RAISI KIKWETE AFANYA MAENDELEO KUSINI MWA TANZANIA


RAIS DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIFUNUA JIWE LA MSINGI KUFUNGUA RASMI BARABARA YA KILOMETA 78 YA PERAMIHO –MBINGA MJINI JULAI 19,2014.WENGINE KATIKA PICHA KUTOKA KUSHOTO NI MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE,WAIRI WA UJENZI DKT.JOHN POMBE MAGUFULI, KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA BWANA SERVASIUS LIKWELILE, MWENYEKITI WA MFUKO MCC TANZANIA BWANA BERNARD MCHOMVU. PICHA NA FREDDY MARO
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa jiwe la Msingi kuzindua rasmi stendi ya Mabasi mjini Mbinga Mkoani Ruvuma leo.Rais Kikwete yupo mkoani Ruvuma Katika ziara ya Kikazi kukagua miradi ya maendeleo. 
 Sehemu ya Barabara ya Peramiho -Mbinga yenye urefu wa Kilometa 78 iliyofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Peramiho-Mbinga yenye urefu wa Kilometa 78.

 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Peramiho-Mbinga 78Km huku akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali na balozi wa China nchini.
Mamia ya wakazi wa Mbinga wakifurahia wakati Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa anamshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa Utendaji wake mzuri wa kuwajali wakazi hao kwa kuwajengea miundombinu bora.
 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wa kwanza kulia akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli kabla ya uzinduzi wa barabara ya Peramiho-Mbinga 78km .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katikati akimshukuru balozi wa China nchini aliye kushoto kwake kwa kazi nzuri iliyofanywa na Mkandarasi kutoka China Kampuni ya Synohdro. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia pamoja na Mawaziri wengine waliohudhuria ufunguzi wa barabara hiyo.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu na Mawaziri waliohudhuria katika ufunguzi wa barabara ya Perahimo Mbinga. Picha na Jackson Msangula
RAISI KIKWETE AFANYA MAENDELEO KUSINI MWA TANZANIA RAISI KIKWETE AFANYA MAENDELEO KUSINI MWA TANZANIA Reviewed by habari motto on 9:46 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.