WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi na mwananchama wa Yanga, Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumshawishi kocha mholanzi Hans Van Pluijm arejee katika kazi yake ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao watetezi wa Ligi kuu.
Uongozi wa Yanga umemwandikia Pluijm barua ya kukataa ombi lake la kujiuzulu huku ikimtaka arejee kazini mara moja kuendelea na majukumu yake.
Nchemba alifanya vikao kadhaa na Pluijm na mwisho amefanikiwa kukamilisha adhma yake ya kuona kocha huyo aliyeipa ubingwa Yanga mara mbili mfululizo anabakia kukinoa kikosi hicho.
Mwigulu amrejesha Pluijm Jangwani
Reviewed by habari motto
on
1:10 AM
Rating:
