MUME AUWA MKE KISA WIVU WA MAPENZI

Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Ntarikwa manispaa ya Tabora aliyefahamika kwa jina la Rehema Hassan(28) anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na mumewe baada ya ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi usiku wakiwa nyumbani kwao.Tukio hilo la kusikitisha limetokea mwishoni mwa wiki majira ya saa saba usiku wakati wanandoa hao walipokuwa wameingia ndani kwa lengo la kutaka kulala.
Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Kijiji cha Ntarikwa Bw. Ali Hamisi Mdaki amemtaja mwanaume aliyemuua mkewe ni Hamad Mohammed Kasanzu(25)ambaye alidai alifanya mauaji hayo baada ya kumkuta na barua iliyokuwa ikihisiwa ya mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.
Mdaki alisema ugomvi huo wa wivu wa kimapenzi kati ya Hamad na mkewe ambaye kwasasa ni marehemu ulisababisha mwanaume huyo kumpiga na kumjeruhi vibaya mkewe na baada ya kutekeleza unyama huo alikimbia kusikojulikana na kumuacha mkewe chumbani akiwa amepoteza maisha huku chumba cha pili mke mwingine ambaye ni bimkubwa akimuonya kutoeleza ukweli wa tukio hilo la kinyama
MUME AUWA MKE KISA WIVU WA MAPENZI MUME AUWA MKE KISA WIVU WA MAPENZI Reviewed by habari motto on 9:45 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.