VIDEO: MABOMU YA MACHOZI YATUMIKA KUWATAWANYA WATU HUKO IRINGA



Jeshi la polisi mkoani Iringa limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi ambao walivamia na kuanza kuchota mafuta kwenye lori la kubeba mafuta baada ya kupata ajali. 

 
Ajali hiyo imetokea jana eneo la msitu wa serikali wa Saohil wilayani Mufindi kwenye barabara kuu ya Iringa –Mbeya ambapo watu wawili walijeruhiwa kwenye ajali hiyo.
 
Polisi wamelazimika kutumia mabomu kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakiendelea kumiminika kutaka kuiba mafuta kwenye lori hilo ili kuwaepusha na hatari ambayo ingeweza kutokea kama lori hilo lingeshika moto.
 
Mashuhuda wamesema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi ya mbele ya lori la mizigo lililokuwa linatokea mkoani Mbeya na hivyo kukosa mwelekeo na kuligonga gari la kubeba mafuta lililokuwa linatokea mkoani Iringa na kuanguka.
 
Jeshi la polisi mkoani iringa limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea.



 
VIDEO: MABOMU YA MACHOZI YATUMIKA KUWATAWANYA WATU HUKO IRINGA VIDEO:  MABOMU YA MACHOZI YATUMIKA KUWATAWANYA WATU HUKO IRINGA Reviewed by habari motto on 9:36 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.