.
Polisi wa Merseyside wamethibitisha kupitia ujumbe wa Twitter kwamba video hiyo imekabidhiwa kitengo husika.
Msemaji wa Liverpool amesema waliwafahamisha polisi kuhusu video hiyo baada ya kuzungumza na mchezaji huyo
Ameongeza kwamba hatua zozote zinazohitajia kuchukuliwa kuhusu tukio hilo zitachukuliwa kwa kufuata mifumo ya ndani.
Video hiyo ambayo imesambazwa sana kwenye Twitter inaonekana kumuonesha mchezaji huyo, akiwa anatumia simu yake akiwa amelisimamisha kwa muda huku akiwa amezingirwa na mashabiki, wakiwemo watoto. Kisha analingurumisha gari na kundoka akiwa bado anaitumia simu yake.

SalahHaki miliki ya picha
Image captionVideo hiyo inayodaiwa kumuonesha Mo Salah akiendesha gari akiwa bado anatumia simu imesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii

Msemaji wa klabu hiyo amesema: "Klabu, baada ya kushauriana na mchezaji, imewafahamisha Polisi wa Merseyside kuhusu kanda hiyo ya video na matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa kupigwa kwa video hiyo."
"Tumezungumza na mchezaji huyo na tutashughulikia hatua nyingine zozote zinazohitajika kuchukuliwa kwa kutumia mifumo ya ndani.
"Hakuna yeyote kati ya klabu na mchezaji ambaye atatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hili."
Raia huyo wa Misri aliwafungia Liverpool magoli 44 msimu uliopita.
Mo Salah alifunga bao Jumapili katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England msimu huu ambapo aliwasaidia Liverpool kuwalaza West Ham 4-0.
Mabao hayo mengine yalifungwa na Sadio Mane (mawili) na Daniel Sturridge.
Mo Salah achunguzwa Mo Salah achunguzwa Reviewed by habari motto on 7:02 AM Rating: 5

Itazame Hapa Ratiba Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18

7:42 AM
Image result for Ligi Kuu Tanzania Bara
RATIBA ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017-2018 imetoka na itatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii, baina ya mabingwa watetezi, Yanga SC dhidi ya washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka nchini (TFF), michuano ijulikanayo kama Azam Sports Federation Cup Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Pazia la Ligi Kuu inayorushwa moja kwa moja na Televisheni ya Azam, litafunguliwa rasmi Agosti 27, mwaka huu kwa timu zote 16 kuingia viwanjani.










Itazame Hapa Ratiba Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18 Itazame Hapa Ratiba Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18 Reviewed by habari motto on 7:42 AM Rating: 5

Ijue Ligi Pekee Anayoshabikia Raisi Kim Jong-UN

6:36 AM
Image result for Kim Jong-UN

Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-UN amejibainisha kuwa ni shabiki mkubwa wa Ligi Kuu Italia ‘Serie A’.

Hayo yalibainika muda mfupi baada ya kinda wa miaka 18 Kwang-Song Han kufunga bao kwenye klabu yake ya Cagliari nchini Italia hivi karibuni.

Seneta wa Italia, Antonio Razzi hivi karibuni alipokutana na wawakilishi wa nchi za bara Asia, alielezwa kwamba siyo tu Rais Kim amekuwa akifuatilia maendeleo ya mshambuliajia Kwang-Son, pia ni shabiki mkubwa wa ligi hiyo kwa ujumla.

Rais huyo wa Korea yeye ni shabiki mkubwa wa timu za Italia na mara kwa mara hufuatilia mechi za timu hizo zinapocheza.

Kiongozi huyo anayeonekana kama dikteta, ilielezwa kwamba amekuwa akifuatilia kwa karibu ligi ya Seria A na maendeleo ya mchezaji wa nchi yake, Kwang-Son.

Pia amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara hilo kufunga bao kwenye Ligi ya Seria A.

Klabu ya Cagliari ilimsajili mchezaji huyo tangu Februari mwaka huu na mkataba wake utamalizika 2022.

Mchezaji mwingine wa Korea Kaskazini alisajiliwa klabu ya Fiorentina mwaka jana na amekuwa akicheza kwenye timu ya vijana kabla ya kutemwa mwishoni mwa mwaka 2016.
Ijue Ligi Pekee Anayoshabikia Raisi Kim Jong-UN Ijue Ligi Pekee Anayoshabikia Raisi Kim Jong-UN Reviewed by habari motto on 6:36 AM Rating: 5

Tukio zima la Miss Tanzania 2016, Tazama Hapa

8:05 AM
Leo kwa mara nyingine tena Tanzania imeingia kwenye Headline ya kumpata Miss Tanzania 2016 baada ya miaka miwili kupita bila kufanyika shindano la Miss Tanzania, Shindano la Miss Tanzania limefanyika Mwanza kwa mara ya kwanza na mrembo kutokea Kinondoni Dar es salaam Diana  Edward Lukumai amekuwa mshindi kwa kati ya warembo 30
3x6a0504
3x6a0491
Wa pili kushoto Lilian Kamazima, Miss Tanzania 2014
3x6a0535
Christian Bella, akitoa Burudani
3x6a0563
3x6a0500
3x6a0472
3x6a0428
Host wa shinadno la Miss Tanzania 2016, Jokati Mwegelo
3x6a0574
Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu
3x6a0615
3x6a0622
Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward Lukumai
3x6a0631
3x6a0650
Zawadi ya Miss Tanzania 2106
                                              KWA HISANI YA MILLARD AYO
Tukio zima la Miss Tanzania 2016, Tazama Hapa Tukio zima la Miss Tanzania 2016, Tazama Hapa Reviewed by habari motto on 8:05 AM Rating: 5

Dc Mtaturu Kuwakutanisha Vijana Kila Mwaka

9:23 AM
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu

Na Mathias Canal, Singida 

Mashindano ya kuibua vipaji vya wafukuza upepo kwa mbio ndefu Ikungi Half Marathon yanayotaraji kufika ukomo jumamosi hii Octoba 29, 2016 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mashindano hayo.

Vijana takribani 60 shupavu waliochomoza kwenye mchujo wa ngazi ya Vijiji, Kata na Tarafa  wataingia barabarani kuisaka ama heshima ya ushindi au ushiriki kwa ngazi ya Wilaya huku wengine waliokosa nafasi katika awamu hii kusubiri awamu ijayo katika mashindano ya Full Marathon yatakayofanyika Mwaka 2017.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amezungumza na washiriki wote wa mbio hizo ambapo amewapongeza kwa kujitokeza kwa wingi jambo ambalo linaonyesha kuwa mchezo huo una wahitaji wengi.

Mtaturu amesema kuwa mashindano haya ya Ikungi Half Marathon yanafanyika kwa mara ya kwanza na yatakuwa endelevu ambapo mwakani yatafanyika pia mashindano yam bio ndefu yatakayojulikana kama Ikungi Marathon 2017.

Dc Mtaturu alisema kuwa Dhamira ya kuanzishwa kwa mashindano haya ni kuibua vipaji kwa vijana na kuviendeleza, Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa vijana na kuwaandaa vijana katika Wilaya hii kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.
Mashindano ya mbio ndefu yenye umbali wa kilomita 21 yatahusisha vijana wenye umri wa kuanzia miaka 17 hadi 30 waishio Wilayani Ikungi na yanatarajiwa kufanyika kila mwaka ili kuinua hamasa ya Mchezo wa riadha hukuyakiambatana na mbio fupi za mita 100, mita 400 na mita 800.

Mashindano haya yalianza Septemba 3, 2016 kwa ngazi ya Vijiji, Octoba Mosi yalifanyika kwa ngazi ya Kata, ambapo mchujo wa ngazi ya Tarafa imemalizika Octoba 15, 2016 na hatimaye kupisha mchuano wa Kiwilaya.
Mashindano haya yatatoa fursa kwa vijana kuonyesha uwezo wao wa kucheza na miguu kwa kasi ya ushindani kwa maana ya manufaa ya pesa lakini pia itaimarisha ajira kupitia chama cha Riadha mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla lakini pia kuwaondoa vijana wengi katika mawazo ovu ya kushinda vijiweni badala yake kujitokeza kwa ajili ya kujihusisha na Kilimo pamoja na ufugaji.
Dc Mtaturu amewasihi washiriki wote kukimbia kwa kutumia muda mzuri ili iwe taswira ya rekodi nzuri katika ukimbiaji jambo litakalokifanya chama cha cha Riadha Taifa kuchagua vipaji vitakavyoendelezwa.
Dc Mtaturu Kuwakutanisha Vijana Kila Mwaka Dc Mtaturu Kuwakutanisha Vijana Kila Mwaka Reviewed by habari motto on 9:23 AM Rating: 5

Dullah Mbabe Athihirisha Ubabe Wake Kwa Mchina Chengbo Zheng

9:14 AM
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akimsukumia makonde mazito Bondia Chengbo Zheng kutoka nchini China na kupelekea mpambano huo kuisha ndani ya dakika mbili na sekunde kadhaa kwa 'KnockOut' ya kiufundi, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam usiku huu.
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akiendelea kumsukumia makonde mazito Bondia Chengbo Zheng yaliyompelekea kwenda chini na kuomba kutoendelea na mpambani huo.
Bondia Chengbo Zheng akimuomba msimamizi wake kumtoa 'Groves' baada ya kushindwa kuendelea na mchezo kufuatia makonde mazito na ya haraka haraka aliyoyapata kutoka kwa Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe (78.2KG) akitangazwa mshindi mara baada ya kumpiga kwa 'KnockOut' Bondia Chengbo Zheng (77.9KG) kutoka nchini China katika raundi kwanza kabisa ya mpambano wao usiokuwa wa Ubingwa uliomalizika usiku huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akimpongeza 
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe kwa ushindi alioupata wa kumpiga Bondia Chengbo Zheng kutoka nchini China, na kufanya heshima ya mchezo huo kuendelea kubaki nchini.
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akizungumza na vyombo vya habari.,
Katika mambano ya utangulizi, kulikuwa na pambano hili la raundi nane lililokuwa na mvuto wa aina yake lililowakutanisha mabondia Said Mbelwa (nyeupe) na Shaban Kaoneka. hili lilikuwa na pambano la rusha nirushe, ambapo Bondia Said Mbelwa alifanikiwa kushinda kwa 'KnockOut' ya kiufundi dakika ya saba ya mpambano huo.
Chukua hiyooooo...





Bondia Paul Kamata (nyeupe) akimsukumia makonde mithili ya mvua Bondia Buta Obed katika mpambano wao usio na ubingwa wa raundi nani, ulichezwa usiku wa leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam. Bondia Paul Kamata alishinda kwa 'KnockOut' ya kiufundi, katika raundi ya tano ya mchezo hio.







Dullah Mbabe Athihirisha Ubabe Wake Kwa Mchina Chengbo Zheng Dullah Mbabe Athihirisha Ubabe Wake Kwa Mchina Chengbo Zheng Reviewed by habari motto on 9:14 AM Rating: 5

Mwigulu amrejesha Pluijm Jangwani

1:10 AM

WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi na mwananchama wa Yanga, Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumshawishi kocha mholanzi Hans Van Pluijm arejee katika kazi yake ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao watetezi wa Ligi kuu.
Pluijm aliwasilisha barua ya kujiuzulu baada kupata taarifa ya kuwasili kwa kocha wa Zesco ya Zambia, George Lwandamina huku ikidaiwa kufanya mazungumzo na vigogo wa wanajangwani hao bila yeye kupewa taarifa yoyote.
Uongozi wa Yanga umemwandikia Pluijm barua ya kukataa ombi lake la kujiuzulu huku ikimtaka arejee kazini mara moja kuendelea na majukumu yake.

Nchemba alifanya vikao kadhaa na Pluijm na mwisho amefanikiwa kukamilisha adhma yake ya kuona kocha huyo aliyeipa ubingwa Yanga mara mbili mfululizo anabakia kukinoa kikosi hicho.
Mwigulu amrejesha Pluijm Jangwani Mwigulu amrejesha Pluijm Jangwani Reviewed by habari motto on 1:10 AM Rating: 5

Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi

2:17 PM

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger
Image captionMkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ana fursa nzuri ya kushinda ligi ya Uingereza msimu huu kwa mara ya kwanza tangu washinde taji hilo bila kushindwa mwaka 2004.
Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa klabu hiyo,Wenger mwenye umri wa miaka 67,alisema kuwa mshindi wa taji la ligi kuu atakuwa na kati ya pointi 82 na 86 mwaka huu.
Alisema: Hii leo tuko katika nafasi nzuri zaidi ya kuwania taji la ligi ya Uingereza ikilinganishwa na miaka mitano au sita iliopita.
Ninaamini tuna timu nzuri katika ligi yenye ushindani mkubwa.
Arsenal ni wa pili katika jedwali la ligi,ikiwa ni mojwapo ya timu tatu zenye pointi 20 na wako katika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya mabao.
Wenger anasema kuwa anafikiri kwamba anahitaji pointi 62 kutoka kwa mechi 29 zilizosalia kushinda taji .
Leicester ndio mabingwa wa taji hilo msimu uliopita.
''Baada ya mechi 9 ,tuna pointi 20,ikimaanisha kwamba ubingwa huo utaamuliwa na kati ya pointi 82 na 86'',alisema.

na BBC SWAHILI
Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi Reviewed by habari motto on 2:17 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.