Results for "siasa"

Naibu Waziri Wa Elimu Afafanua Utaratibu Wa Kupata Cheti Mbadala

9:50 AM
NAIBU Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia,William OleNasha,amefafanua utaratibu wa kupata cheti mbadala/uthibitisho kwa mtu aliyepoteza cheti ambapo ameeleza kuwa Baraza la Mitihani litafanya kazi hiyo kwa muda usiozidi siku 30.

Ole Nasha aliyasema hayo jana bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini,Cosato Chumi (CCM) lililokuwa likihoji ‘’Je ni utaratibu gani unaotumika pale mtu anapopoteza cheti ili aweze kupata cheti kingine’’?,Je ni unapata cheti halisi au nakala? na ni taratibu gani anatakiwa kuzifuata  mtu ili ombi lake lifanyiwe kazi ipasavyo na bila kucheleweshwa?.

Katika majibu yake Naibu Waziri huyo alieleza kuwa mhitimu aliyepoteza cheti hupatiwa cheti mbadala/uthibitisho wa matokeo kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kuhusu upotevu wa cheti na kupata hati ya upotevu.

Pia  mtu aliyepotelewa na cheti atatakiwa kutangaza gazetini kuhusu upotevu huo  kwa lengo la kuutaarifu umma ili kusaidia kukipata na endapo cheti hakitapatikana hata baada ya kufuata utaratibu huo ,mhitimu atajaza fomu ya ombi la cheti mbadala /uthibitisho wa matokeo na kuiwakilisha Baraza la Mitihani.

‘’Baada ya mhitimu kujaza fomu hiyo Baraza la Mitihani hufanya uchunguzi wa uhalali wa umiliki wa cheti husika na kutoa huduma stahiki ,wahitimu waliofanya mtihani kuanzia Mwaka 2008 ambao vyeti vyao vina picha hupatiwa vyeti mbadala ‘’alisema na kuongeza kuwa

“Na waliofanya mtihani kabla ya Mwaka 2008 hupatiwa uthibitisho wa matokeo ambao hutumwa kwa waajiri wao au mahali pengine kwa mahitaji yaliyotolewa na mwombaji na kundi hilo halipewi cheti mbadala’’

Alisema cheti mbadala kinachotolewa ni cheti halisi ambacho huongezwa maandishi yanayosomeka ’DUBLICATE’ kuonyesha kuwa cheti hicho kimetolewa mara ya pili.
Naibu Waziri Wa Elimu Afafanua Utaratibu Wa Kupata Cheti Mbadala Naibu Waziri Wa Elimu Afafanua Utaratibu Wa Kupata Cheti Mbadala Reviewed by habari motto on 9:50 AM Rating: 5

Hili Ni Tamko La CHADEMA Baada Ya Kuzuiwa Kufanya Kongamano

6:55 AM

CHADEMA walikutana na Waandishi wa Habari na kutoa tamko lao baada ya kuzuiwa na Jeshi la Polisi Geita kufanya Kongamano kumuenzi aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.
Akizungumza baada ya zuio hilo mmoja wa wanachama wa CHADEMA, Dr. Mussa Mdede ambaye alikuwa mmoja wa watoa mada katika Kongamano hilo, alisema kitendo cha Polisi kuzuia Kongamano hilo ni kukiuka sheria.
>>>”Kongamano ambalo limezuiwa ni shughuli ya ndani ambayo kimsingi Sheria ya Vyama vya Siasa inatulinda. Kimsingi ni Kongamano ambalo lilikuwa halali na tunapofanya Kongamano la ndani hatuhitaji ulinzi wa Jeshi la Polisi.
“Jeshi la Polisi linahitajika kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mikutano ya hadhara, ndivyo Sheria Namba 5 ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1995 inavyosema, si vinginevyo. Kitu ambacho wamekifanya kipo kunyume na Sheria.”
Aidha, Mdede amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kuwakumbusha Askari Polisi majukumu yao kwa kuwa siku za hivi karibuni wanatumika kisiasa.
“CHADEMA tunasema, kwanza tunamwambia IGP Simon Sirro kwamba awakumbushe Askari wake wafanye kazi kwa weledi wasifanye kazi kwa kisiasa. Katika Awamu ya Tano Jeshi la Polisi limekuwa likifanya siasa waziwazi.” – Mussa Mdede.
Hili Ni Tamko La CHADEMA Baada Ya Kuzuiwa Kufanya Kongamano Hili Ni Tamko La CHADEMA  Baada Ya Kuzuiwa Kufanya Kongamano Reviewed by habari motto on 6:55 AM Rating: 5

Maneno Ya Nape Nnauye Kuhusu CCM

10:25 AM

Usiku wa kuamkia jana Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia tiketi ya CCM Nape Moses Nnauye ametumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe wake wa wazi aliyowahi kuandika kipindi cha nyuma kuhusu CCM, lengo likiwa ni kuweka kumbukumbu sawa kwa watu kuhusu CCM.

“Watu wengi wanaamini nimeisaidia sana CCM lakini ukweli ni kuwa CCM imenisaidia sana mimi kuliko mimi nilivyoisaidia, CCM ni SHULE.

“Bahati niliyopata kwa kuwa muenezi CCM ni kufanya kazi na ndg Kinana ni mwema, mzalendo, hodari, uwezo mkubwa, upendo na maarifa mengi” Ameandika Nape
Maneno Ya Nape Nnauye Kuhusu CCM Maneno Ya Nape Nnauye Kuhusu CCM Reviewed by habari motto on 10:25 AM Rating: 5

Hili Ni Agizo La Raisi Kwa Waliopatikata Na Vyeti Feki

10:19 AM
Raisi John Pombe Magufuli
Rais John Magufuli amesema watumishi 9732 waliobainika na vyeti feki wakatwe mshahara wa mwezi huu na wafukuzwe kazi, Kama watakaidi mpaka kufikia Tarehe 15 mwezi Mei  wachukuliwe hatua kwa kufungwa jela miaka saba.

Amesema kwa kuwa watumishi hao wanajijua, hata majina yao yachapishwe kwenye magazeti kwa kuwa wameiibia serikali.

“Hawa ni majambazi, majizi kama yalivyo majizi mengine,” amesema.
Hili Ni Agizo La Raisi Kwa Waliopatikata Na Vyeti Feki Hili Ni Agizo La Raisi Kwa Waliopatikata Na Vyeti Feki Reviewed by habari motto on 10:19 AM Rating: 5

Ni Raila Odinga! Hongereni NASA

6:46 AM





Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya, NASA, umemteua Mhe. Raila Odinga kuwa mgombea Urais na Kalonzo Musyoka kuwa Naibu Rais. Mwezi uliopita nilipokuwa Nairobi nilikutana na kuzungumza na Mhe. Raila kwa Dakika kadhaa kwenye Mkutano wa Vyama vya Kiliberali barani Afrika . Lakini nilipata fursa ya kushiriki naye katika kundi kazi la viongozi wachache kwa siku nzima. Raila alinihakikishia kuwa NASA haitavunjika, leo nashuhudia kauli yake ikiwa ukweli mtupu. NASA has spoken it clearly, it is Raila Odinga! Hongereni NASA!
Ni Raila Odinga! Hongereni NASA Ni Raila Odinga! Hongereni NASA Reviewed by habari motto on 6:46 AM Rating: 5

Live: Maswali na majibu kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma

11:01 AM
Tazama hapa moja kwa moja kutoka Bungeni, Bunge la kumi na moja, kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, kisha maswali ya kawaida kwa Serikali. Bofya hapa kutazama

Live: Maswali na majibu kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma Live: Maswali na majibu kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma Reviewed by habari motto on 11:01 AM Rating: 5

CHADEMA Waijibu CCM

7:55 AM
Baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia msemaji wake Christopher Ole Sendeka kusema kuwa aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa, kuwa si tishio kwa CCM.

Jumamosi ya Oktoba, 29 Chadema imejibu kuwa Lowassa pamoja na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) utaendelea kuwa tishio kwa chama hicho na kwamba CCM ijiandae kuachia madaraka mwaka 2020 kwa kuwa imejipanga kuchukua dola.

Mkuu wa Idara ya Uenezi Chadema Taifa, Hemed Ali wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam amesema Lowassa ni tishio kwa kuwa alipokihama chama hicho aliacha mpasuko na kudai kuwa aliondoka na nguvu ya chama hicho.

“CCM wana homa kubwa iitwayo Lowassaphobia na ndio maana imeacha kuendelea na shughuli zao na kumuandama Mjumbe wa kamati kuu wa chama chetu Lowassa. Kimsingi mchakato wa kumpata Mgombea Urais na Mgombea mwenza wa chama chetu ulikuwa wa kidemokrasia kwa mujibu wa katiba yetu ambapo ibara (7.7.16 (a) kamati kuu inapewa mamlaka ya kuwafanyia utafiti wagombea Urais wa chama chetu na kupeleka ripoti Baraza kuu,

“Baraza kuu la chama kwa mujibu wa katiba ( 7.7. 13 (a)) inapendekeza majina ya wagombea au mgombea aliejitokeza na hatimae kwa mujibu wa katiba (7.7.10 (c)) Mkutano mkuu wa chama utachagua mgombea Urais na Mgombea Mwenza,” amesema na kuongeza.

” Lowassa alipitia hatua zote kama mwanachama halali wa CHADEMA mwenye haki sawa na mwanachama yeyote kwa mujibu wa katiba (5.1) na (5.2) kimatendo na kiimani kwa kufuata katiba , nilitaraji Sendeka aeleze kile kiini macho cha kumchagua Ndugu Magufuli Dodoma kuwa Mgombea wao huku wenyewe kwa wenyewe wakipinga mchakato wa kumpata usiofuata katiba na kanuni za chama hicho kama walivyojitenga na uamuzi huo baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ile kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa maamuzi ndani ya vikao.”

Amedai kuwa, Kamati Kuu yao ilipasuka katikati baina ya wajumbe wake na kudai kuwa wajumbe waliokuwa wanamuunga mkono Lowassa, wengi wao hawakuchaguliwa kushika nyadhifa serikalini .

“Ni kawaida ya CCM kuchafua mtu ambae atakua na msimamo na nia ya kulivusha taifa , Wamefanya hivyo kwa viongozi wetu wa chama na watu binafsi hivyo hatushangai walivyo mshambulia Lowassa akiwa ndani ya CCM na hata Sasa CHADEMA. Sendeka amesema kuwa yupo kiongozi ndani ya chama chetu aliyepata dola milioni 15 takribani bilioni 33 eti apangesafu ya uongozi ndani ya chama,

“Kiuhalisia na kwa hesabu ndogo tu ni kuwa pesa hiyo si tuu kuwa inatosha kwa ajili ya kupanga uongozi ndani ya chama bali ni inatosha kwa ushindi wa mitaa, kata na halmashauri , ubunge na urais hivyo wakati anataja tarakimu hizo ajue na michanganuo ya kimahesabu badala ya kuwa mkurupukaji na ningemuelewa kama angekuja hadharani kuaga rasmi kwa niaba ya chama chake na kutupisha kuwatumikia watanzania kuliko kuongea uongo,”amesema.
CHADEMA Waijibu CCM CHADEMA Waijibu CCM Reviewed by habari motto on 7:55 AM Rating: 5

Rais Magufuli Amkumbuka Augustine Mrema Na Kumteua Kuwa Mwenyekiti Bodi Ya Parole

7:39 AM
Augustine-Mrema-Mwenyekiti-Bodi-Ya Parole
Augustine-Mrema-Mwenyekiti-Bodi-Ya Parole
Ahadi ni deni. Kama utakumbuka wakati wa kampeni za Urais mwaka jana, Rais Magufuli alipofika jimboni Vunjo mkoani Kilimanjaro alikutana na Waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Augustine Lyatonga Mrema ambaye kwa miaka mingi alihamia kambi ya upinzani.
Mambo yalikuwa hayaendi vizuri kwa Mrema. Nafasi ya ubunge aliyokuwa nayo katika jimbo la Vunjo kupitia chama chake cha TLP ilikuwa hatarini. Kambi ya UKAWA ilikuwa ikitishia kulichukua jimbo la Vunjo kupitia chama cha NCCR-Mageuzi na mgombea wake, James Mbatia.
Mrema aliona mbali. Akatamka wazi kumuunga mkono mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dr. J.P.Magufuli ambaye alikwenda kushinda Urais. Katika mkutano ule wa Vunjo, Mrema alielezea kwamba bado yupo fit na anahitaji “kazi”. Dr.Magufuli alikuwa muungwana na kumwahidi kumfikiria Bw.Augustine Mrema ambaye aliwahi kutamba katika upinzani pengine kushinda wanasiasa wengi wengine.

Yaelekea Dr.Magufuli hakuwa muungwana asiye na nia ya kutimiza ahadi.Kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, akiwemo Bw.Augustine Mrema ambaye amemteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
Mhe. Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.

Pia Dr.Magufuli amefanya teuzi zingine mbalimbali kama zifuatazo;
Prof. William R. Mahalu– Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.

Prof. Mohamed Janabi-Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

Prof. Angelo Mtitu Mapunda-Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

Bi. Sengiro Mulebya-Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Bw. Oliva Joseph Mhaiki-Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa-Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Dkt. Charles Rukiko Majinge-Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.


Dkt. Julius David Mwaiselage-Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Rais Magufuli Amkumbuka Augustine Mrema Na Kumteua Kuwa Mwenyekiti Bodi Ya Parole Rais Magufuli Amkumbuka Augustine Mrema Na Kumteua Kuwa Mwenyekiti Bodi Ya Parole Reviewed by habari motto on 7:39 AM Rating: 5

Rais Magufuli Amteua Mkuu Wa Wilaya Ya Kongwa Mkoani Dodoma

7:23 PM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi anachukua nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. John Ernest Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.

Uhamisho wa Bw. John Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya Mhe. Rais Magufuli kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi.

Bw. Deogratius John Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Julai, 2016
Rais Magufuli Amteua Mkuu Wa Wilaya Ya Kongwa Mkoani Dodoma Rais Magufuli Amteua Mkuu Wa Wilaya Ya Kongwa Mkoani Dodoma Reviewed by habari motto on 7:23 PM Rating: 5

Kinana Ataka Wabunge CCM Wafuate Moto wa Ukawa

6:29 PM
Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamefunguliwa milango na chama chao kuhakikisha wanaibana serikali itekeleze ilani na kuziba mianya ya ubadhirifu wa fedha za umma.

Hatua hiyo imelenga kuhakikisha kwamba wapinzani wanakosa hoja za kuidhoofisha serikali bungeni.

Wabunge wa vyama vya upinzani wamekuwa wakiibana serikali kwa kuikosoa na kufichua mianya yote ya ufisadi inayofanywa viongozi mbalimbali waliopo madarakani.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ndiye aliyetoa rungu hilo katika semina ya siku mbili ya wabunge wa chama hicho iliyofanyika Makao Makuu ya CCM mjini hapa jana.

Kikao hicho kilianza juzi chini ya Kinana, na kwa siku ya kwanza kinadaiwa kilikuwa na ajenda tatu; wajibu wa wabunge wa CCM kwa serikali, tathmini ya uchaguzi mkuu na mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama, huku siku ya pili ambayo ni jana kulikuwa na ajenda moja ya Ilani ya chama hicho na namna ya kuitekeleza.

Mbali na hilo, Kinana aliwataka wabunge kuhakikisha wanapambana ili sheria zote kandamizi kwa wananchi zifutwe, jambo litakalowawekea wananchi mazingira mazuri.

Hata hivyo, katika ajenda ya wajibu wa wabunge wa CCM kwa serikali kwenye mfumo wa vyama vingi, iliwasilishwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, ambayo ilibainisha namna ambavyo kambi ya upinzani bungeni ilivyo na mkakati wa kuidhoofisha serikali ili katika uchaguzi wao wachukue madaraka.

Katika mada hiyo, Msekwa aliwataka wabunge wa CCM kutafuta mbinu za kujilinda na kujitetea ili wapinzani wakose hoja za kuidhoofisha serikali.

"Wajibu wa kila mbunge wa CCM ni kuiwezesha serikali ya chama chake kutekeleza majukumu yaliyoahidiwa katika ilani ya uchaguzi kwa kupitisha miswada ya sheria inayowasilishwa na serikali kwa madhumuni hayo, ikiwamo bajeti zinazopendekezwa na serikali," ilieleza sehemu ya mada hiyo iliyowasilishwa na Msekwa.

Aidha, Msekwa alisema ni halali kabisa kwa wabunge wa CCM kutumia wingi wao kuidhinisha maombi ya bajeti yanayopelekwa bungeni na serikali ili kuiwezesha kutimiza ahadi zilizotolewa kwa wananchi kupitia ilani ya uchaguzi ya Chama.

Kwa upande wa Kinana, aliwataka wabunge hao 'kufinya' hoja ili isiwe kazi ya wapinzani kuchokonoa moto, jambo litakalowafanya kukosa mwanya wa kuilipua serikali.

"Katibu Mkuu katutaka tufanye kazi kama wabunge, tutetee na wananchi na amesema hakuna kamati kuu iliyoagiza wabunge wasiibane serikali, hasa Kinana anachotaka ni nchi hii kufanikiwa kwa kuziba mianya yote ya ubadhirifu wa fedha za umma na kutatua matatizo yanayowakabili wananchi ili wapinzani wakose hoja," walisema baadhi ya wabunge katika semina hiyo.

Kuhusu kufuta kodi ambazo ni mzigo kwa wananchi, wabunge hao wamejadili na kukubaliana  namna ya kuhakikisha wanaondoa kodi mzigo ambazo ni kero kwa wananchi na kandamizi.

Inadaiwa miongoni mwa kodi ambazo ni mzigo kwa wananchi ni kodi ya Ewura ambayo ina kodi ya ukaguzi, uthibiti ambazo ni   kitu kimoja, hivyo zitachambuliwa na kufutwa ili kuleta unafuu kwa wananchi, hivyo kusaidia hata bei ya mafuta kushuka.

Hata hivyo, wakichangia mijadala baadhi ya wabunge wametaka kuwapo na bandari ya nchi kavu mkoani Dodoma kwa kuwa ni mkoa wa kati ambao ni rahisi kwa kila sehemu kuchukulia mizigo yake hata nchi za jirani.

Aidha, wabunge wengi wametaka upatikanaji wa maji mijini na vijijini huku wengi wakisema yasipopatikana itakuwa ni hati hati kwa CCM kushinda uchaguzi ujao kwa hofu ya kusulubiwa na wapigakura wanawake ambao hiyo ndiyo kero yao kubwa.

Kuhusu sheria kandamizi, Kinana aliwaambia wabunge hao kuwa sheria zingine za mkoloni mpaka sasa zipo na kwamba hazimsaidii mwananchi wa kawaida.

Kadhalika katika kikao hicho Kinana alisema vyombo vya habari vinapendwa lakini wabunge hao wajitahidi kutunga sheria hasa itakayotetea maslahi kwa waandishi wa habari.

"Katibu Mkuu anasema ikiwekwa sheria ya aina hiyo, waandishi kulipwa vizuri hasa kwenye vyombo binafsi, magazeti mengine yatakufa yenyewe huna haja ya kugombana nayo, maana mwandishi anatakiwa aajiriwe na apate haki zake...hii itafanya kusiwe na uholela holela wa kusajili magazeti wakati mmiliki hana uwezo wa kuajiri na matokeo yake utakuta gazeti habari zake nyingi na mwandishi wetu," alisema mmoja wa wabunge ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.

Alipotakiwa kuzungumzia kuhusu semina hiyo, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama, alisema hataweza kuzungumzia chochote kwa kuwa semina hiyo imeratibiwa na chama hivyo anayetakiwa kuzungumza ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Kwa upande wake. Nnauye alisema: "Hatujatoa taarifa kwa umma juu ya semina na hatujawaambia lolote.
Kinana Ataka Wabunge CCM Wafuate Moto wa Ukawa Kinana Ataka Wabunge CCM Wafuate Moto wa Ukawa Reviewed by habari motto on 6:29 PM Rating: 5

Hatimaye Samwel Sitta Akubali Yaishe Aamua Kustaafu Rasmi Siasa

8:12 AM
Hatimaye mzee Samwel Sitta atangaza kustaafu rasmi siasa, hajasema kama atarudi kijijini kulima kama ilivyo kwa wanasisa wengi ambao Mara nyingi wanapostaafu hutangaza kurudi kijijini na kuwa wakulima, lakini pia kilimo kwanza ilikuwa ndiyo Sera ya chama chake katika Serikali ya awamu iliyopita.

Source: Magazeti ya leo
Hatimaye Samwel Sitta Akubali Yaishe Aamua Kustaafu Rasmi Siasa Hatimaye Samwel Sitta Akubali Yaishe Aamua Kustaafu Rasmi Siasa Reviewed by habari motto on 8:12 AM Rating: 5

Haya Ni Majipu Matano (5) Sugu Anayotakiwa Kuyatumbua Rais Magufuli

5:27 PM

Wasomi, wanasiasa na watu kutoka makundi mengine ya jamii wamesema Rais John Magufuli atapimwa katika miaka mitano ijayo kwa mambo makubwa matano yaliyoonekana kuwa ‘majipu sugu’ na changamoto kwa mtangulizi wake, Jakaya Kikwete.


Majipu (mambo matano) hayo ni;
1.Kudhibiti mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya. 
2.Kukomesha rushwa na ufisadi. 
3.Kufumua mtandao wa majangili. 
4.Kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana na 
5.Kuua ‘mchwa’ unaoitafuna fedha za Serikali.


Maoni yaliyotolewa na wasomi, wanasiasa na wananchi wa kawaida yanaonyesha kwamba kufanikiwa kwake kutategemea aina ya ushirikiano atakaoupata kutoka kwa wananchi na wanasiasa na hasa wa kutoka chama chake.


Mhadhiri kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Elijah Kondi alisema Dk Magufuli anahitaji kupigana vita kali kufanikisha ahadi zake na akaonya kuwa hawezi kusimama mwenyewe na kushinda vita hiyo bila kuungwa mkono na wananchi hasa chama chake, CCM.


“Vigogo wengi ndani ya chama chake wamekuwa wakihusishwa na majipu hayo. Hivyo, kufanikisha azma hiyo, kutategemea wingi wa wanaCCM watakaomuunga mkono, lakini kama watakuwa wachache, itakuwa vigumu. Hilo hata yeye (Magufuli) analifahamu ndiyo maana anasema vita hiyo ni kubwa,” alisema Kondi.


Pia, alisema kushughulikia mtandao wa dawa za kulevya, ujangili na kuanzisha mahakama ya mafisadi kutategemea ushirikiano atakaoupata kutoka kwa watendaji na baraza lake la mawaziri.


Kondi alisema kushindwa kwa Rais mstaafu Kikwete katika mambo hayo kulitokana na udhaifu wa baraza lake la mawaziri na watendaji wa taasisi za Serikali. 

“Rais anaweza kuwa na dhamira njema, lakini je, atapata mawaziri wazuri wa kumsaidia? Hao mawaziri watakuwa na ari gani ya kushiriki vita hiyo?” alihoji na kuongeza:


“Kwa sababu anaweza kuanzisha mahakama ya mafisadi lakini ikashindwa kuonyesha uhai kama anavyotarajia. 

"Jaribio la kutumbua majipu hayo itategemea ushirikiano wa chama chake, mawaziri atakaowateua na watendaji wa Serikali.”


Mhadhiri wa Idara ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda alisema kilichosababisha marais waliomtangulia kushindwa kutumbua majipu hayo ni utofauti mkubwa ulioonekana kati yao.


“Utofauti katika uwezo wao ukoje? Dhamira zao zinatofautianaje? Lakini hata kiwango cha utashi wa kushughulikia hilo jipu kinatofautianaje na uongozi uliopita. Ukisikiliza kauli ya Rais Magufuli anaonyesha matumaini,” alisema Mbunda.


Meneja wa Soko la Machinga Complex, Nyamsukura Masondore alisema kupandishwa mahakamani kwa vigogo wa Serikali katika kashfa ya EPA ni sehemu ya juhudi zilizoonekana kwa uongozi uliopita.

“Hivyo, hakuna kitakachoshindikana kwa Rais Magufuli endapo watendaji wa chini watakuwa tayari kubadilika na kutoa ushirikiano wa kushinda vita ya majipu hayo,” anasema


Profesa George Shumbusho wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema ana imani Rais Magufuli anaweza kushughulikia changamoto hizo sugu ambazo ameziita majipu kutokana na historia ya utendaji wake. 

“Rais Magufuli atafanikiwa kazi hiyo kutokana na historia yake ya kutojihusisha kwa karibu na mtandao wa wafanyabiashara wakubwa hapa nchini na nje,” alisema.


Profesa Shumbusho alisema kuwa endapo ataendelea na msimamo huo, changamoto ya ukwepaji kodi, misamaha ya kodi, biashara haramu ikiwamo ya dawa za kulevya zitakoma.


Dawa za kulevya
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alinukuliwa Agosti 2013 bungeni akikiri kuwapo baadhi ya majina ya wabunge miongoni mwa watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini alisema Serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa haraka.


Hata Kikwete wakati wa awamu yake ya kwanza, aliwahi kusema anawajua wauza dawa za kulevya lakini tatizo hilo limeendelea kuwa sugu hadi anamaliza kipindi chake cha pili.


Mwaka huohuo, Umoja wa Mataifa (UN) ulitoa ripoti inayobainisha Tanzania kuwa kinara wa kupitisha dawa za kulevya katika nchi za Afrika Mashariki. 

Kuanzia 2010 hadi 2013 ilipitisha tani 64 za dawa za kulevya aina ya heroine na ikitaja Bandari ya Tanga kuwa njia kuu ya upitishaji huo.


Je, baada ya kuanzishwa kwa Sheria ya Kupambana na Kuthibiti Dawa za Kulevya ya mwaka 2015, Rais Magufuli ataweza kusimamia mapambano dhidi ya vinara wa biashara hiyo?


Ujangili wa tembo
Kabla ya kuondoka madarakani, Rais Kikwete aliwahi kunukuliwa Februari 2014 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) akikiri kuwatambua majangili 40 wa meno ya tembo na kwamba kiongozi wao anaishi Arusha. Pia, alikiri kuwa vita dhidi ya ujangili ni tatizo sugu.


Vilevile, Mei 2014, ripoti iliyoitwa ‘Ivory’s Curse: The Militarization and Professionalization of Poaching in Africa’, ilieleza kuwa tangu mwaka 2000 wizara inayohusika na utalii ilikuwa imetawaliwa na kashfa za rushwa. Ripoti hiyo ilifafanua jinsi vikundi mbalimbali vya waasi barani Afrika vinavyoendesha shughuli za ujangili.

Katiba ya Jaji Warioba
Oktoba 2014, Bunge Maalumu la Katiba lilipitisha Katiba Inayopendekezwa kwa tofauti ya kura mbili tu zilizonusuru kukwamisha Katiba hiyo kwa upande wa Zanzibar. Mvutano kati ya CCM na upinzani wakati wa upitishaji wa Katiba hiyo ulitokana na tofauti za itikadi na sera kuhusu muundo wa Muungano.

Wajumbe wa CCM walipigania sera yao ya muungano wa Serikali mbili wakati wenzao wa wapinzani walipigania muundo uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji mstaafu, Joseph Warioba wa Serikali Tatu. Hadi sasa haijapigiwa kura ya maoni.
‘Mchwa’ Serikalini
Kila mwaka, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amekuwa akikagua na kuibua ufisadi mkubwa katika Serikali Kuu, Idara za Serikali na mashirika ya umma. 
Ripoti iliyotolewa mwaka huu inaonyesha ukaguzi ulifanyika katika taasisi 176 za Serikali kuu, halmashauri 163 na mashirika ya umma 109. 
Kikwete amewahi kupangua baraza lake la mawaziri na kuwafukuza kazi watendaji lakini bado ufisadi umeendelea katika nyanja tofauti kama ulipaji mishahara hewa na ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo.
Mahakama ya mafisadi
Moja ya ahadi kubwa za Rais Magufuli wakati wa kampeni na Novemba 20 alipozindua Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano ni kuanzisha Mahakama Maalumu ya kushughulikia mafisadi.
Tayari mchakato umeanza lakini wachambuzi wanasema kinachotakiwa ni kuipa meno Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili iweze kufanya kazi zake bila kuogopa mtu.

Haya Ni Majipu Matano (5) Sugu Anayotakiwa Kuyatumbua Rais Magufuli Haya Ni Majipu Matano (5) Sugu Anayotakiwa Kuyatumbua Rais Magufuli Reviewed by habari motto on 5:27 PM Rating: 5

Baraza la Mawaziri Kenya, labadilishwa

7:02 AM
Rais wa Kenya amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri, na kuwaacha wote wizara zao zilizotajwa katika ufisadi.
Rais Uhuru Kenyatta amechukua hatua hiyo siku moja tu baada ya kutangaza ufisadi kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa. Rais ameahidi kufanya mabadiliko zaidi katika afisi yake hivi karibuni.
Katika hotuba ilioonyeshwa kwa njia ya Televisheni,Rais Uhuru Kenyatta ameongeza idadi ya wizara kutoka kumi na tisa hadi ishirini na kuongeza idara mpya chini ya wizara mbalimbali katika kile alichosema ni kusaidia mawaziri kutekeleza majukumu yao bora zaidi.
Idara hizo zimeongezwa kutoka ishirini na sita hadi arobaini na moja.
Rais Kenyatta amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri baada ya mawaziri sita kulazimika kujiondoa kutokana na wizara walizosimamia kuhusishwa na ufisadi huku wawili kati yao wakikabiliwa na kesi mahakamani.
Ni Mabadiliko yaliyotarajiwa hasa baada ya hatua ya aliyekuwa waziri wa Ugatuzi Anne Waiguru kujihuzulu mwishoni mwa juma kutokana na kile alichosema ni ushauri wa daktari wake- baada ya usumbufu aliopata wizara yake ilipohusishwa na sakata kadhaa za ufisadi.
Kwa mujibu wa katiba idadi ya mawaziri inapaswa kuwa kati ya kumi na wanne na ishirini na wawili- na hivyo kujiuzulu kwake kulisababisha idadi hiyo kupungua hadi kumi na tatu.
Baraza jipya la mawaziri linajumuisha wanawake wanne na wanaume kumi na sita.
Baadhi ya mawaziri wamesalia katika nafasi zao huku wengine wapya wakiteuliwa kuchukua nafasi za mawaziri waliohusishwa na ufisadi.
Hatua itakayofuata sasa ni kwa mawaziri wapya kuchunguzwa na kamati ya bunge kabla ya kuidhinishwa kikamilifu.
Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imekuwa ikikabiliwa na changamo ya ufisadi katika wizara kadhaa na kumekuwepo shinikizo sio tu kutoka kwa wananchi lakini pia kutoka kwa mashirika ya kijamii,viongozi wa upinzani na hata mabalozi wa nchi za kigeni kutaka hatua zichukuliwe.
Baraza la Mawaziri Kenya, labadilishwa Baraza la Mawaziri Kenya, labadilishwa Reviewed by habari motto on 7:02 AM Rating: 5

Waziri Mkuu Ataka Apewe Sababu Kwa Nini Mabasi yaendayo Haraka Hayajaanza kazi Hadi Leo......Pia Kaagiza Kila Mgurugenzi Awe na Nakala ya Hotuba ya Rais

7:00 AM

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wakurugenzi wa vitengo na wakuu wa taasisi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) wapate nakala ya hansard ya hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuzindua Bunge la 11, waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha.

“Katibu Mkuu hakikisha umepata hansard ya hotuba ya Mheshimiwa Rais wakati akizindua Bunge na uhakikishe kila mkurugenzi ana nakala na kila mmoja wenu lazima ahakikishe anafanyia maeneo ambayo Mheshimiwa Rais ameyaainisha. Ni lazima tuelewane ni nini tunapaswa tufanye,” alisema.

Ametoa kauli hiyo jana (JANA) mchana (Jumanne, Novemba 24, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) kwenye mkutano uliofanyika ofisi ndogo ya TAMISEMI, barabara ya Kivukoni, jijini Dar es Salaam.

“Ninatamani kuona mabadiliko ya utendaji kazi Serikalini katika kipindi kifupi. Natamani kila mmoja asiridhike na uzembe unaofanywa huku chini. Ni nyote ni wataalamu, kwa hiyo mnapaswa kudhirisha elimu yenu na ujuzi mlionao,” aliwasisitizia Wakurugenzi hao.

Alisema kila mkurugenzi na mkuu wa taasisi anapaswa kuongeza usimamizi na ufuatiliaji wa kazi kwenye sekta yake kwani hilo litasaidia kukidhi matarajio ya Watanzania ya kuona mabadiliko ya utendaji kazi kwenye Serikali ya Awamu ya Tano.
 
“Ninyi wakurugenzi siyo desk officers bali ni field officers. Nataka muweke utaratibu wa kwenda vijijini mkasimamie watu wenu, pia mhimize uadilifu, uaminifu na weledi wa kazi,” alisisitiza.

“Mambo ninayotaka mhimize watendaji waliopo chini yenu ni pamoja na haya yafuatayo: muda wa kuripoti kazini uzingatiwe, muda wa kukaa kazini uzingatiwe, utokaji kazini kwenda kwenye chai na chakula cha mchana udhibitiwe, na mipango na malengo ya kazi kwa siku ni lazima yafikiwe,” alisema.

“Tunataka kujua mtumishi amefanya nini tangu alipoingia ofisini. Suala siyo kukaa tu ofisini, kwani kuna mtu anakaa ofisini, hajaenda hata kunywa chai lakini ukiuliza amefanya nini hupati jibu la kueleweka. Sisi kama vongozi wao ni lazima tujue wanafanya kazi gani wanapokuwa maofisini,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa ameitisha kikao ofisini kwake kesho (LEO )saa 4 asubuhi akitaka kupatiwa taarifa ni kwa nini mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) haujaanza kazi hadi sasa.
 
 “Kesho( LEO)  saa 4 asubuhi Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mkuu DART na watendaji wako mje ofisini. Nataka kupata maelezo ni kwa nini mabasi hayajaanza kazi hadi leo, je ni lini yataanza kazi, je ni nani anakwamisha. Na hata kama ni sheria, ni kwa nini tusiziharmonise ili kuondoa hivyo vikwazo,?” alihoji Waziri Mkuu.

“Ninataka kupata haya maelezo kwa sababu Watanzania na hasa wana-Dar es salaam, wamesubiri kwa muda kuona mradi ukianza kazi ili uondoe kero ya usafiri. Wao wanajua anayehusika ni TAMISEMI,”aliongeza.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na watumishi na viongozi wa TAMISEMI, Katibu Mkuu wa OWM-TAMISEMI, Bw. Jumanne Sagini alimweleza baadhi ya mafanikio na changamoto ambazo wizara hiyo imekabiliana nazo katika utendaji wake wa kazi.

Kuhusu ujenzi wa vyumba vya maabara kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji wa masomo ya sayansi, Bw. Sagini alisema vyumba hivyo vimeongezeka kutoka 247 mwaka 2005/2006 na kufikia 6,161 mwaka 2014/2015. Pia alisema vyumba 4,228 viko kwenye hatua za kukamilika ujenzi wake.

Kuhusu utengaji wa madirisha ya kuhudumia makundi yenye msamaha kama wazee na watu wenye ulemavu hospitalini na kwenye vituo vya afya, Katibu Mkuu alisema nayo yameongezeka kutoka madirisha 5,074 mwaka 2010 na kufikia 7,903 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 55.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM

JUMANNE, NOVEMBA 24, 2015.
Waziri Mkuu Ataka Apewe Sababu Kwa Nini Mabasi yaendayo Haraka Hayajaanza kazi Hadi Leo......Pia Kaagiza Kila Mgurugenzi Awe na Nakala ya Hotuba ya Rais Waziri Mkuu Ataka Apewe Sababu Kwa Nini Mabasi yaendayo Haraka Hayajaanza kazi Hadi Leo......Pia Kaagiza Kila Mgurugenzi Awe na Nakala ya Hotuba ya Rais Reviewed by habari motto on 7:00 AM Rating: 5

Magufuli Apeta Mitandao Ya Kijamii Kenya

12:45 PM
Uchapakazi wa Rais Dkt John Magufuli unatuma ujumbe si kwa maafisa wa Tanzania pekee, bali na nchi za jirani pia na kuwaacha viongozi wa nchi hizo kwenye wakati mgumu.
Kenya ambayo imekuwa ikifuatilia siasa za Tanzania tangu wakati wa kampeni, imeonesha kupenda mbinu za Magufuli na wananchi wake wanatamani mtu kama yeye.
Kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani, Magufuli amefanya mambo makubwa na wananchi wamependa.
Ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali ya Muhimbili ilifichua uovu mwingi na kupelekea kufutwa kwa bodi ya wakurugenzi wa hospitali hiyo na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk Hussein Kidanto.
Ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za serikali kwaajili ya kugharamia safari za nje za viongozi wa nchi, Magufuli aliamua kuzisitisha mara moja.
Dkt Magufuli pia alielekeza kiasi cha shilingi milioni 225 zilichangwa kwaajili ya kugharamia hafla ya wabunge kupongezana mjini Dodoma zipelekwe kwenda kununua vitanda. Badala yake shilingi milioni 15 pekee zilitumika kwaajili ya sherehe hiyo.
Siku chache baadaye vitanda hivyo na vifaa vingine vilinunuliwa na kupelekwa Muhimbili.
Jumatatu hii Magufuli alitangaza kuondoa sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru December 9 na fedha za maandalizi hayo zitumike kwa mambo mengine muhimu.
Hayo na mambo mengine yamefanya Dkt Magufuli atrend nchini Kenya.
Hizi ni baadhi ya tweets za wakenya:

Magufuli Apeta Mitandao Ya Kijamii Kenya Magufuli Apeta Mitandao Ya Kijamii Kenya Reviewed by habari motto on 12:45 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.