Mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Katika hali ya kushangaza madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam walipigwa na butwaa baada ya mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi kufikishwa hospitalini hapo akiwa amekatwa seheme zake za siri na mtu aliyedaiwa ni mganga wa kienyeji na kukimbilia kusikojulikana.Akizungumza kwa masikitiko makubwa wiki iliyopita, baba wa mtoto huyo, Ismail Kamaga alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Kijiji cha Omukagando, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Alisema mganga huyo aliyemtaja kwa jina moja la Adinali alifanya kitendo hicho kwa watoto wawili akidai anawafanyia tohara.“Alidai anawafanyia tohara watoto wawili, baada ya muda mwenzake alipona wa kwangu hakuna kitu na nyeti aliondoka nayo, sina namna tena ya kumsaidia mwanangu.
Nilimpeleka Hospitali ya Mugawa, Kagera ambako aliwekewa mpira wa kutolea haja ndogo na madaktari wakasema hawana jinsi.“Pia nilikwenda Kituo cha Polisi Karagwe kuomba msaada wa kumkamata mtuhumiwa lakini imeshindikana,” alisema baba Mzazi wa mtoto huyo
HUYU NDIYE MTOTO AMBAYE ANAYEISHI KWA NGUVU ZA MUNGU... MGANGA ATOWEKA NA SEHEMU ZAKE ZA SIRI
Reviewed by habari motto
on
9:52 AM
Rating: