Results for "michezo"

Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi

2:17 PM

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger
Image captionMkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ana fursa nzuri ya kushinda ligi ya Uingereza msimu huu kwa mara ya kwanza tangu washinde taji hilo bila kushindwa mwaka 2004.
Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa klabu hiyo,Wenger mwenye umri wa miaka 67,alisema kuwa mshindi wa taji la ligi kuu atakuwa na kati ya pointi 82 na 86 mwaka huu.
Alisema: Hii leo tuko katika nafasi nzuri zaidi ya kuwania taji la ligi ya Uingereza ikilinganishwa na miaka mitano au sita iliopita.
Ninaamini tuna timu nzuri katika ligi yenye ushindani mkubwa.
Arsenal ni wa pili katika jedwali la ligi,ikiwa ni mojwapo ya timu tatu zenye pointi 20 na wako katika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya mabao.
Wenger anasema kuwa anafikiri kwamba anahitaji pointi 62 kutoka kwa mechi 29 zilizosalia kushinda taji .
Leicester ndio mabingwa wa taji hilo msimu uliopita.
''Baada ya mechi 9 ,tuna pointi 20,ikimaanisha kwamba ubingwa huo utaamuliwa na kati ya pointi 82 na 86'',alisema.

na BBC SWAHILI
Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi Reviewed by habari motto on 2:17 PM Rating: 5

Leicester City yang'ara UEFA

6:02 AM

Riyad Mahrez na Islam Slimani waling'ara katika mchezo huo
Image captionRiyad Mahrez na Islam Slimani waling'ara katika mchezo huo

Klabu ya soka ya Leicester City imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Copenhagen.
Wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani King Power, Leicester walipata bao hilo dakika tano kabla ya kwenda mapumzikoni kupitia kwa Riyad Mahrez aliyekuwa katika kiwango cha hali ya juu baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mualgeria mwenzake Islam Slimani.

Islam Slimani alikataliwa bao baada ya kuotea
Image captionIslam Slimani alikataliwa bao baada ya kuotea

Kwa matokeo hayo Leicester wanabaki kileleni mwa kundi G wakiwa na alama 9 baada ya kushinda michezo yote mitatu ya ufnguzi wa ligi ya mabingwa Ulaya.
Timu pekee zilizowahi kushinda michezo mitatu ya ufunguzi katika michuano hiyo ni AC Milan, Paris St-Germain, Juventus na Malaga.

Matokeo mengine ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya

Bayer 04 Leverkusen 0-0 Tottenham Hotspur F.C.
CSKA Moscow 1-1 AS Monaco FC
Real Madrid 5-1 Legia Warsaw
Sporting 1 -2 Borussia Dortmund
Club Brugge 1-2 FC Porto
Dinamo Zagreb 0- 1 Sevilla
Lyon 0- 1 Juventus

credit kwa BBC swahili
Leicester City yang'ara UEFA Leicester City yang'ara UEFA Reviewed by habari motto on 6:02 AM Rating: 5

Hali Bado Ni Tete Simba SC

10:27 AM
Baada ya mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oyesterbay, ambao ulikuwa na ajenda 10, moja kati ya ajenda hizo ilikuwa ikizungumzia taarifa ya kamati ya maboresho ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Katika ajenda hiyo ndipo lilipojitokeza suala zima la MO ambapo wanachana hao wa Simba zaidi ya 700 waliojitokeza kwenye mkutano huo walitaka bilionea huyo apewe timu hiyo kutokana na hali mbaya ya kiuchumi iliyopo klabu hapo ambapo imekuwa ikijiendesha kwa hasara kila mwaka.
Katika msimu wa 2014/15 klabu hiyo ilifanikiwa kujikusanyia Sh bilioni 2, 096, 721, 493  kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya mapato lakini ikatumia Sh bilioni 2,101,100,303 na kujikuta ikidaiwa 4, 378,810.

Lakini pia katika bajeti yake ya msimu ujao wa 2016/17 uongozi huo unatarajia kukusanya kiasi cha Sh bilioni 3, 583, 000,000 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato lakini matumizi yake yanatarajiwa kuwa Sh bilioni 4, 411,025, 000, hivyo itakuwa ikidaiwa Sh milioni 828, 025, 000.

Kutokana na hali hiyo wanacha hao waliutaka uongozi huo, kukubali kumpatia Mo timu  kwani wanataka mabadiliko na wamechoshwa na hali hiyo ya ukata wa kila wakati ambao umekuwa ukiwatesa na kuwakosesha amani kila siku.

Hata hivyo uongozi wa klabu hiyo chini ya rais wake, Evans Aveva haukuwa tayari kufanya hivyo licha ya kelele za wanachama hao ambao kila wakati walikuwa wakiimba na kulitaja jina la MO.
Hali Bado Ni Tete Simba SC Hali Bado Ni Tete Simba SC Reviewed by habari motto on 10:27 AM Rating: 5

Jerry Muro Awaongoza Mashabiki Wa Yanga, Kwa Haji Manara Wa Simba

10:42 PM
Wanachama na mashabiki wa klabu ya Yanga wakiongozwa na Jerry Muro wamemtembelea mkuu wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Bw. Haji Manara na kumkabidhi mchango wao kwa ajili ya matibabu ya jicho lake ambalo limepoteza uwezo wa kuona.

Wanazi hao wa Yanga walifika nyumbani kwa Manara na kutoa mchango wao ambao walichanga kupitia makundi mbalimbali ya kwenye mitandao ya kijamii.

Manara anatarajiwa kusafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali katika hospitali kadhaa za hapa nchini.

Msemaji huyo wa wekundu wa Msimbazi amesema gharama kwa ajili ya matimu zinakadiriwa kuwa ni zaidi ya dola 10,000 za Marekani.

Manara amewashukuru mashabiki hao kutokana na moyo wao wa kiungwana wa kumtembelea kwa ajili ya kumsalimia na kumjulia hali lakini pia kukabidhi mchango wao katika jitihada za kuhakikisha anapata matibabu.

“Mimi niwashukuru sana kwa mchango wenu, mnaweza mkakakiona kidogo lakini hakuna kidogo katika tiba. Ni kweli gharama ya matibabu ni kubwa ni zaidi ya dola 10,000 lakini hiki kitakuwa ni sehemu kitakuwa ni sehemu ya mchango mkubwa, kwanza si kwa suala la kiasi lakini ni kwasababu kimetoka kwa watu ambao wameonesha utamaduni unaotakiwa,” alisema Manara wakati akitoa shukrani kwa mashabiki wa Yanga waliomtembelea nyumbani kwake.
Jerry Muro Awaongoza Mashabiki Wa Yanga, Kwa Haji Manara Wa Simba Jerry Muro Awaongoza Mashabiki Wa Yanga, Kwa Haji Manara Wa Simba Reviewed by habari motto on 10:42 PM Rating: 5

Simba yashikwa Shati na STAND UNITED

8:19 PM

Kikosi cha Simba...

Kikosi cha Stand United...

Kipa wa Stand United, John Mwenda, akidaivu kudaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba Amis Tambwe, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa tAIFA Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1. Picha kwa hisani ya Habari Mseto
MATOKEO YA MECHI NYINGINEZO ZA LIGI KUU ZILIZOPIGWA LEO NI :- 

SIMBA 1- STAND UNITED 1
PILISI MORO 1- KAGERA SUGAR 1
AZAM FC 0 - TANZANIA PRISONS 0
RUVU SHOTING 0 - MBEYA CITY 0
COASTAL UNION 2 - NDADA FC 1
Simba yashikwa Shati na STAND UNITED Simba yashikwa Shati na STAND UNITED Reviewed by habari motto on 8:19 PM Rating: 5

CHELSEA YAMNASA, MNYONGE WA LIVERPOOL

8:51 AM


Wakati Liverpool walimuona hana afya njema kwa kufeli vipimo vya afya, Chelsea imemsajili mshambuliaji Loic Remy raia wa Ufaransa.

Remy kutoka QPR ametua Chelsea kwa mkataba wa miaka minne wenye thamani wa pauni milioni 8.

Chelsea imemsajili Mfaransa huyo huku Arsenal ikiwa katika hatua za mwisho kumnasa, lakini wapi 

CHELSEA YAMNASA, MNYONGE WA LIVERPOOL CHELSEA YAMNASA, MNYONGE WA LIVERPOOL Reviewed by habari motto on 8:51 AM Rating: 5

MANJI AKASIRIKA, ATISHIA KUINUNUA SIMBA YOTE

12:32 PM

YETU macho katika hili; Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi, ambaye juzi jioni alijiunga na Simba kudai kuwa atapambana na Wanajangwani hao kuhakikisha haki yake inapatikana.


Maneno hayo ya Okwi yamekuja baada ya kudai kuwa Yanga imevunja naye mkataba kisha 
kumfungulia mashtaka katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa madai ya kushindwa 
kuzingatia makubaliano yake na klabu hiyo kwa mujibu wa mkataba wake.

Akizungumza Okwi atahakikisha anapambana Yanga hadi hatua ya mwisho kuhakikisha
 anapata haki yake.Alisema klabu yoyote ile inapoingia mkataba na mchezaji inatakiwa 
kumlipa fedha zake zote za usajili kwa mujibu wa makubaliano na siyo kumzungusha na 
kufanya mambo yake kama viongozi wake wanavyotaka.

“Sina hofu kabisa juu ya jambo hili, naamini haki itapatikana kwa sababu hayo ambayo 
Yanga wananipakazia hayana ukweli wowote na kama kuna ukweli basi kutakuwa na 
sababu.

Hata hivyo kwa sasa haina haja ya kuongea mambo mengi ila jambo la msingi ambalo
 ningependa kusema ni kwamba, nipo tayari kusimama sehemu yoyote ile juu ya jambo
 hili ili kuhakikisha haki yangu inapatika.
 
“Hata kama TFF na Fifa watanihitaji leo hii nitasimama mbele yao na kutoa ushahidi 
wangu juu ya jambo hili,” alisema Okwi ambaye Yanga imeachana naye akiwa bado na 
mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
 
Yanga ilimsajili Okwi akitokea SC Villa ya Uganda ambayo alijiungana nayo akitokea Etoile
 du Sahel ya nchini Tunisia ambayo alikuwa na matatizo nayo.

MANJI AKASIRIKA, ATISHIA KUINUNUA SIMBA YOTE MANJI AKASIRIKA, ATISHIA KUINUNUA SIMBA YOTE Reviewed by habari motto on 12:32 PM Rating: 5

PICHA ZA MATUKIO; OKWI NDANI YA SIMBA TENA

1:24 PM


Mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi akitambulishwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba Zakaria Hans Pope.
Staili ile ile waliyotumia mahasimu wao Dar es salaam Young Africans kumpata mshambuliaji mganda Emmanuel Arnold Okwi ndiyo ambayo klabu yake ya zamani, wekundu wa Msimbazi Simba SC imeitumia kumrejesha kundini Mganda huyo hii leo
“Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji
“Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe
Tayari Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF na ataungana na mganda mwenzake, Joseph Owino, Warundi Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa kigeni
Kwa upande wake Okwi ambaye ameahidi makubwa msimu huu mara baada ya kurejea hii leo alianza kuichezea Simba kwa mara ya kwanza akiwa kinda wa miaka 17 akitokea Sports club Villa ya Uganda mnamo mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia
Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu na hivyo Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao
Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani
Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo
Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu mwezi Machi, ikiwa ni miezi minne tangu asajiliwe.
Lakini majaliwa ya mshambuliaji huyo mwenye kasi ya kutisha na uwezo wa kufumania nyavu kuichezea Simba kwa sasa yako mikononi mwa TFF na FIFA.

PICHA ZA MATUKIO; OKWI NDANI YA SIMBA TENA PICHA ZA MATUKIO; OKWI NDANI YA SIMBA TENA Reviewed by habari motto on 1:24 PM Rating: 5

FIGGO NDANI YA BONGO

9:46 PM
Mchezaji Luis Figo akiwa katika picha ya pamoja na mtangazaji wa E FM 93.7 Mauld Kitenge wakati alipowasili usiku huu katika uwanja wa kimataifa wa JNIA Dar tayari kwa mechi yao ya Jumamosi ya wachezaji wa zamani wa Real Madrid watakapokipiga mechi ya kirafiki na wachezaji wazamani wa Tanzania waliowahi chezea Timu ya Taifa na club ya Yanga na Simba wanaojulikana kama Tanzania Eleven siku ya Jumamosi Aug 23, 2014 uwanja wa Tai
FIGGO NDANI YA BONGO FIGGO NDANI YA BONGO Reviewed by habari motto on 9:46 PM Rating: 5

ROJO ATUA MAN UNITED

11:00 AM
KLABU ya Manchester United imekubali kutoa Pauni Milioni 16 kumnunua beki wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo.Rojo, ambaye ametua mjini Manchester leo na kusema kuhamia United ‘anahisi kama ndoto’, anatarajiwa kusaini Mkataba wa miaka minne akifaulu vipimo vya afya na kukubali vipengele binafsi vya kandarasi yake.Louis van Gaal ametoa kipaumbele kwa usajili wa beki huyo mtumia mguu wa kushoto, Rojo, mwenye umri wa miaka 24, kufuatia kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England Jumamois na Swansea.Winga Luis Nani, aliyejiunga na United kutoka Sporting kwa Pauni Milioni 17 mwaka 2007, amerejeshwa kwa mkopo klabu yake hiyo ya zamani, ilia ni sehemu ya dili hilo la Rojo.
Amewasili: Marcos Rojo amewasili England leo kwa ajili ya kukamilisha usajili wake Manchester United
ROJO ATUA MAN UNITED ROJO ATUA MAN UNITED Reviewed by habari motto on 11:00 AM Rating: 5

YANGA YAKUBWA NA JANGA LINGINE...

2:47 PM
Uongozi wa klabu ya Young Africans unasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Dereva wa Bus Kubwa la Wachezaji (Yutong) Bw Maulid Kiula kilichotokea alfajiri ya leo Ilala jijini Dar es salaam.

Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu mtaa wa Chunya karibu na Bungoni Ilala jijini Dar es salaam.

Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi Amen.


                         hili ndilo bus alilokuwa akiendesha marehemu
YANGA YAKUBWA NA JANGA LINGINE... YANGA YAKUBWA NA JANGA LINGINE... Reviewed by habari motto on 2:47 PM Rating: 5

TETESI ZA USAJILI ULAYA

12:41 PM
Beki wa Liverpool Kolo Toure, 33, anajiandaa kujiunga na Trabzonspor ya Uturuki katika mkataba wa pauni milioni 1.5 (Daily Mail), boss wa Liverpool Brendan Rodgers anafikiria kumchukua mshambuliaji kutoka Cameroon, Samuel Eto'o, 33, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Chelsea msimu uliopita (Guardian), Galatasaray wanafikiria kutoa pauni milioni 28 kuwachukua Joel Campbell, 22, na Lukas Podolski, 29, kutoka Arsenal (Daily Express), QPR wapo tayari kumtoa Loic Remy, 27, kubadilishana na Andros Townsend, 23, na Harry Kane, 21 kutoka Tottenham (CaughtOffside), Remy pia huenda akawindwa na Chelsea, wakati Jose Mourinho akitafuta mchezaji wa kuziba pengo la Didier Drogba, 36, aliyeumia (Goal), kiungo kutoka Spain Santi Cazorla, 29, ametupilia mbali tetesi kuwa anataka kuondoka Arsenal na kurejea La Liga (Daily Mirror), Stoke City wamepanda dau jipya na kutoa pauni milioni 5 kutaka kumchukua winga wa Norwich Nathan Redmond, 20 (Daily Mail), Aston Villa wanakaribia kumchukua Carlos Sanchez, 28, kwa pauni milioni 3.5 (Birmingham Mail), mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba huenda asiweze kucheza kwa miezi minne baada ya kuumia 'enka' katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ferencvaros (Daily Mirror), Southampton huenda wakampiga faini Morgan Schneiderlin, 24, iwapo kiungo huyo Mfaransa atakataa kucheza mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili (Daily Telegraph), kipa wa Manchester City Willy Caballero, 32 amemwambia kipa mwenzake Joe Hart, 27, atalazimika kupigania namba moja, Etihad (Telegraph), Chelsea wanamfuatilia beki wa kati wa Roma, Mehdi Benatia, 27, ambaye anadhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30 (Daily Mirror), Arsenal wanafikiria kutoa pauni milioni 10 kumshawishi beki wa kati wa Liverpool Daniel Agger (The Sun), Everton na Tottenham wako 'macho' baada ya kuambiwa Salomon Kalou anaweza kuondoka Lille kabla ya dirisha la usajili kufungwa (Daily Mirror), Arsenal wapo tayari kumfuatilia beki wa Olympiakos Kostas Manolas kuziba pengo la Thomas Vermaelen aliyekwenda Barcelona (Daily Express).
TETESI ZA USAJILI ULAYA TETESI ZA USAJILI ULAYA Reviewed by habari motto on 12:41 PM Rating: 5

ARSERNAL TO BARCELONA.. WENGER AZIDI KUUZA TU

1:33 AM
BARCELONA IMEONYESHA KUVUTIWA NA KAZI YA KOCHA ARSEN WENGER WA ARSENAL.ANGALIA NAMNA AMBAVYO IMEKUWA IKIBEBA WACHEZAJI WA CHAGUO LAKE.
ARSERNAL TO BARCELONA.. WENGER AZIDI KUUZA TU ARSERNAL TO BARCELONA.. WENGER AZIDI KUUZA TU Reviewed by habari motto on 1:33 AM Rating: 5

HUYU NDIYE ALIYETIMULIWA NA TIMU YA SIMBA SPORTS CLUB

1:49 PM
Simba imemtimua kocha wake, Zdravko Logarusic ikiwa ni siku moja tu baada ya kufungwa mabao 3-0 na Zesco ya Zambia.Loga anatuhumiwa kuzozana na wachezaji mara baada ya mechi akiwatuhumu kuonyesha kiwango duni.Uongozi wa Simba umechukua uamuzi huo baada ya kikao cha takribani masaa matano.

Tayari Simba imeanza kufanya maarifa ya kumpata kocha mpya.
HUYU NDIYE ALIYETIMULIWA NA TIMU YA SIMBA SPORTS CLUB HUYU NDIYE ALIYETIMULIWA NA  TIMU YA SIMBA SPORTS CLUB Reviewed by habari motto on 1:49 PM Rating: 5

MJUE MCHEZAJI WA KIKE ALIYEWAVUTIA WANAUME WENGI KUJA UWANJANI.. VIDEO CHECK HAPA

6:17 PM

Kwa kawaida mashabiki wa mpira wa miguu, mpira mikono, mpira wa kikapu au hata ‘handball’ huingia kwa wingi uwanjani kushangilia mechi kati ya timu zao na wapinzani. Lakini hii imekuwa tofauti kwa mashabiki wa mpira wa Volleyball huko Taiwan.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimeeleza kuwa wadau wa mpira wa Volleyball wamemlalamikia mchezaji wa kike mrembo na mwenye mvuto haswaa anaefahamika kwa jina la Sabina Altynbekova  kuwa chanzo cha kuharibu uhalisia na utamu wa mechi za mchezo huo pale timu yake inayoitwa ‘Kazakhstan’ inapokutana na timu nyingine.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa umati wa mashabiki hasa wanaume wanaonekana kuwa huingia uwanjani kumuangalia zaidi msichana huyo mwenye umri wa miaka kati ya 17 na 18, na hivyo mvuto wake huharibu uhalisia wa mechi kwa kuwa kila anaposhika mpira hushangiliwa sana kama ndiye mchezaji pekee kitu ambacho kinaonekana kuwa tatizo hata kwa wachezaji wenzake.
Kocha wa timu hiyo, Nurlan Sadikov pia ameonekana kusikitishwa na hali hiyo inayoathiri saikolojia ya wachezaji wengine wa timu yake.


 Haiwezekani ifanyike hivi…umati wa watu unafanya kama vile kuna mchezaji mmoja tu kwenye hii ligi hii ya mabingwa.
Kocha  Sadikov aliiambia Tengrin News.
Video ya sabina, Altynbekova iliwekwa YouTube wiki iliyopita na tayari imeshatazamwa zaidi ya 1, 153, 646.
MJUE MCHEZAJI WA KIKE ALIYEWAVUTIA WANAUME WENGI KUJA UWANJANI.. VIDEO CHECK HAPA MJUE MCHEZAJI WA KIKE ALIYEWAVUTIA WANAUME WENGI KUJA UWANJANI.. VIDEO CHECK HAPA Reviewed by habari motto on 6:17 PM Rating: 5

FABIO BORINI WA LIVERPOOL KUIKACHA TIMU HIYO..

4:01 PM
Mshambuliaji wa Liverpool, Fabio Borini alifanya mazungumzo na Sunderland juu ya uwezekano wa kuhamia Kaskazini mashariki.
DILI la Fabio Borini kujiunga na Sunderland linaweza kurudi tena baada ya klabu hizo kufanya mazungumzo juu ya mshambuliaji huyo wa Liverpool.
Paka weusi waliweka mezani paundi milioni 14 mapema mwaka huu wakiitaka saini ya nyota huyo raia wa Italia.
Msimu uliopita, nyota huyo alikuwa na msimu mzuri wakati anacheza kwa mkopo ndani ya dimba la Stadium of Light.
Baada ya ofa ile kukubalika, ilionekana kama Borini anaweza kurudi Kaskazini mashariki.
Janga: Mshambuliaji wa Liverpool, Borini alipata majeruhi kwenye bega lake wakati wa mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu dhidi ya Roma
Borini akipata matibabu baada ya kuumia kwenye mechi dhidi ya Roma.
Hata hivyo nyota huyo mwenye miaka 23 alisafiri na Liverpool kwenye ziara ya Marekani na kuambulia majeruhi tu ya bega na kurudi Uingereza.
Tayari ameshazungumza na Sunderland, lakini majeruhi yameleta utata.
Majaribio ya Liverpool kumsajili mshambuliaji wa QPR, Loic Remy yameshindikana baada ya nyota huyo kushindwa kufuzu vipimo vya afya mwishoni mwa wiki na kocha Brendan Rodgers anasema hali ya Borini inaweza kumshawishi kununua mshambuliaji mwingine.
Dili limekamilika? Sunderland wamekubali kulipa ada ya uhamisho ya paundi milioni 14 ili kuinasa saini ya Borini aliyeng`ara msimu uliopita kwa mkopo.
FABIO BORINI WA LIVERPOOL KUIKACHA TIMU HIYO.. FABIO BORINI WA LIVERPOOL KUIKACHA TIMU HIYO.. Reviewed by habari motto on 4:01 PM Rating: 5

CHRISTIANO RONALDO AZIDI KUPAA.. AMBWAGA MESSI KWA KUTWAA TUZO BORA DUNIANI..

11:19 AM

439340_heroa
CRISTIANO Ronaldo ameshinda tuzo ya Goal 50 ya mchezaji bora wa dunia baada ya kuwa na msimu mzuri wa 2013-14.
 Mshambuliaji huyo ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu kama sehemu ya kuheshimu kazi aliyoifanyia Real Madrid kutwaa taji la 10 la ligi ya mabingwa barani Ulaya.
 Nyota huyo mwenye miaka 29, pia alishinda kombe la mfalme (Copa del Rey) na kufunga magoli 51 katika mashindano yote ya klabu na taifa lake.
 WALIOSHINDA TUZO YA Goal 50 mpaka sasa:
2008- Cristiano Ronaldo
2009 -Lionel Messi
2010- Wesley Sneijder
2011-Lionel Messi
2012- Cristiano Ronaldo
2013 -Lionel Messi
2014 -Cristiano Ronaldo.
 Ronaldo alishinda kiatu cha dhahabu sambamba na Luis Suarez na mapema mwaka huu alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia na kushinda tuzo ya 2013 FIFA Ballon d`Or.
 Baada ya kupokea tuzo hiyo, Ronaldo alisema: “Ni heshima kubwa kwangu kuchaguliwa kuwa mchezaji bora. Kiukweli nimefurahi sana”.
 “Nashawishika kusema nisingeweza kutwaa tuzo hii bila sapoti kutoka watu wa Real Madrid”.
 Goal 50 ni moja ya tuzo za heshima kwenye mchezo wa soka kwasababu wanaochagua wanatoka katika mitandao mikubwa ya soka duniani.
 Kura zinapigwa baada ya kumalizika kwa misimu ya ligi za ndani na mashindano ya kimataifa na wanaopiga kura wanatoka mataifa mbalimbali.
 Zaidi ya waandishi wa habari 600 kutoka katika machapisho 35 wanachagua wachezaji 50 wa juu kwenye tuzo hiyo.
Ronaldo ameongoza mwaka huu akifuatiwa na Arjen Robben, aliyeifanyia makubwa Uholanzi katika fainali za kombe la dunia na kuisaidia klabu yake ya Bayern kutwaa makombe manne msimu wa 2013-14.
Mshindi wa mwaka jana, Lionel Messi alishika nafasi ya tatu baada ya msimu mbaya katika klabu yake ya Barcelona na kushindwa kutwaa kombe la dunia nchini Brazil.


CHRISTIANO RONALDO AZIDI KUPAA.. AMBWAGA MESSI KWA KUTWAA TUZO BORA DUNIANI.. CHRISTIANO RONALDO AZIDI KUPAA.. AMBWAGA MESSI  KWA KUTWAA TUZO BORA DUNIANI.. Reviewed by habari motto on 11:19 AM Rating: 5

LIVERPOOL WAVUNJA REKODI... WAMSAJILI DEJAN LOVREN

10:50 AM
BEKI wa kimataifa wa Croatia, Dejan Lovren amekamilisha uhamisho wake kutua Liverpool kwa
dau la Pauni 20 kutoka Southampton.
Sasa mchezaji huyo anaweka rekodi ya kuwa beki ghali zaidi kuwahi kusajiliwa na Wekundu hao wa Anfield akipiku dau la Pauni Milioni 18.6, ambalo Liverpool ililipa kumsajili beki wa Paris St
Germain, Mamadou Sakho Septemba mwaka jana.
Lovren, ambaye amekuwa mlengwa chaguo la kwanza la beki wa kati katika mawindo ya kocha
Brendan Rodgers dirisha hili la usajili, amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kufuzu
vipimo vya afya Merseyside.


Sasa ni mwekundu wa Anfield: Lovren akiwa ameshika jezi ya Liverpool viwanja vya mazoezi vya
timu hiyo, Melwood 
On the move: Dejan Loven has sealed a £20m switch to Liverpool from Southampton
Lovren sasa ni beki ghali zaidi kihistoria kuwahi kutokea Liverpool 

LIVERPOOL WAVUNJA REKODI... WAMSAJILI DEJAN LOVREN LIVERPOOL WAVUNJA REKODI... WAMSAJILI DEJAN LOVREN Reviewed by habari motto on 10:50 AM Rating: 5

TETESI ZA SOKA MAJUU..

4:40 PM

West Ham wanataka kumsajili mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto'o, 33 ambaye aliondoka Chelsea msimu uliopita (Sun on Sunday), Inter Milan wanafikiria kumtoa Fredy Guarin, 28, kubadilishana na Javier Hernandez, 26, kutoka Manchester United (Sun on Sunday), Romelu Lukaku aliyecheza Everton kwa mkopo msimu uliopita, anataka uhamisho wa kudumu kwenda Goodison Park (Talksport), Arsenal wanakaribia kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Shakhtar Donetsk, Douglas Costa, 23 ambaye ameomba kuondoka Ukraine kwa sababu za matatizo ya kisiasa nchini humo (Caughtoffside), Atlètico Madrid wamefikia makubaliano ya kumsajili Antoine Griezmann, 23 kutoka Real Sociedad kwa pauni milioni 24 (AS), meneja wa. Manchester United bado ana nia ya kumsajili kiungo wa Roma Kevin Strootman, 24, licha ya mchezaji huyo kuwa majeruhi kutokana na kuumia goti (Sky Sports), Real Madrid wanapanga kumchukua Radamel Falcao, 28, kwa mkopo na uhamisho wa kudumu mwaka 2015 (AS), jaribio la Stoke City kumsajili Oussama Assaidi, 25, kutoka Liverpool kwa pauni milioni 7, huenda likashindikana kutokana na winga huyo kutaka mshahara mkubwa (Daily Express), mshambuliaji wa Lille Divock Origi, 19, anakaribia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 12.5 kwenda Liverpool (Sunday Mirror), Sami Khedira anataka mshahara wa pauni milioni 7.1 kwa mwaka ili kujiunga na Arsenal (La Sexta), Arsenal wanafikiria kupanda dau kumchukua kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin (Daily Star), Angel Di Maria anajiandaa kusaini mkataba wa miaka mitano siku chache zijazo na Paris St-Germain (Marca).

TETESI ZA SOKA MAJUU.. TETESI ZA SOKA MAJUU.. Reviewed by habari motto on 4:40 PM Rating: 5

MANCHESTER CITY WAISAMBARATISHA SPOTING KANSAS

9:49 AM
NI MECHI ZA MAJARIBIO AMBAPO ILICHEZA MANCHESTER CITY THIDI YA SPOTING KANSAS ILIYOPOKEA KICHAPO CHA MABAO 4 KWA 1.




MANCHESTER CITY WAISAMBARATISHA SPOTING KANSAS MANCHESTER CITY WAISAMBARATISHA SPOTING KANSAS Reviewed by habari motto on 9:49 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.