Mshambuliaji wa Liverpool, Fabio Borini alifanya mazungumzo na Sunderland juu ya uwezekano wa kuhamia Kaskazini mashariki.
DILI la Fabio Borini kujiunga na Sunderland linaweza kurudi tena baada ya klabu hizo kufanya mazungumzo juu ya mshambuliaji huyo wa Liverpool.
Paka weusi waliweka mezani paundi milioni 14 mapema mwaka huu wakiitaka saini ya nyota huyo raia wa Italia.
Msimu uliopita, nyota huyo alikuwa na msimu mzuri wakati anacheza kwa mkopo ndani ya dimba la Stadium of Light.
Baada ya ofa ile kukubalika, ilionekana kama Borini anaweza kurudi Kaskazini mashariki.
Janga: Mshambuliaji wa Liverpool, Borini alipata majeruhi kwenye bega lake wakati wa mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu dhidi ya Roma
Borini akipata matibabu baada ya kuumia kwenye mechi dhidi ya Roma.
Hata hivyo nyota huyo mwenye miaka 23 alisafiri na Liverpool kwenye ziara ya Marekani na kuambulia majeruhi tu ya bega na kurudi Uingereza.
Tayari ameshazungumza na Sunderland, lakini majeruhi yameleta utata.
Majaribio ya Liverpool kumsajili mshambuliaji wa QPR, Loic Remy yameshindikana baada ya nyota huyo kushindwa kufuzu vipimo vya afya mwishoni mwa wiki na kocha Brendan Rodgers anasema hali ya Borini inaweza kumshawishi kununua mshambuliaji mwingine.
Dili limekamilika? Sunderland wamekubali kulipa ada ya uhamisho ya paundi milioni 14 ili kuinasa saini ya Borini aliyeng`ara msimu uliopita kwa mkopo.
FABIO BORINI WA LIVERPOOL KUIKACHA TIMU HIYO..
Reviewed by habari motto
on
4:01 PM
Rating: