Wakati ikidaiwa kuwa mwanadada Aunt Ezekiel anamzunguka Wema Sepetu na kula Penzi la shemeji yake Diamond, sasa ameamua kufunguka na kudai kuwa kamwe hawezi kumsaliti Wema na kikubwa anachokiheshimu ni kwamba anajua Diamond ni mpenzi wa ndugu yake.....
Aunt
alisema hajawahi kulala na Diamond, wala kumuomba kutoka
kimapenzi kama watu wanavyodhani bali wao ni marafiki wa
karibu kwani anatambua kuwa Wema anampenda Diamond, na ndio
maana wakati wote wanakuwa pamoja na si kwamba yeye ana lengo
la kuchukua nafasi hiyo.....
"Mimi
jamani sijawahi kutoka na Diamond na wala sina lengo
hilo,najua yeye ni shemeji yangu kwa Wema,sasa inakuwaje na
mimi nijipeleke wakati najua kinachoendelea?
"Hayo
mambo siwezi kufanya na ninachohitaji kuwaambia mashabiki wangu
ni kwamba kila mmoja ana mpenzi wake na hatuwezi kuibiana
wanaume kama inavyodhaniwa," alisema Aunt.
Hata hivyo alisema kuwa safari zote wanazokuwa pamoja ni jibu tosha na kama angetaka kufanya hivyo ni wazi wangegombana na rafiki yake, kitu ambacho hataki kiwe hivyo.
MHHH.....KAMA HUJUI BASI JUA ALICHOKISEMA AUNT EZEKIEL KUHUSU MAHUSIANO YAKE NA DIAMOND
Reviewed by habari motto
on
9:31 AM
Rating:
Reviewed by habari motto
on
9:31 AM
Rating:
